Mwabhleja
JF-Expert Member
- Jan 27, 2016
- 1,351
- 2,061
Kuna falsafa moja Wamarekani wanapenda kuitumia wakisema, "LET US DOUBT EVERYTHING" na inawasaidia sana kufumbua mambo mbalimbali ambayo kwa namna moja au nyingine wananchi wanakuwa na kiu ya kuyafahamu.
Awali ya yote niseme nimpenda kwa namna ambavyo waziri mkuu Mhe. Kassim Majaliwa anavyochukua hatua mbalimbali za kuhakikisha serikali inatekeleza wajibu wake kwa raia ipasavyo. Naamini hata kipindi kile cha kina David Jairo angekuwa yeye ndiye waziri mkuu basi angechukua hatua badala ya kulalamika.
Vile vile naamini hata mwaka 2009 mauaji ya walemavu wa ngozi yaliposhamiri yeye angetoa suluhisho badala ya kulia hadharani kama alivyofanya Mzee wetu Kipenzi, Mizengo Pinda. Lakini pamoja na hayo, bado kuna jambo ambalo Mhe. Majaliwa hajalitekeleza kwa ufasaha nalo ni kutangaza mali zake. Hata Mhe. Rais Magufuli sijapata taarifa za kina kuhusiana na mali anazomiliki jambo ambalo linatia wasiwasi kwa watu hawa kujiweka huru. Mtindo wa mawaziri kujaza fomu za maadili na kuliwa na mende katika makabati yaliyonunuliwa kwa fedha za walalahoi tumezoea lakini sasa tunataka mabadiliko katika hili.
Ni wakati muafaka sasa kwa serikali ya Mhe. Magufuli kujiweka huru kwa kila mmoja ili tujue mapema amekuja na nini na siku akitoka serikali tushuhudia akitoka na vile vinavyowiana na namna alivyoingia.