Good Father
JF-Expert Member
- Feb 28, 2014
- 10,272
- 18,334
Wakuu nimeona taarifa ITV ikionesha idadi kubwa ya ng'ombe waliokamatwa na watumishi wa hifadhi za taifa huko Rukwa, hali inasikitisha sana, wahusika wameonesha uzembe wa hali ya juu, wanashuhudia mifugo ikikosa huduma mpaka inafia zizini, wanaendelea kuongeza mifugo mingine mipya kwenye zizi lenye mizoga!
Wanaendelea kulinda mifugo ambayo hata kutembea haiwezi kwa sababu ya njaa.
Suala hili halipaswi kuachwa hivi hivi, kama tuliweza kupaza sauti kuhusu suala la vifaranga vilivyoteketezwa Arusha basi hili ni baya zaidi kuliko la Arusha kwa maana lile la Arusha wahusika walijibu kwamba ni sheria zipo na zinaruhusu kitu hicho. Japo kwa moyo wa kibinadamu ilitia huzuni sana.
Watumishi wa hifadhi wapo wamenenepa kabisa na afya zao safi eti wanalinda mifugo iliyokufa na mingine inaendelea kufa.
Sikatai wananchi waliingia maeneo ya hifadhi lakini kwanini hao ng'ombe wasingeendelea kupatiwa huduma? Au wangeuzwa kwa taratibu zilizopo.
Waziri kaamua mifugo irudishwe kwa wamiliki, sasa vipi kuhusu hiyo hasara? Je wizara au nchi imefaidika vipi kwa kushikiria hiyo mifugo kwa zaidi ya mwaka mzima? Mwananchi kapata hasara zaidi, serikali imemtia hasara mwananchi.
Ninachoweza kusema ni kwamba hawa watumishi wa hifadhi ni watu wanastahili kuwajibishwa, siwaombei mabaya ila hawa walitakiwa wafukuzwe kazi na taratibu ziangaliwe ili kufikishwa mahakamani kwa kuiingizia hasara serikali na wananchi wake.
Tuachane na wale wakurugenzi walioshindwa kujua takwimu, hawa wahifadhi wanastahili ile adhabu ya kupumzishwa na kusubiri kupangiwa kazi nyingine na wakati huo wakisubiri kupangiwa kazi nyingine basi wangeendelea kujibu kesi zao mahakamani. Huu ni uzembe wa hali ya juu.