Mhe. Rais, Nikupongeze kwa kuona kuwa MRISHO GAMBO hafai kuwa Katibu Mkuu UVCCM...

Meitinyiku L. Robinson

JF-Expert Member
Aug 29, 2011
412
90
Ikiwapendeza wadau;

Katika Mkutano Mkuu wa Vijana na ule Mkutano Mkuu wa CCM Taifa uliomalizika wiki iliyopita palizuka maneno mengi jambo ambalo liliwapelekea Makatibu wa Vijana wa Mikoa kukutana kwa faragha ili kulijadili jambo hili. Jambo hili si siri bali ulikuwa ni mpango wa Mhe Raisi ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa kufikiri ama kushurutishwa na Prince kumteua Mrisho Gambo (DC) Korogwe kuwa Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa.

Tetesi hizi ziliwapa taabu sana Makatibu wa Mikoa (wale wa Jumuiya husika) kwa kuona ugumu ama namna ambavyo heshima na umoja wa Jumuiya unavyoelekea kuanguka kwa kukabidhiwa Mtendaji ambaye si tu kwamba hana uwezo bali hana ushirikiano na mtu yeyote ndani ya Jumuiya hiyo jambo ambalo lingempelekea yeye kusimama kama yatima.

Ila katika hili Raisi ameonekana kutumuia busara ya hali ya juu hasa baada ya kujua kuwa muhusika alianza kujigamba akidhani na kuamini kuwa alichoahidiwa yatakuwa ila kinyume na hapo Raisi aligundua namna ambavyo sifa na utoto unavyomsumbua muhusika na namna ambavyo angeleta tafrani ndani ya Jumuiya.

Kipekee tunamshukuru sana Mhe Raisi kwa namna alivyolitatua hili na kwa namna ambavyo ameona kuwa sasa yamfaa yeye kuamua mambo ambayo yatasaidia si tu Jumuiya tulizo nazo bali Chama kwa ujumla wake, hongera sana Mhe Raisi.

Lakini kipekee nimtake huyo muhusika pamoja na swaiba wake wajue kwamba Chama pamoja na Nchi haiongozwi kwa maneno ya mitaani bali kwa STK's yani (Sheria, Taratibu, na Kanuni) na kama hawataki basi waache.

Mwisho niendelee na ntaendelea kumpongeza Mhe. Martine Shigela (MNEC, SG wa UVCCM (T) kwa umakini, busara, heshima, bidii, mshikamano na umoja ambao ameuonesha na kuendelea kuuonesha ndani ya Jumuiya jambo limemgusa Raisi na kuona kuwa hana haja ya kuteua mtu mwingina kurithi nafasi hiyo. Nasi kama Watendaji wa Jumuiya husika tunamwaidi Raisi ushirikiano na mapenzi yaliyotukuka katika kukijenga Chama chetu na Nchi kwa ujumla.........
 
Hivi umri wa kuwa UVCCM ni miaka mingapi? Maana ka- Martine Shigela nakafahamu tokea kakiwa pale UDSM akikokotwa na mwenzie KAPENJAMA (sijui kachinjiwa wapi huyu maana alijidai yupo kwa Lowassa)......hat aakiwa UDSM (1999-2002) tayari kalikuwa kajeba, sasa leo hii 100 years after bado ni kijana tu wa UVCCM? Nina uhakika haka kajamaa ni kazeee

CCM na UVCCM kulikoni??
 
Umri kwa watendaji hauna limit Comrade!!! Na hilo la huko aliko binafsi sina shaka na wala siwezi kumlaumu kwalo manake hilo ndilo fungu alilolichagua of which kila mmoja wetu anaweza kuchagua tatizo ni maelekezo apewayo mtu na mtu atoaye hayo maelekezo pamoja na uwezo wa muhusika....
 
Unampongeza kwa kukataa ushauri wa mwanae? Ajabu sana hii! JKN alimpaka sana yule aliyekuwa akishauriwa ndani ya shuka kumbe kaja mwingine anashauriwa mambo mazito na mtoto? Kweli CCM ni kichekesho
 
Hivi umri wa kuwa UVCCM ni miaka mingapi? Maana ka- Martine Shigela nakafahamu tokea kakiwa pale UDSM akikokotwa na mwenzie KAPENJAMA (sijui kachinjiwa wapi huyu maana alijidai yupo kwa Lowassa)......hat aakiwa UDSM (1999-2002) tayari kalikuwa kajeba, sasa leo hii 100 years after bado ni kijana tu wa UVCCM? Nina uhakika haka kajamaa ni kazeee

CCM na UVCCM kulikoni??

Mkuu mwenyekiti wao naye anajiita Janki sasa hawa wazee wengine nao wanajiita vijana. Shigela ni mtu mzima kabisa na hafai kuwa kwenye kundi la vijana. hawa CCM wakitembea na vibinti vidogo wanajiona vijana:A S angry:
 
Back
Top Bottom