Mhe. Rais, haya ndio tuyatakayo kwa nchi yetu... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mhe. Rais, haya ndio tuyatakayo kwa nchi yetu...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by majata, Jan 17, 2011.

 1. majata

  majata JF-Expert Member

  #1
  Jan 17, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 385
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 45
  1- Elimu Bora.
  2- Afya Bora.
  3- Makazi bora.
  4- Ajira za kutosha na zenye ujira bora.
  5- Haki sawa kwa wote bila kubagua rangi, dini wala kabila.

  Tunaimani kwamba serikali yetu inao uwezo wa kutupatia haya yote kwa ufanisi hata sasa bila kusubiri miaka mingi ijayo kama tu itabadili mbinu za kiutawala kuanzia serikali kuu mpaka serikali za mitaa kwa kusimamia vema matumizi ya kodi zetu pasipo ufisadi ambao ndio kikwazo kikubwa cha maendeleo ya nchi yetu.

  Toa matamko makali na wachukulie hatua kali wote wanao husishwa na ufisadi,wananchi tunaamini tangu ufisadi ugundulike hapa nchini wewe taarifa kamili za wahusika unazo, ila bado huwachukulii hatua kitu ambacho kinajenga hasira kwa wananchi na nihatari kwa usalama wetu.

  Mh JK, imani ile ambayo watu wengi walikuwa nayo kwako walipokupa dhamana hiyo mwaka 2005 imepotea kufwatia kukaa kwako kimya katika mambo yaliyowazi kabisa na kutotekeleza ahadi zako, usipokuwa makini uongozi wako utakuwa unaongoza kwa kutotekeleza ahadi zake na migogoro mingi kupita marais wote waliowahi na watakao tawala Tanzania, hutakumbukwa kwa mema, na historia itakuhukumu kwa yatokeayo katika uongozi wako.

  Watanzania tulio wengi sasa tumechoka kwakuwa humfanyi yale tunayoyataka, kufwatia ugumu wa maisha ndio maana tunjaribu kutafuta mkombozi wa kweli ambae anaweza kutukomboa hali hii inapelekea wengi tuanze kuunga mkono siasa za upinzani ambazo tunaona zinaukweli mwingi kuliko muendelezo wa hadaa za kutufanya hatuna macho na akili za ccm, Hata ccm ikifanya mema itapendwa tu ila Imechafuka na Inanuka Ufisadi na Rushwa hivyo haipendwi kabisa kwasasa.

  Mbona familia zenu nyie viongozi zina maisha mazuri sana?

  Nyie pia si ni watanzania pia kama sisi? Kwanini nyie tu ndio matajiri sana?

  JK wewe Binafsi una magorofa mangapi ukiacha lile unalojenga Bagamoyo?

  Mawaziri wako hasa wale waliopita mbona matajiri sana?

  Kwanini inashindikana kuwapa maisha bora watanzania wengine pia?

  "Acheni ubinafsi walipeni watanzania wote stahiki yao na si kuwadhulumu wanacho stahili".
   
Loading...