Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,979
Kama wabunge wasio na sifa wataendelea kulipwa fedha za umma na viongozi wakuu wa nchi wasikemee wala kudhibiti huu wizi wa wazi ni vigumu kupambana na wizi wa mali za umma. Kama mwanasiasa atapewa haki na baraka za Serikali kufuja Mali za umma ni vigumu Serikali hiyo kuadhibu Watumishi wa Umma na wafanyabiashara kwa wizi.
Kama CAG ataleta ripoti inayoonyesha wanasiasa walivyotumia fedha za umma vibaya na Serikali ikakaa kimya,lakini Serikali hiyohiyo ikisikia ripoti ya CAG inamtaja Mkurugenzi mara moja mwanasiasa anakimbilia kumsimamisha kazi hii haiwezi kuwa nchi yenye usawa.
Kama hotuba za viongozi wakuu wa nchi zinazotoa mwelekeo zitaacha kutoa maelekezo kuhusu taarifa za watafiti wa Serikali ikiwemo taarifa ya CAG nikuonyesha Serikali kutokuwa na imani na vyombo vyake. Kwa muktadha huo huo endapo Serikali itaendelea kuamini maneno yasiyo na facts kutoka kwa wanasiasa basi utumishi wa Umma hauna haja yakuwepo Bora wanasiasa waongoze kila sikta
Kama wakuu wa nchi wataendelea kusimamia sheria zinazotoa Kinga yakuishtakiwa wanasiasa akiwemo Spika na Naibu Spika nivigumu kwao kulijenga Taifa lenye maendeleo na haki. Dunia Leo hii inawavua watawala Kinga za kushtakiwa sisi tunaongeza idadi ya kutokushtakiwa.
Kama nchi ikiwa inaona wazi kwamba sheria Ni mbovu na ikaziruhusu kupelekwa Bungeni na ubovu wake na baada ya muda flani kwa bunge linavyojisikia likaelekeza zirekebishwe kuendana na wabunge wanataka nini, Ni vigumu kuwa na Taifa endelevu.
Mhe. Rais na Makamu wa Rais maneno yenu na matendo yenu yanakosolewa nakutoaminika kwa sababu mizania haipo sawa. Double standard nikubwa sana Kati ya raia na mwanasiasa.
Siku tukiondoa ubaguzi wakisheria na kimamlaka ndipo mtaanza kutoa hotuba zikatekelezeka. Kwa Sasa nivigumu kutekelezeka kwa Yale mnayodhani mlitaka kuwafanyia Watanzania kwa sababu Watanzania wanaona hayapo kwenye misingi ya sheria Bali yapo zaidi kwenye misingi ya utashi na tafsiri ya anayetaka kutekeleza.