Mhe. Rais Magufuli alikataa rushwa wazi, watumishi walioiba wawajibishwe kumuenzi

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Hakuna ubadhirifu uliofanywa na Rais aliyepita, ubadhirifu ulifanya na viongozi wasio kuwa na maadili wakiwemo Mawaziri, makatibu wakuu na maafisa suuri wengine katika sekta mbalimbali.

Kama tunataka kumuenzi JPM Basi tuwawajibishe wanaohusika Kama ambavyo angeafanya endapo angekuwa hai.

Kuacha kuwawajibisha nikuruhusu wizi mkubwa zaidi na kisha kumtupia lawama Rais aliyepo Sasa.
 
kukataa rushwa na wizi ni rahisi sana...ila kuiba na kupokea rushwa ni suala lingine la gizani.

Taifa hili linahitaji mifumo imara yenye uwezo wa kudeal na yeyote.
 
tunachojua sisi magufuli alikua na nia ya dhati kwa maendeleo ya tanzania..ambao hawakuliona hilo nawachukulia kama wachawi tuuh hawakosekanagi katika jamii...
 
Wengi wao wamebebwa na upepo wa mkumbo.,in their mind they real know exactly what the late jpm hax done for the coming good of our nation..in short wana appriciate kazi ya jpm ingawa wanajitia kiburi
 
Wengi wao wamebebwa na upepo wa mkumbo.,in their mind they real know exactly what the late jpm hax done for the coming good of our nation..in short wana appriciate kazi ya jpm ingawa wanajitia kiburi

Hakuna kiongozi mwenye nia njema na nchi yake akawa muuaji na mnajisi box la kura. Vinginevyo tukubaliane kuwa Kaburu Pieter Botha, alikuwa kiongozi mzuri kuliko Mandela kwa jinsi aliyoijenga Afrika kusini.
 
Hakuna ubadhirifu uliofanywa na Rais aliyepita, ubadhirifu ulifanya na viongozi wasio kuwa na maadili wakiwemo Mawaziri, makatibu wakuu na maafisa suuri wengine katika sekta mbalimbali.

Kama tunataka kumuenzi JPM Basi tuwawajibishe wanaohusika Kama ambavyo angeafanya endapo angekuwa hai.

Kuacha kuwawajibisha nikuruhusu wizi mkubwa zaidi na kisha kumtupia lawama Rais aliyepo Sasa.
Hata kama amefariki lazima tuseme ili waliopo wajifunze

1. Alikuwa mtu mwenye roho mbaya, mshenzi, muuaji na aliyependa kuona watu wenye maendeleo au waliotofautiana nae wakiteseka sana. Mfano wa haya ni kwa vile walivyowafanyia Manji, Erick Kabendera, Ben saanane, Rwabaje, Mama yake Erick Kabendera, Mdude Nyangali, Zacharia na watu wengine wengi

2. Alikuwa mtu Mbinafsi sana, aliyependa sifa zote zirudi kwake. Alipenda kusifiwa, kuonekana yeye ni bora kuliko wenzake. Hata kwenye hotuba zake alipenda kujionesha ni yeye zaidi na wala sio wenzake. Rejea hotuba alizokuwa akisema bila yeye miradi haitofanikiwa. Aliwapa vyeo bila aibu watu waliokuwa wakimsifu yeye binafsi. Mf. Katambi, Sabaya, kafulila, Mrema, Babu

3. Alikuwa mkabila na mbaguzi wa kikanda aliyetukuka. Kwenye awamu yake alijaza watu wa kanda ya ziwa hasa wasukuma na mapandikizi wenzake kutoka Rwanda na Burundi kwenye nafasi nyeti serikalini. Bashiru, Kakoko, Doto James na wengineo wengi ni mifano michache tu. Hawa watu walikuwa hawagusiki na waliweza kufanya lolote lile kwa jina lake na yeye hakusema lolote. Hawa watu waliweza hata kuwadharau waziwazi Waziri Mkuu na Makamu wa Rais na wala hawakujali mfumo wa utendaji serikalini. Waliweza kupiga simu au kupita moja Kwa moja ikulu hadi kwa Magufuli bila kupita kwa waziri, waziri mkuu au hata Makamu wa Rais.

4. Kwa kujua kwake kuwa ni kweli aliharibu uchumi wa nchi kwa sera zake mbaya, aliwekeza sana kwenye propaganda za kujitangaza sana kupitia vyombo vya Habari ili kuwa brainwash watu wasiofikiri vizuri. Tv zote, magazeti, blogu na hata viongozi wa dini aliwatumia kumtangaza yeye muda wote na kumsifu yeye muda wote ili aonekane ni Bora kuliko wenzake. Ofisi za Taifa zilifanywa kutengeneza data za uongo ili aonekane anafanya vizuri kumbe nchi ilikuwa inaenda pabaya sana. Rejea taarifa aliyotoaga kuwa ATCL inapata faida ya bil 28.

5. Aliwadharau sana wenzake. Na alifanya kila jitihada wenzake waonekane watu wasiofaa ( hasa viongozi waliopita). Aliishi nao kiunafiki akiwatumia vijana wake Kama Msiba, Sabaya , Makonda na Aly Happi kuwatukana na kuwatisha ili aharibu taswira yao kwa jamii na ajitengeneze kuwa ni Bora kuliko wao.

6. Alianzisha mambo ili kuwakomoa watu waliokuwa tofauti nae. As Kofi niwemugizi, Aidan Eyakuze, Yusuph Manji ni wachache kwenye hii list, walianza kuhojiwa uraia, wakanyang’anywa passport na kupewa kesi mbalimbali ili kukomolewa kutokana na kutofautiana nae.

7. Kwa sera zake mbovu, aliharibu kwa kiasi kikubwa uchumi hivyo kupelekea kuwepo tatizo kubwa la ajira . Ili kujiokoa na Tatizo hili Kwa kuwapumbaza watanzania wajinga alianzisha utaratibu wa kujifanya kuwa karibu na Mama lishe na bodaboda huku akisema kuwa wanaruhusiwa kufanya Biashara popote pale. Alifanya hili Kwa sababu alijua kabisa kuwa ameharibu uchumi wa Tanzania na amesababisha watu wengi kukosa ajira. Kuepuka lawama akataka kuifanya nchi nzima kuwa nchi ya wachuuzi huku akiharibu mipango miji na kusababisha walipa kodi wapungue kwa kasi.

8. Kutokana na kuwa na sera mbovu za kiuchumi huku akiiba Mali za watanzania Kwa kigezo cha uzalendo, akiogopa kupinduliwa na jeshi na wasaidizi wake, aliamua kufuatilia maongezi ya wasaidizi wake wote akiwemo Makamu wa Raisi , Mawaziri na viongozi wa Ccm. Alikuwa hadi meseji zao anasoma na alivyo mshamba alikiri hadharani kuwa anafuatilia mawasiliano ya watu. Alianzisha pia utaratibu wa wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama kuwa nae popote pale anapokuwepo. Huu utaratibu ulikuja kuonekana katika awamu ya 5 tu maana Kwa awamu ya 1 hadi ya 4 haikuwai kutokea wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na spika na Jaji mkuu kuambatana na Rais popote pale anapokuwa.

9. Alikuwa muuaji
Niliwai bishia watu wengi kwenye hili ila nilikuja kuthibitisha alipokuja tamka hadharani kuwa huwezi kuwa msaliti alafu uka survive na baada ya hotuba yake iyo Tundu Lissu alikuja kushambuliwa kwa Risasi 38 huku 16 zikiingia mwilini wake.

10. Alijiona ni Bora kuliko mtu yeyote yule na alitaka neno lake ndo liwe mwisho. Alisema hadharani kuwa hashauriki na kila mtu aliyekuwa akimshauri alimchukulia kama adui yake. Siku za mwisho za uhai wake alitofautiana na kupingana Hadi na viongozi wa dini wa kanisa katoliki ambao waliamua kushauri nchi kuchukua hatua tofauti dhidi ya corona.

Mungu fundi sana! Alale anapostahili mwendazake.
 
Magufuli amesababisha hasara mara 5000 zaidi ya rushwa aliyozuia. Hakuna kiongozi aliyefanya vibaya kama huyu. Mtajua mengi tulieni.
acha unafiki wewe, haya waliokuwa wakipiga enzi zile walifanya nini?? na hata kama alipiga at least tunaona maendeleo
 
Maendeleo? Pengine Chato.
wewe umezaliwa nchii kweli? au ndo wale wakimbikizi au vibaraka...mwenye macho haambiwi tazama Mazuri ya Magufuli yanaonekana na ameacha alama zisizofutika katika Nchi hii na alama hizi karibu mikoa na wilaya zote za Tanzania.... haya tupe status za wapiga dili enzi hizo walifanya nini
 
wewe umezaliwa nchii kweli? au ndo wale wakimbikizi au vibaraka...mwenye macho haambiwi tazama Mazuri ya Magufuli yanaonekana na ameacha alama zisizofutika katika Nchi hii na alama hizi karibu mikoa na wilaya zote za Tanzania.... haya tupe status za wapiga dili enzi hizo walifanya nini
Kwa ufupi tu Kikwete amefanye mengi ya maana zaidi ya Magufuli. Kinachoendelea sasa ni kuganga hasara na ubadhirifu kipindi cha Magufuli, alitumia nguvu zote kuficha makosa lukuki aliyofanya sasa yameanza kuanikwa, mtaona mengi.
 
Kwa ufupi tu Kikwete amefanye mengi ya maana zaidi ya Magufuli. Kinachoendelea sasa ni kuganga hasara na ubadhirifu kipindi cha Magufuli, alitumia nguvu zote kuficha makosa lukuki aliyofanya sasa yameanza kuanikwa, mtaona mengi.
hamnazo wewe..... ata mtoto wa kindergattern anajua ukweli kuhusu JPM
 
Back
Top Bottom