Mhe. Rais Kikwete kwanini serikali itatudanganya mpaka lini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mhe. Rais Kikwete kwanini serikali itatudanganya mpaka lini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by makoye2009, Feb 19, 2011.

 1. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #1
  Feb 19, 2011
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Kwako Mhe. Rais wa JMT, naamini utasoma waraka huu kupitia kwenye huu mtandao wetu wa JF kama siyo wewe basi wasaidizi wako wanaopitapita humu watakufikishia salamu.

  Kamba serikali yako mheshimiwa Rais imekuwa kila siku ikisema uongo na kuwafanya Watanzania waonekana kuwa ni majuha mbele ya Ulimwengu wa kimataifa na mbele ya Mwenyezi Mungu.


  Uongo wenyewe umejikita kwenye maswala ambayo yanagusa maisha ya Watanzania moja kwa moja. Nitajaribu tu kuainisha baadhi ya uongo ambao wewe mwenyewe au wateule wako wamekuwa wakiwalaghai Watanzania kwa kutumia kigezo cha AMANI,UPENDO NA MSHIKAMANO.
  1. Wakti unaingia madarakani mwaka 2005 uliahidi MAISHA BORA kwa kila Mtanzania,leo ni mwaka 2011 ukiwa kwenye awamu yako ya 2 na ya mwisho hakuna MAISHA BORA kwa Mtanzania. Kwanini ulisema uongo?
  2. Baada ya Mahakama ya Biashara ya Kimataifa ICC kuihukumu TANESCO kwamba iwalipe DOWANS sh.BILIONI 94/=na Watanzania wakaanza kupinga malipo hayo kwa nguvu zote,wewe tarehe 5/2/2011 ukadai kuwa WAMILIKI WA DOWANS HUWAJUI WALA HUJAWAHI KUWAONA NA HAWAKUHITAJI!ICC wanasema ROSTAMU AZIZI ALIPEWA NGUVU YA KISHERIA(Powers of Attorney)na DOWANS. Kwa maana nyingine RA ndiye mmiliki au mwanahisa wa DOWANS.Je, ni kweli humjui Rostam Aziz,MB wa Igunga kwa tiketi ya CCM na MWEKA HAZINA WA CCM huko nyuma?
  3. Maandamano ya CHADEMA kupinga uchaguzi haramu wa Meya wa Jiji la Arusha ulipelekea mauaji ya Watanzania 2 na Mkenya 1 Jeshi la POLISI LILIENEZA UONGO KWENYE VYOMBO VYA HABARI ILI KUBARIKI MAUAJI HAYO. WM PINDA naye juzi akarudia uongo huo huo lakini baada ya Mbunge G.Lema kuhoji uongo huo na akaambiwa na Spika awasilishe ushahidi wake kuwa WM alidanganya Bunge na akafanya hivyo Spika akabadilisha mwelekeo!Huu ni uongo mara 2,wa WM na Spika. Je watu wako wanawadanganya Watanzania kwa faida ya nani??
  4. Baada ya MAUAJI YA ARUSHA, Waziri wako wa Mambo ya Ndani alisema kuwa atawakutanisha CCM na CHADEMA ili kumaliza mgogoro uliosababisha MAUAJI hayo. Mpaka sasa hivi NAHODHA hajatekeleza ahadi hiyo.Je,alikuwa anamdanganya nani kwa faida ya nani?
  5. Milipuko ya MABOMU ya Mbagala April,2009 Waziri wako wa Ulinzi Dr. Hussein Mwinyi na Mkuu wako wa Majeshi ya Ulinzi Jen.Mwamnyange walisema HILO TUKIO LA MBAGALA HALITAJIRUDIA TENA. Sasa limejirudia G/Mboto. Kwanini walitudanganya Watanzania?
  6. Jana WM Pinda alitangaza Bungeni kuwa ni Watanzania 20 tu waliokufa kwenye hili janga la G/Mboto. Vyombo vya habari vinavyomilikwa na Serikali ya CCM vinanukuu idadi hiyo ya WATU 20.Lakini mpaka sasa hivi IDADI YA WATU WALIOKUFA NI 39.Kwanini watu wako wanataka kuficha IDADI HALISI YA WALIOKUFA? Kwa faida ya nani?
  7. Wasemaji wako wa Jeshi jana wamedai KUWA WANAJESHI HUWA HAWAJIUZULI maana wao si wanasiasa. Tunajua kuwa Mkuu wa Majeshi Mwamnyange AMETEULIWA NA RAIS na kwa maana hiyo RAIS ANAWEZA KUMFUKUZA KAZI. Kwanini anawadanganya watu kuwa wanajeshi huwa hawajiuzulu?Je,anapoharibu kazi kwa uzembe kama ilivyo sasa hivi, UTAENDELEA KUMWEKA HAPO MPAKA LINI? Hivi angegundulika kuwa ANATAKA KUPINDUA SERIKALI YAKO utamwacha hapohapo kwasababu si mwanasiasa?
  Namaliza kwa kukuomba kwa heshima na taadhima hawa Viongozi wako wanaodanganya Wapiga kura UWAWAJIBISHE KWA KUWASHINIKIZA WAJIUZULU AU UWAFUKUZA KAZI AMA KUWASHUSHA MADARAKA(DEMOTIONS). Na wewe kama Rais UOMBE RADHI KWA WATANZANIA KWA UONGO ULIOSEMA. Hii itakujengea heshima wewe,serikali yako na Chama chako CCM.

  Nawasilisha.
   
 2. M

  Mchekechoni JF-Expert Member

  #2
  Feb 19, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 280
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mtu muongo ni muongo tu, hata cku1 ucmwamini, kwa kifupi achana naye na uendelee na maisha yako kama vile hayupo!
   
 3. semango

  semango JF-Expert Member

  #3
  Feb 19, 2011
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 532
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Well said mkuu lakini uliyemwambia ni msanii asiye elewa lolote.hapo ni sawa na kumpigia mbuzi guitar.
   
 4. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #4
  Feb 19, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,229
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  siredi yako imetulia mno...sema mtu mwenyewe kiziwi halaf kipofu kwa maoni ya watz...anywei tutamfikishia ujumbe kwa njia mbadala...yaani maandamano ya umma!!!
   
 5. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #5
  Feb 19, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,127
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Wasadizi alionao wanamwambia kile tu wanachofikiria kitamfanya endelee na vicheko vyake visivyo na mwisho. Sidhani wala sitegemei kama ujumbe wako mzuri utamfikia. Ninachoelewa ni kwamba hata wao hawaelewi vigezo vya uteuzi wao kwenye nafasi walizo nazo.
   
 6. K

  K007 Member

  #6
  Feb 19, 2011
  Joined: Jan 30, 2011
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mkuu huyo jamaa kwanza CCM inamfikia mikononi mwake, pili amani itavunjika akiwa madarakani! we subiri si wanatuona watanzania wajinga! sasa ajiangalie tunaweza kumtoa kabla ya kumaliza muda wake 2015! hatupendi hayo yatokee lakini TUNAELEKEA KUCHOKA!
   
 7. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #7
  Feb 19, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  :spider: hasikii
   
 8. Fasta fasta

  Fasta fasta JF-Expert Member

  #8
  Feb 20, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 620
  Likes Received: 114
  Trophy Points: 60
  Na hapo hatujasikia sera za Makamba na CCM yake. Mbona lile la Arusha alikuwa anapayukapayuka sana.
   
 9. mikonomiwili

  mikonomiwili JF-Expert Member

  #9
  Feb 20, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 274
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mkuu niongezee hi ya umeme waziri alitudanganya kua tatizo lakukatika kwaumeme litakua historia badalayake mgawo kama kawaida.
  JK kwenye ule wmaka kuliokuia na mgao waumeme alitudanganya mitambo ya IPTL ingewashwa ndani ya wiki mojo badala yake ili washwa
  Baada ya mwezi na majuma kathaa
  Waziri wake wakatiba akatuiambia kua serikali haina mpango wa kubadili katiba baadae tukasikia inawezekana .
  Jk akatundanganya uleuwanja wa ndege unaojengwa mbeya utakamilika mwakaulio pita lakini mpaka sasa hakuna kinachoendelea
  waziri wa fetha akatudanganya kua eti hela zinazo chuja rangi ndo halali ,hata kwa mtoto wadarasa la kwanza hawezi amini hiki
   
Loading...