Mhe. Rais, hii ndiyo Julius Nyerere International Airport inavyowatesa wageni na kuwakimbiza

pepe17

JF-Expert Member
Oct 17, 2007
295
221
Mheshimiwa Rais, labda hili litakuwa gumu kidogo kwa wewe kuligundua maana viongozi wote wanapopita pale uwanjani huwa hawatumii njia na process hii ambayo sisi watu wa kawaida na wageni wanaotoka nje huwa wanaitumia katika kupata viza (tourist visa) ya kuingia nchini.

Pale kuna uozo mkubwa sana na si hilo tu basi upoteaji mkubwa wa fedha za serikali ambazo nadhani huwa zinaingia mifukoni mwa baadhi ya wafanyakazi na viongozi wao, ni mtandao ambao upo kwa muda mrefu tu. Ni usumbufu kwelikweli usiokuwa na sababu yoyote.

Sasa ninaelezea kwa kirefu:
Wageni wengi wanaokuja Tanzania na kuchukulia visa zao pale aiport huwa wanatozwa dola za kimarekani 50 ($50.00 Usd) na huwa hawakubali aina nyingine yoyote ya pesa isipokuwa dola za kimarekani tu. (hilo ni tatizo namba 1).

Wageni wanapofika basi kuna mtu (sijui ni nani na anatoka department gani) husimama pale na kukusanya passport zote na hizo dola 50 (kila passport huwekwa dola 50 ndani yake) huyo mtu huzikusanya bila hata ya kutoa risiti yoyote,(na kuwaambia msubiri) na kuenda nazo kusikojulikana (labda ni ofisini kwao) kwa ajili ya kuweka hizo viza, hapo sasa ndiyo kuna tatizo kubwa sana, Mtasubiri si chini ya saa moja ndipo mtarudishiwa passport zenu na viza tayari zimo ndani, akifika huyu mtu anaanza kuita majina na kukukabidhi passport zenu ili sasa muelekee uhamiaji kwa ajili ya kupata entry ya kuingia, wakati huo sasa wale wenzenu wote mliokuja nao wameshamaliza kupita kwa watu wa forodha na wako nje tayari.

Nimesikia kwa sasa hivi huyo mtu wa kukusanya hizo passport hayupo ila walichofanya ni kuweka kijiofisi kidogo ambacho hufanya hivyo hivyo, unafika pale kwenye hicho kijiofisi na kumpa passport na dola 50 (hawataki aina nyingine yoyote ya fedha) na HUPEWI risiti yoyote, halafu unaambiwa usubiri, baadaye anakuja mtu kuzikusanya passport zote hizo anaenda nazo ndani huko, hapo bado tena mtasubiri siyo chini ya saa moja au mawili ndiyo mrudishiwe hizo passport. Mimi nilishuhudia wageni wenye asili ya kizungu wakilalamika sana pale airport kuhusu huo usumbufu.

Sasa mimi maswali yangu ni kwa nini wanapenda kuwafanyia watu huu usumbufu? na hapo ni dhahiri kuwa kuna pesa nyingi tu ambayo badala ya kwenda serikalini basi huingia mifukono mwa watu.

Sasa Mheshimiwa Rais kama tuko kwenye kuitengeneza Tanzania hii kuwa nzuri, bora na ya uwajibikaji, kwa nini basi usisafishe na kulitatua tatizo hili? Mimi naamini kabisa kuwa wageni wengi wanaokuja TZ wakishapata usumbufu huu basi huwa hawarudi tena na badala yake wanakwenda nchi jirani.

Nini cha kufanya:
Nimetembelea nchi nyingi ambazo hutoa viza palepale airport (visa on arrival) na hukuti matatizo kama haya kwa sababu hakuna wizi.

Nchi 1: Hapa ukifika tu utakuta kuna ofisi, unaenda dirishani unampa passport yako na pesa au bank card (pesa ya kigeni yoyote inayotambulika, zote zimeorodheshwa pale), palepale anakubandikia visa (sticker) na unaelekea kwa uhamiaji. Kitendo hicho hakichukui hata dakika 5.

Nchi 2: Hawa hawataki fedha taslimu kabisa, ni bank card tu, ukifika tu unaenda kwa uhamiaji moja kwa moja, pale unafanya malipo kwa bank card yako, unapata risiti na anakugongea viza (mtu huyohuyo mmoja), kwa hiyo yeye hakamati fedha taslimu kabisa. Hapa sasa tunaweza kusema kwa wale wasio na card je? Jibu ni hivi, kwanza watu wengi wanaoomba viza hapo airport ni wageni na ndiyo maana wanaomba hizo viza, kwa asilimia kubwa ya hao watu wanazo kadi, na pili unaweza kununua Prepaid visa/mastercard, kwa wale wanaoishi ughaibuni watanielewa, kupata bank card huko ughaibunu siyo big issue.

Nchi 3: Hawa sasa ukifika unaenda dirishani kulipa kwa bank card au fedha taslimu, halafu anakupa risiti unaenda nayo kwa uhamiaji na passport yako na uhamiaji anakupigia entry visa kwenye passport yako na kwenye ile risiti, hapo huchukui hata dakika kumi.

Sasa mimi sisemi tuige hayo hapo juu (lakini kama ni mazuri kwa nini tusiige?) lakini tukichukua yote hayo na kuyachanganua vizuri basi tunaweza kutengeneza mfumo wetu wenyewe ambao hautampa mgeni usumbufu hapo airport. Pili ningependa pia kuiomba serikali hizi balozi zake ziwe zinajaribu kutoa visa kwa waombaji wake kwa haraka kidogo ili kuondoa nenda rudi nyingi.

Mimi naamani kabisa kuwa hilo tatizo linaweza kutatulika na mtiririko wa wageni unaweza kuongezeka, maana wenzetu wageni huwa hawapendi usumbufu, kwanza huwa wanakuja kutembea na hivyo huwa hawapendi kupata bugudha kama hizo hasa ukizingatia kuwa Airport ndiyo kioo cha nchi, maana ya kwamba mgeni akiona mwenendo wa pale airport (airport yoyote duniani) basi tayari inampa taswira ya nchi hiyo ilivyo.

Kwa hiyo Naomba Mheshimiwa Rais na waziri husika mlifumbulie macho suala hili, Fedha za serikali pale airport bado zinaliwa na wajanja.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu mbariki JPM
 
Mheshimiwa Rais, labda hili litakuwa gumu kidogo kwa wewe kuligundua maana viongozi wote wanapopita pale uwanjani huwa hawatumii njia na process hii ambayo sisi watu wa kawaida na wageni wanaotoka nje huwa wanaitumia katika kupata viza (tourist visa) ya kuingia nchini. Pale kuna uozo mkubwa sana na si hilo tu basi upoteaji mkubwa wa fedha za serikali ambazo nadhani huwa zinaingia mifukoni mwa baadhi ya wafanyakazi na viongozi wao, ni mtandao ambao upo kwa muda mrefu tu. Ni usumbufu kwelikweli usiokuwa na sababu yoyote.
Sasa ninaelezea kwa kirefu:
Wageni wengi wanaokuja Tanzania na kuchukulia visa zao pale aiport huwa wanatozwa dola za kimarekani 50 ($50.00 Usd) na huwa hawakubali aina nyingine yoyote ya pesa isipokuwa dola za kimarekani tu. (hilo ni tatizo namba 1).
wageni wanapofika basi kuna mtu (sijui ni nani na anatoka department gani) husimama pale na kukusanya passport zote na hizo dola 50 (kila passport huwekwa dola 50 ndani yake) huyo mtu huzikusanya bila hata ya kutoa risiti yoyote,(na kuwaambia msubiri) na kuenda nazo kusikojulikana (labda ni ofisini kwao) kwa ajili ya kuweka hizo viza, hapo sasa ndiyo kuna tatizo kubwa sana, Mtasubiri si chini ya saa moja ndipo mtarudishiwa passport zenu na viza tayari zimo ndani, akifika huyu mtu anaanza kuita majina na kukukabidhi passport zenu ili sasa muelekee uhamiaji kwa ajili ya kupata entry ya kuingia, wakati huo sasa wale wenzenu wote mliokuja nao wameshamaliza kupita kwa watu wa forodha na wako nje tayari.
Nimesikia kwa sasa hivi huyo mtu wa kukusanya hizo passport hayupo ila walichofanya ni kuweka kijiofisi kidogo ambacho hufanya hivyo hivyo, unafika pale kwenye hicho kijiofisi na kumpa passport na dola 50 (hawataki aina nyingine yoyote ya fedha) na HUPEWI risiti yoyote, halafu unaambiwa usubiri, baadaye anakuja mtu kuzikusanya passport zote hizo anaenda nazo ndani huko, hapo bado tena mtasubiri siyo chini ya saa moja au mawili ndiyo mrudishiwe hizo passport. Mimi nilishuhudia wageni wenye asili ya kizungu wakilalamika sana pale airport kuhusu huo usumbufu.
Sasa mimi maswali yangu ni kwa nini wanapenda kuwafanyia watu huu usumbufu? na hapo ni dhahiri kuwa kuna pesa nyingi tu ambayo badala ya kwenda serikalini basi huingia mifukono mwa watu.
Sasa Mheshimiwa Rais kama tuko kwenye kuitengeneza Tanzania hii kuwa nzuri, bora na ya uwajibikaji, kwa nini basi usisafishe na kulitatua tatizo hili? Mimi naamini kabisa kuwa wageni wengi wanaokuja TZ wakishapata usumbufu huu basi huwa hawarudi tena na badala yake wanakwenda nchi jirani.
Nini cha kufanya:
Nimetembelea nchi nyingi ambazo hutoa viza palepale airport na hukuti matatizo kama haya kwa sababu hakuna wizi.

Nchi 1: hapa ukifika tu utakuta kuna ofisi, unaenda dirishani unampa passport yako na pesa au bank card (pesa ya kigeni yoyote inayotambulika, zote zimeorodheshwa pale), palepale anakubandikia visa (sticker) na unaelekea kwa uhamiaji. Kitendo hicho hakichukui hata dakika 5.

Nchi 2: hawa hawataki fedha taslimu kabisa, ni bank card tu, ukifika tu unaenda kwa uhamiaji moja kwa moja, pale unafanya malipo kwa bank card yako, unapata risiti na anakugongea viza (mtu huyohuyo mmoja), kwa hiyo yeye hakamati fedha taslimu kabisa.Hapa sasa tunaweza kusema kwa wale wasio na card je? Jibu ni hivi, kwanza watu wengi wanaoomba viza hapo airport ni wageni na ndiyo maana wanaomba hizo viza, kwa asilimia kubwa ya hao watu wanazo kadi, na pili unaweza kununua Prepaid visa/mastercard, kwa wale wanaoishi ughaibuni watanielewa, kupata bank card huko ughaibunu siyo big issue.

Nchi 3: hawa sasa ukifika unaenda dirishani kulipa kwa bank card au fedha taslimu, halafu anakupa risiti unaenda nayo kwa uhamiaji na passport yako na uhamiaji anakupigia entry visa kwenye passport yako na kwenye ile risiti, hapo huchukui hata dakika kumi.

Mungu ibariki Tanzania, mungu mbariki JPM

Wageni wanakuja kufwata nini wakati muda wa kututawala ulishafika kikomo tena natamani hawa watu wasije kabisa kwani utalii ni nini bwana wakae kwao wauze mahindi sio kuja kutusumbua k koo na mitaani
 
#

sijaona tatizo lolote kwenye yote uliyoyaelezea na ni utaratibu wa kawaida kabisa, kwa kuwa tu mtu anakuja kama Mtalii haimaanishi kuwa yeye ni Mungu mtu, ni lazima afuate Sheria na taratibu zetu kama yeye hataki huo usumbufu basi akachukue VIZA Ubalozi wetu ulioko nchini mwake, ni rahisi kihivyo tu!
 
Wacha wageni waisome namba tukienda kwao wanatubagua sana nakushangaa mtoa mada kuwatetea mabeberu kimsingi sitaki hata kuwaona hapa bongo maana wanatuzarau sana
wewe hujatembea yawezekana. Siyo wageni wote wenye roho za kibaguzi. Hata huko kwao siyo wote wenye roho za kibaguzi. Mbona hata sisi tunabaguana? au ubaguzi tunaofanyiana sisi kwa sisi huuoni?

Alichokisema mtoa mada ni pesa kuingia mifukoni mwa wajanja wachache. Bureaucracy iliyopo pale JKN international airport si ya kutetea kabisa. Kuna pesa nyingi sana za serikali zinazopotelea kwa watendaji wake kama alivyosema mtoa mada. Kutotoa risit kwa pesa uliyolipwa kutokana na huduma uliyotoa ni wizi.

Pale mimi naona suluhisho ni kuweka Mashine za EFD au malipo yote yafanyike kwa bank card ili kuepusha wizi huo. Pia kumbuka hawa wageni wanakuja kutalii, wanatuletea pesa lazima wapewe huduma kama wateja.
 
Natamani nikuunge mkono, lakini kusubiri masaa 2 kwa entry visa at the aiport, si jambo la kulalamikia. Muhimu washakuwa attended na visa ziko kwenye process. Ukiona mzungu analalamika sana ujuwe ni either racist au paedophile huyo anatakuja kuja kuharibu watoto wadogo anaogopa kufanyiwa screening! Sisi wanatuweka masaa 6 huko makwao
 
Endelea kuwaogopa wazungu maana utalii wao ni wa kuja kutuibia rasilimali tu
masikini wewe moshi vijijini,njoo mjini kwanza ujifunze mengi.ama kweli hata hujui hii dunia inavyokwenda, ni mungu tu pekee ndiye atakayekusamehe!!
 
Huu ni utaratibu wa Ofisi nyingi za uhamiaji kwenye uwanja wa ndege na Mipakani. Kibaya zaidi hizo $50 huwa hazina risiti, hivyo huingia kwenye mifuko ya watu binafsi. Ile mipaka inayoingiza wakongo na raia wengine ambao sio wa EAC ndio huwa vinara wa michezo hii. JPM tupia macho huku.
 
Natamani nikuunge mkono, lakini kusubiri masaa 2 kwa entry visa at the aiport, si jambo la kulalamikia. Muhimu washakuwa attended na visa ziko kwenye process. Ukiona mzungu analalamika sana ujuwe ni either racist au paedophile huyo anatakuja kuja kuharibu watoto wadogo anaogopa kufanyiwa screening! Sisi wanatuweka masaa 6 huko makwao
uko nje ya mada.
#

sijaona tatizo lolote kwenye yote uliyoyaelezea na ni utaratibu wa kawaida kabisa, kwa kuwa tu mtu anakuja kama Mtalii haimaanishi kuwa yeye ni Mungu mtu, ni lazima afwate Sheria na taratibu zetu kama yeye hataki huo usumbufu basi akachukue VIZA Ubalozi wetu ulioko nchini mwake, ni rahisi kihivyo tu!

kwa hiyo mtu alipie viza na asipewe risiti, pesa iingie mifukoni mwa wajanja badala ya kwenda serikalini. Mhe. Magu ana kazi kweli kweli ya kuwaelimisha na kuwabadili nyinyi watu, kila siku anasema MALIPO YOYOTE YAWE NA RISITI!!
 
Huu ni utaratibu wa Ofisi nyingi za uhamiaji kwenye uwanja wa ndege na Mipakani. Kibaya zaidi hizo $50 huwa hazina risiti, hivyo huingia kwenye mifuko ya watu binafsi. Ile mipaka inayoingiza wakongo na raia wengine ambao sio wa EAC ndio huwa vinara wa michezo hii. JPM tupia macho huku.
kumbe mchezo huo siyo pale JNIA tu.
 
Wacha wageni waisome namba tukienda kwao wanatubagua sana nakushangaa mtoa mada kuwatetea mabeberu kimsingi sitaki hata kuwaona hapa bongo maana wanatuzarau sana
Ukienda kihalali na ukamaind business zako awakubagui sanasana wataongea hila utawaelewa ukiwa omba omba lazima wakujue kwa sababu tabia zako zinajulikana.Hila awana wizi rushwa na uzembe kwenye mambo ya muhimu Kule kwao tuchukue mfano halisi waingereza walisema wanajitoa wakambiwa tokeni brexit means brexit hivyo uwo uzembe hapo airport wakufanya mambo locally sio mzuri kwanini tusiweke mfumo wa kuswap card na serikali ipate mapato yake tutaenda kianalog mpaka lini.
 
34 Reactions
Reply
Back
Top Bottom