Serikali kutumia kigezo cha kupitia JKT ili kupata nafasi za kazi wakati si vijana wote huchaguliwa kujiunga na JKT ni ubaguzi wa wazi

Nimesoma matangazo ya kazi tume ya ajira hivi karibuni,wanataka waombaji wawe wamepitia JKT na wakati huox2 JKT hawana uwezo wa kuchukua wanafunzi wote.Nani wa kulaumiwa hapo,nashauri muondoe hicho kigezo.
 
Kumekuwa na tabia za hivi karibuni, kwamba ili upate nafasi za kazi kwa vyombo vya ulinzi na usalama, mojawapo ya sifa ya waombaji ni kupitia mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa. Huu ni ubaguzi wa wazi kabisa.

Hivi toka lini vijana wote waliohitimu kidato cha sita waliitwa wote kujiunga na jeshi la kujenga Taifa? Ina maana hata wale ambao hawakuchaguliwa kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa, pasipo hiari yao, wameondolewa sifa za kuwa watumishi wa vyombo hivi vya Ulinzi na Usalama.

Kufanya kigezo cha kupitia mafunzo ya JKT kama moja ya sifa ya kupata kazi Polisi, Magereza, Uhamiaji na TAKUKURU ni ubaguzi wa wazi kwa watu ambao hawakuchaguliwa kujiunga na vyombo hivyo na pia ni mwendelezo wa upendeleo kwa watu waliopendelewa kujiunga na kozi hizi za JKT.
Wasomi wa law school wajumuike kufungua kesi yakikatiba juu ya huo unoonekana ni ubaguzi .
Wanasheria changamkeni.peleken mahakamani kupata ufafanuzi kisheria
 
Kupitia jkt haikupaswa kuwa kigezo kulingana na mazingira yetu kwa sasa . Itabidi serilikal iliangalie upya swala hili lasivyo wahusika wanaligawa taifa
 
Yupo humu pia wasaidizi wake wa karibu wapo humu pia ikitokea hajasoma huu ujumbe na kuufanyia kazi wao watafikisha ujumbe huu kwake kuna mantiki katika ujumbe huu maana kuna watu walifaulu pia kidato cha sita ila hawakupata nafasi ya kulitumikia jeshi la kujenga taifa, kama kweli ana nia ya dhati kuboresha vyombo vya ulinzi na usalama ni vyema ajira za majeshi hayo yasiangalie kama umepita jkt ama lah, enzi za JK na Mkapa ilikuwa hivi pia.

Asante kwa kumbusho.
Naaply mwisho inagoma
 
Back
Top Bottom