Serikali kutumia kigezo cha kupitia JKT ili kupata nafasi za kazi wakati si vijana wote huchaguliwa kujiunga na JKT ni ubaguzi wa wazi

DidYouKnow

JF-Expert Member
Jul 28, 2019
1,094
1,691
Kumekuwa na tabia za hivi karibuni, kwamba ili upate nafasi za kazi kwa vyombo vya ulinzi na usalama, mojawapo ya sifa ya waombaji ni kupitia mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa. Huu ni ubaguzi wa wazi kabisa.

Hivi toka lini vijana wote waliohitimu kidato cha sita waliitwa wote kujiunga na jeshi la kujenga Taifa? Ina maana hata wale ambao hawakuchaguliwa kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa, pasipo hiari yao, wameondolewa sifa za kuwa watumishi wa vyombo hivi vya Ulinzi na Usalama.

Kufanya kigezo cha kupitia mafunzo ya JKT kama moja ya sifa ya kupata kazi Polisi, Magereza, Uhamiaji na TAKUKURU ni ubaguzi wa wazi kwa watu ambao hawakuchaguliwa kujiunga na vyombo hivyo na pia ni mwendelezo wa upendeleo kwa watu waliopendelewa kujiunga na kozi hizi za JKT.
 
Yupo humu pia wasaidizi wake wa karibu wapo humu pia ikitokea hajasoma huu ujumbe na kuufanyia kazi wao watafikisha ujumbe huu kwake kuna mantiki katika ujumbe huu maana kuna watu walifaulu pia kidato cha sita ila hawakupata nafasi ya kulitumikia jeshi la kujenga taifa, kama kweli ana nia ya dhati kuboresha vyombo vya ulinzi na usalama ni vyema ajira za majeshi hayo yasiangalie kama umepita jkt ama lah, enzi za JK na Mkapa ilikuwa hivi pia.

Asante kwa kumbusho.
 
Ndomana mkatakiwa muende,sababu mmepitia malezi ya kibwege Sana,mmelegea,Hamna nidhamu,Hamna uzalendo
Hujui unachoongea sio kila za huko zinatumia nguvu nyingine ni akili tu sasa takukururu na matumizi ya nguvu wapi na wapi boss
 
Kumekuwa na tabia za hivi karibuni, kwamba ili upate nafasi za kazi kwa vyombo vya ulinzi na usalama, mojawapo ya sifa ya waombaji ni kupitia mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa. Huu ni ubaguzi wa wazi kabisa.

Hivi toka lini vijana wote waliohitimu kidato cha sita waliitwa wote kujiunga na jeshi la kujenga Taifa? Ina maana hata wale ambao hawakuchaguliwa kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa, pasipo hiari yao, wameondolewa sifa za kuwa watumishi wa vyombo hivi vya Ulinzi na Usalama.

Kufanya kigezo cha kupitia mafunzo ya JKT kama moja ya sifa ya kupata kazi Polisi, Magereza, Uhamiaji na TAKUKURU ni ubaguzi wa wazi kwa watu ambao hawakuchaguliwa kujiunga na vyombo hivyo na pia ni mwendelezo wa upendeleo kwa watu waliopendelewa kujiunga na kozi hizi za JKT.
Umeandika ukweli mtupu mkuu. Kwa yeyote mwenye akili timamu hili ni jambo la kushangaza sana.
 
Kumekuwa na tabia za hivi karibuni, kwamba ili upate nafasi za kazi kwa vyombo vya ulinzi na usalama, mojawapo ya sifa ya waombaji ni kupitia mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa. Huu ni ubaguzi wa wazi kabisa.

Hivi toka lini vijana wote waliohitimu kidato cha sita waliitwa wote kujiunga na jeshi la kujenga Taifa? Ina maana hata wale ambao hawakuchaguliwa kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa, pasipo hiari yao, wameondolewa sifa za kuwa watumishi wa vyombo hivi vya Ulinzi na Usalama.

Kufanya kigezo cha kupitia mafunzo ya JKT kama moja ya sifa ya kupata kazi Polisi, Magereza, Uhamiaji na TAKUKURU ni ubaguzi wa wazi kwa watu ambao hawakuchaguliwa kujiunga na vyombo hivyo na pia ni mwendelezo wa upendeleo kwa watu waliopendelewa kujiunga na kozi hizi za JKT.
Nani alianzisha utaratibu wa JKT? Mizigo mingine msimbebeshe SSH
 
Kila jambo lina sababu kijana,ila nna ushahidi wa vijana wengi opp magufuli ambao wapo maeneo tofauti tofauti kwenye idara flan ni wachapa kazi wazuri sana ,
 
Kwa zamani,sifa ya JKT ilikuwa na maana lakini sikhiizi hizo nafasi wanaitwa wachache..je ni kosa la mwanafunzi au la serikali?serikali inabidi ibebe lawama kwa wote kwa kutoa ajira kwa ubaguiz wa kigezo ya kuwa muhusika lazima awe amepita JKT
 
Vijana wanaochaguliwa kwenda jeshi la mujibu wa Sheria hawafiki hata nusu ya wahitimu wote kidato cha SITA. Hivyo kuweka Cheti cha jeshi kama kigezo cha ajira ni upunguani kabisa. Yaani huko serikalini kuna waajiriwa huko vichwa vya kuwaza ni Bora vya panzi.
 
Back
Top Bottom