Mhe. Mulugo alishaonyesha kushindwa hata kabla hajaanza kusoma taarifa yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mhe. Mulugo alishaonyesha kushindwa hata kabla hajaanza kusoma taarifa yake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MpangoA, Oct 26, 2012.

 1. MpangoA

  MpangoA JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2012
  Joined: Jul 27, 2012
  Messages: 363
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wakuu Wanajamvi,

  Hili suala la Mhe. Mulugo mimi bado linanisumbua. Suala si kukosea kutamka, hili kila mtu linaweza kumtokea, bali mimi tatizo langu ni mambo aliyoyazungumzia (content). Honestly the content of his presentation was very weak and shallow.

  Naomba niwaambie, Mhe. Mulugo alishashindwa hata kabla hajaanza kutoa hiyo presentation. Chini hapo mtaona ratiba ya siku hiyo. Alitanguliwa na mawaziri wawili; kutoka Botswana na Zimbabwe (ndio huyo mtangulizi wake aliyetaka kujifananisha naye).

  Ukiangalia presentations mbili zilizotangulia, zote zinamuonyesha Mhe. Mulugo kwa mbali. Alionyesha kuwa na wasiwasi mkubwa na kujifariji kwa kunywa maji. Angalieni vizuri.

  Kuhusu content, mawaziri wote watatu walipewa mada moja: Education for Employment, Development Skills for Vocation. Sasa linganisha ubora wa presentations, jinsi mtu anavyo-present na ufahamu wa presenter juu ya kile anacho-present.

  TUNAHITAJI HURUMA YA MUNGU TU, MAANA VIONGOZI WETU WAMESHINDWA. KARIBUNI, LINKS ZIKO HAPO CHINI.

  Saturday 6th October 2012

  Opening Session – Welcome

  Mr Donald Grant – Minister of Education, Government of the Western Cape
  Hon. Prof. Hlengiwe Mkhize – Deputy Minister of Economic Development, South Africa

  Education for Employment, Developing Skills for Vocation
  Hon. Pelonomi Venson-Moitoi – Minister of Education & Skills Development, Botswana
  Hon. Senator David Coltart – Minister of Education, Sport, Arts & Culture, Zimbabwe
  Hon. Philipo Augustino Mulugo – Deputy Minister of Education and Vocational Training, Tanzania
  Mr Horst Weinert – Managing Director, Festo Didactic

  Presentation ya Waziri kutoka Botswana
  Hon. Pelonomi Venson-Moitoi – Minister of Education & Skills Development, Botswana | AfricanBrains - Innovation Africa

  Presentation ya Waziri kutoka Zimbabwe
  Hon. Senator David Coltart

  Presentation ya Waziri kutoka Tanzania (Mulugo)
  Hon. Philipo Augustino Mulugo

  source: Innovation Africa - Official Summit for Education, ICT, Science & Technology, Research & Development
   
 2. Mkuu rombo

  Mkuu rombo JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 18, 2012
  Messages: 1,559
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  aiseee hata sisi watu wa huku rombo 2nasikitika sana kwa hotuba aliyetowa waziri msaidizi
   
 3. controler

  controler JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2012
  Joined: Jul 3, 2012
  Messages: 1,537
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hata mwalimu wa horombo primary anamshinda waziri msaidizi au nasema uongo?
   
 4. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Sikonge huku hatuna la kusema. Labda kwa sababu bado tunaishi Tanganyika.
   
 5. Goodrich

  Goodrich JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 2,050
  Likes Received: 632
  Trophy Points: 280
  Ombi langu ni kwa MoDs !
  Nawaomba waiache hii mada kama ilivyo kwa kuwa inazungumzia mambo ambayo hayakubainishwa awali.
  Namuunga mkono mtoa mada maana hata mimi presentation ya Mulugo kwa ujumla ilinikumbusha darasa la tatu.
  Kwa kweli alitia aibu sssana !
   
 6. M

  Mercyless JF-Expert Member

  #6
  Oct 26, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 652
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Sina muda wa kumjadili kilaza kama Mulugo.
   
 7. m

  mchaichai JF-Expert Member

  #7
  Oct 26, 2012
  Joined: Nov 5, 2011
  Messages: 650
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nasema mulugo bado una muda wa kusoma kama huwezi kusoma huku unafanya kazi tunakuomba achia ngazi ukikataa utakuja kuumbuka siku moja...tutamwomba Sembeye akuite kwenye this week in perspective shauri yako kaka...piga msuli na walimu wa shule za english medium na soma vitabu sana jamaa yangu hali ni tete
   
 8. mzushi

  mzushi JF-Expert Member

  #8
  Oct 26, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,376
  Likes Received: 1,985
  Trophy Points: 280
  du sijui bwana mkubwa pale magogoni anangoja nini kumwajibisha huyu kilaza .kweli kupata uwaziri tanzania ni laini kama urojo wa Zanzibar ila kutoka ni sawasawa na ngamia kupenya kwenye tundu la sindano
   
 9. k

  kinauche JF-Expert Member

  #9
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 17, 2012
  Messages: 7,682
  Likes Received: 838
  Trophy Points: 280
  Tatizo la Mulugo siyo lugha bali ni uelewa mdogo wa mambo. Ni walimu wachache wa sampuli yake wanaoweza kudai Tanzania ilitokana na muungano wa Pemba, Zanzibar na Tanganyika. Kwa hiyosiyo suala la slip of the tongue bali ni suala la weledi. Hata hivyo, Waziri mwenye dhamana ya Elimu anatakiwa aifahamu vizuri lugha ya Kiingereza. Matamshi siyo tija sana lakini pamoja na hayo kusema jontromeni badala ya gentlemen, haikubaliki. Kama kweli ni mwalimu kama anavyodai, asingeweza kuanza ile presentation kama alivyoanza. Yeye akubali ni novice katika haya mambo. Aliwahi kuitisha mkutano wa walimu wakuu wa shule za msingi na sekondari wa Dar es Salaam akawa anasema, 'Mimi niko very care, I am very care. Sitaki kumwangusha Mhe. Kikwete.
   
 10. MPIGA ZEZE

  MPIGA ZEZE JF-Expert Member

  #10
  Oct 26, 2012
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 2,084
  Likes Received: 515
  Trophy Points: 280
  Kwa vile Mhe Rais Dkt JK ni mbishi (halali kiutawala) huwa hapendi kushinikizwa juu ya mawizi na watendaji wake wengine wanapovurunda, uwezekano wa Mhe Dkt Mulugo kujiuzulu ni mdogo kabisa. Lakini kwa vile maoni ya watu wengi ya kumtaka aachie ngazi yanasukumwa na moyo wa kuitakia mema nchi yetu na wala si 'wivu wa kike' (chambilecho watawala wapendavyo kujitetea wanapovurunda au kufisadi), basi njia mbadala tuliyobaki nayo ni kumwomba Mhe Rais Dkt JK ambadilishe nafasi - amtoe kwenye wizara ya elimu na ampeleke wizara nyingine yo yote ile ambayo Mhe Dkt Mulugo atachagua. Mhe Mulugo amepoteza uhalali wa kuwa kiongozi wa juu wa Elimu nchini. Wizara ya Elimu iachwe ipumuwe!
   
 11. brazilian

  brazilian JF-Expert Member

  #11
  Oct 26, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 607
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Siku akialikwa na Simbeye wa TBC lazima ataugua kiharusi. Hawezi kuthubutu kuhudhuria :Hali ni Tete sana
   
 12. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #12
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Mulugo hasi to step down, this should be the turning point to all those who like short-cuts in this country. Lazima Mhe apishe ofisi ya umma, watanzania katuaibisha sana, sijui kwa nini hana hata aibu? Mhe Mulugo, uko wizara nyeti ondoka kwa heshima.
   
 13. k

  katitu JF-Expert Member

  #13
  Oct 26, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 213
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  kwa hata mimi nilivyoisikiliza ile video nilishangaa sana.i was expect from him to say atleast i am and correct his statement but he did not
   
 14. Bhbm

  Bhbm JF-Expert Member

  #14
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 716
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Chezaea Jei Kei weweee ei kei ei mr. Dhaifu hahaha nimetoka kimlugolugoooo inhi inhi inhi.,.lol
   
 15. Mdakuzi

  Mdakuzi JF-Expert Member

  #15
  Oct 26, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 2,748
  Likes Received: 526
  Trophy Points: 280
  Viongozi wetu bwana, ni ngumu kweli kujivunia kuwa nao!
   
 16. Tigga Mumba

  Tigga Mumba JF-Expert Member

  #16
  Oct 26, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 747
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Aliniacha hoi aliposema.... I will end up with conclusion..... HahahaaaaaaaAAaaaaaa
   
 17. L

  LIpili Member

  #17
  Oct 26, 2012
  Joined: Apr 14, 2012
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiyo mada kulikuwa na haja ya kuanza kutaja mipaka ya nchi kweli?, au ni katika kujaziajazia .Haahaa JK ana kazi kwelikweli
   
 18. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #18
  Oct 26, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  ukiangalia katika hao waliotoa speech nchi zote hizo zinazungumza english kwenye mabunge yao na hata serikalini isipokua ya kwetu...jamaa alivoona wenzake english safi inapanda nafikiri alianza kupanic ndo mana akachemsha...simlaumu lakini nalaumu mifumo yetu hapa bongo kila kitu kiswahili haya tuone tutafika wapi
   
 19. j

  joshua_ok JF-Expert Member

  #19
  Oct 27, 2012
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 4,555
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  Daah! namchek hapa Mulugo kwa kweli ali-panic toka mwanzo. Yaani ni kama anajuta kwa nini alienda kwenye ule Mkutano but ndo ashafika mkutanoni hana namna kukimbia hawezi. But my advice kwa Watanzania wenzangu tuchukue jitihada binafsi kujifunza Kiingereza vinginevyo yatatukuta ya MULUGO, soma NOVEL, DAILY NEWS, SIKILIZA TV zinazotumia kiingereza BBC,CNN, AL JAZEERA angalia MOVIE za KIINGEREZA at least utaboresha KIINGEREZA chako vinginevyo ukikomalia KISWAHILI!!! yatakukuta ya MULUGO
   
 20. B

  BUBERWA D. JF-Expert Member

  #20
  Oct 27, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 446
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 45
  Nadhani huyu hata cheti cha form four alifoji. Haiwezekani umalize kidato cha nne ushindwe hata kusoma yaliyo andikwa. Mi niliwahi pata tetesi kuwa huyu jamaa ni ujanja ujanja shule hana aliungiwa mpango na mamaaa fulani kwa dhaifu apate uwaziri. Jamani wana mbeya nawaamini kwa kutuletea wasomi bungeni, ilikuwaje mkaleta huyukihiyo? Shame on you mbeya (songwe)people! Msirudie tena.
   
Loading...