Mhe. Paul Makonda; ziko wapi salamu za pole kwa wafiwa wa TBC? Ulihudhuria mazishi?

Entim

JF-Expert Member
Jun 7, 2013
4,021
2,253
Mhe. Paul C. Makonda, Mkuu wa Mkoa, Heri ya Pasaka!
Tunasikitika kukujulisha kuwa Taasisi kubwa ya TBC na Taifa kwa ujumla limepata pigo kubwa la kuondokewa na wapendwa wetu ambao ni watumishi wa TBC.
Hata hivyo, tofauti na utamaduni wako wa kujitokeza hadharani mara kwa mara, umeamua kutulia kweli bila kutoa salamu za pole? Mfano; Uliweza kufika kwenye kituo cha TBC?
Tunakusubiri kwenye mazishi na utoe salamu za pole, aidha tunatamani kusikia kauli yako kuhusu hali ya COVID 19 ndani ya mkoa wa DSM. Tuendelee kuchapa kazi? Tusio na kazi maalum tujitokeze kusafisha mitaro ya maji taka?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom