Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,197
- 25,516
- Mheshimiwa Rais Dr. John Pombe Magufuli ameshajipambanua kama mpenda kazi, uwajibikaji; mchukia rushwa na ufisadi na mwenye maono makubwa kwenye uwekezaji ili Serikali ipate kodi nyingi kwa maendeleo ya nchi yetu.
- Mheshimiwa Rais amekuwa akitoa maelezo na maelekezo, hasa kwa wateule wao, wahakikishe kuwa kuna utumishi wa kutukuka kwa wananchi na kutatua shida/changamoto zao. Huu ndiyo msimamo wake mwema kwa Taifa hili.
- Kila kada ya kimaisha ina changamoto zake. Wafanyabishara wana changamoto zao pia. Ni matumaini ya Mhe. Rais kuwa wateule wake watazitatua kero na changamoto hizo ili kuweka mazingira wezeshi na Rafiki kwa wawekezaji lengo kuu likiwa ni kupata walipakodi wa kutosha.
- Kodi husaidia maendeleo ya miundombinu na huduma nyinginezo za kijamii.
- Mhe. Rais pia amejipambanua kuwa ni Rais anayechukia rushwa na ufisadi kwa maneno na matendo yake. Hana urafiki wala huruma kwa mafisadi na walarushwa. Napo, wateule wake wanapaswa kuelekea uelekeo huo.
- Tuhuma dhidi ya Mkuu wa Wilaya ya Hai (kama zilivyo kwenye video niliyoiambatisha) si za kuzinyamazia. Kama mwananchi mzalendo, ninawiwa kuomba Mamlaka husika zichunguze tuhuma hizi na kuchukua hatua stahiki kwa Mhusika.
- Vitendo vinavyodaiwa kutendwa na Mkuu wa Wilaya anayedaiwa kujipamanua kama anayeripoti moja kwa moja kwa Mhe. Rais (nilidhani angeanzia kwa Mkuu wa Mkoa), si vitendo vyema. Vitendo hivyo hufifisha na kusawajisha taswira njema ya Mhe. Rais na Serikali yake kwa wananchi.
- Hatua stahiki zinapaswa kuchukuliwa kwa mujibu wa taratibu na sheria za nchi yetu pendwa Tanzania. Kwenda kinyume na vision na mission za Mhe. Rais si hujuma kwake?