Mhe Rais hongera kwa madarasa na majengo ya hospitali, ila kwanini kipaombele kwanini kimekuwa makao Mijini na siyo kwenye shule za tembe?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Mhe. Rais umeeleza madarasa yajengwe Ila waliokwenda kujenga wamekosea strategy, uwezi kujenga madarasa mawili kwenye shule zenye madarasa ya kutosha mjini ukaenda kujenga madarasa mawili kijijini kwenye nyumba za tembe. Zipo shule zilihitaji madarasa Saba yote yajengwe lakini hakuna Fedha zilizpelekwa Hadi Sasa, zipo shule zimechakaa na hazihitaji madarasa mapya zinahitaji UKARABATI wa yaliyopo lakini hakuna aliyejikita kwenye UKARABATI wote wamejikita kwenye ujenzi wa madarasa mapya.

This kind of thinking ya viongozi wetu inatia mashaka kama kweli wanajua changamoto za wananchi. Haiwezekani shule Ina madarasa kumi ya mkoloni yaliyochakaa Bada yakuyakarabati unakuja kujenga mengine mawili, Nan aiwaambia wanataka Madasa mapya?

Mhe. Waziri unaweza kuwa unafanya KAZI nzuri Ila pia ukawa haufanyi KAZI kitaalamu. Nendeni kwenye shule mlizojenga madarasa mapya angalieni madarasa ya zamani yana Hali Gani. Mlishindwa Nini kuona tatizo lilipo?

Kibaya zaidi mnakuja na kauli za kisiasa kutoka Dodoma na DSM, mtu yupo wizarani anapanga Nini Wananchi wa Murongo au Kanyigo au Kaisho wafanyiwe in terms of service wakati yupo DC, DED katibu tarafa na viongozi wa serikali za mtaa.

Nimeona shule imejengewa madarasa mawili complete lakini Ina madarasa nane yasiyo na sakafu wala madawati yakutosha.

Nikuombe Mhe. Rais unapotembelea huko fedha za mradi shule zilipokwenda jaribu kulinganisha Hali ya uchakavu ya majengo ya zamani then angalia kama tulipaswa kujenga madarasa kila shule au tulipaswa kujenga na kukarabati baadhi ya maeneo? Lakini pia wataalamu wakusaidie kujua kwanini shule za vijijini ndani huko hazijajengewa madarasa? Tatu tujiulize ni lini tutazisaidia shule ambazo hazina majengo ya kisasa huko kijijini?

Wataalum msaidieni mama, halmashauri sikilizeni wananchi kabla ya kupeleka miradi. Haya niliyoandika ndiyo yanayojadiliwa vijijini.

Wanauliza tunaweza kuwajengea wanafunzi 80 madarasa mawili tukawaacha wanafunzi 600+ wanakaa kwenye vumbi na baadhi bila madawati?
 
Hiyo ni kweli mkuu. Mi nilikua naona kila halmashauri iorodheshe shule ambazo ni mbovu ili kila bajeti wawe wanakarabati. Kuna shule nyingine ni mbovu sana unaweza kusema ni mabanda ya kufugia kuku.
 
Kila mahali kuna upigaji
Ukarabati na kujenga
Kwenye ujenzi ndio kuna hela nje nje
Taifa letu bado sana kwa uaminifu na kujituma
 
Mama katuokoe zile inshu za mwananchi kujipeleka kufanya kaz za maendeleo zilkuwa znaniboa sana,unalipa kodi tena unaenda kuhangaika kusomba mchanga na wakat huo huo familia inakutegemea
 
Back
Top Bottom