Mhe. Rais si vibaya katika hili sakata la madini ukawapongeza Wapinzani

ponopono

JF-Expert Member
Dec 21, 2016
483
500
Ni jambo lililowazi na hakuna mwenye utashi asiyejua jinsi hawa jamaa tunaowaita wapinzani walivyosimama kideti kupinga hii miswada ya dharura iliyopitisha wizi huu wa kutisha wa madini yetu pia na gesi.

Hakuna asiyejus jinsi akina Zitto na mnyika walivyoadhibiwa na wengine kuwekwa rumande na kuitwa kila jina baya na wabunge wa ccm. Hakuna asiyejua wabunge wa upinzanj wengi wao walivyofukuzwa bungeni na waliobaki kuamua kulisusia bungd ili tu wasishiriki kwenye uovu huu ambao ccm iliufanya kwa taifa hili.

Ninachokuomba mhe.Rais onyesha tuu moyo wa ku appreciate hawa jamaa wala halitakupunguzia umaarufu ulionza kuupata ndani na nje ya nchi hii. Ukizid kukomaa kutaka waonekane ndio wasaliti watu wanaokumbuka udhalikishaji wapinzani waliofanyiwa na bunge la makinda kwa ajili ya kutetea rasilimali hizi hawatakuelewa kabisa.

Na badala yake watasema unapiga siasa tuu. Wewe ni mcha Mungu na ulisema mwenyewe jambo hili halina siasa basi na wewe usiingize siasa humu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom