Mhe. Rais, hii ndiyo Julius Nyerere International Airport inavyowatesa wageni na kuwakimbiza

Kwa jinsi nilivyokusoma sijajua unalalamikia kipi kati ya Muda unaokaa kusubiria taratibu za Ki-Uhamiaji, namna mnavyochangishwa fedha za malipo ya VISA, au matumizi ya kadi za kibenki katika kufanya malipo ya VIZA. Kwa yale machache niliyokuelewa naomba nikujibu kama ifuatavyo;
1. Suala la kukaa muda mrefu hapo Airport ukisubiria taratibu za Ki-Uhamiaji ni sahihi kabisa kwa sababu ulitakiwa uombe VISA ukiwa nchini kwako kabla hujaja nchini ili taratibu za kiusalama kuendelea katika kubaini kama ni tishio kwa usalama wa nchi yetu au la.
2. Suala la kukusanya pesa na pasipoti sioni kama ni tatizo, tatizo kama hawapewi risiti.

3. Suala la matumizi ya kadi za kibenki kama VISA au American Express linahitaji miundombinu na utaalam, kama ujuavyo nchi yetu ni 3rd World huezi kulinganisha na huko Ulaya, Japan au Marekani, hivyo itafika wakati na sie tutafikia huko
 
Back
Top Bottom