Mhe. Mussa Zungu mtetezi wa wanaoishi mabondeni una maoni gani juu ya mafuriko ya Dar? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mhe. Mussa Zungu mtetezi wa wanaoishi mabondeni una maoni gani juu ya mafuriko ya Dar?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Alwatan, Dec 22, 2011.

 1. Alwatan

  Alwatan JF-Expert Member

  #1
  Dec 22, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 409
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Wakati wa mjadala wa bajeti ya wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi, July mwaka huu. Huyu Mheshmiwa alikonekana kupinga kwa nguvu kubwa sana mpango wa wizara wa kuwahamisha wakazi wa maeneo ya mabondeni na maeneo hatarishi, kama wale wa bonde la msimbazi/jangwani. Mpango huu ulikua uwatafutie maeneo mbadala wakazi wote wa haya maeneo na kuacha eneo husika kama flood plain.

  Mheshmiwa huyu, aidha kwa kutafuta kuwafurahisha wapiga kura wake, bila ya kujali madhara ya upotevu wa maisha na mali yanayoweza kutokea pindi nature itapokasirika na kuleta gharika kama la mafuriko tunayoyashuhudia sasa hivi au ndiyo alichokiamini siwezi kujua. Watanzania tumekua ni watu wa kuchezewa kama pawns kwa ajili ya watu kujipatia umaarufu wa kisiasa(cheap popularity) bila ya ya viongozi kutazama the bigger picture ya kauli zao za kutafuta umaarufu bungeni.

  Nakumbuka Mheshmiwa Tibaijuka, ilimbidi abackpedal na kuacha hili suala la kuhamisha wanaokaa kwenye maeneo hatarishi liwe pending(sijui mpaka lini). Nimekua nikitazama picha za kusikitisha sana kutoka maeneo yaliyoathiriwa na haya mafuriko makubwa, na nimejitahidi kusaidia nilichojaaliwa. Lakini swali kubwa ninalobaki nalo ni je hivi mheshmiwa Mussa Zungu anajionaje wananchi wake wanapopata madhara makubwa kama haya huku yeye kama muwakilishi wao akishindwa kuwaongoza kwenye resettlement plan ya wizara.

  Mheshmiwa Zungu kwa heshima na taadhima tunaomba utoe ushirikiano kwa mamlaka husika ili mpango wa kuwahamisha mabondeni uendelee. Uongozi si tu kutoa maamuzi yanayofurahisha wengi kila wakati na kwenye kila situation, lakini vilevile ni pamoja na maamuzi yanayotazama the bigger picture ya maslahi kwa jamii nzima.
   
 2. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #2
  Dec 22, 2011
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,380
  Likes Received: 3,338
  Trophy Points: 280
  Wananchi wanafiki waliochagua mbunge mnafiki. Subiri Zungu akumbushwe huo upuuzi wake wa kukataa watu wa mabondeni wasihamishwe umsikie atakavyoleta viswahili vingi
   
 3. K

  KALABASH JF-Expert Member

  #3
  Dec 22, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 463
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Watu wa magezeti na Tv mnasubiri nini? Huu ndiyo wakati muafaka wa kwenda kumhoji mb Zungu na kupata msimamo wake.
   
 4. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #4
  Dec 22, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Atawapa majibu rahisi tu.Kwamba wasipotoshe na walimnukuu vibaya.FULL STOP!
   
 5. Sungurampole

  Sungurampole JF-Expert Member

  #5
  Dec 22, 2011
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 987
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Zungu ni mmoja wa wahanga wa kupoliticize kila jambo ambayo imekuwa tabia yetu- kuback pedal kwa waziri ndiyo tunachosema - SERIKALI LEGELEGE HAIWEZI KUSIMAMIA LOLOTE. Watu wanacommit suicide wanaachwa ili tupate kura sasa wanahatari ya kufa hayupo wakusema
   
Loading...