Mbowe ambana Waziri Mkuu atoe kauli juu ya masuala yanayokwaza demokrasia na utawala bora

Unategemea kuna jibu litakalopatikana kutoka kwao, Utaambiwa mchakato wa kuwashughulikia wahusika unaendelea na tutapewa majibu bunge lijalo na inakuwa ndo imekwisha.

Waziri mkuu tuliye nae sijui kama ana uwezo wa kuchukua maamuzi magumu kama hayo ya kuwawajibisha wahusika au kutoa kauli ya walau kukemea mambo kama haya

Tuna serikali yenye watu ambao hawako tayari kuchukua maamuzi magumu ya kuwatetea wananchi wao au kupoigania maisha ya wananchi wao ila ipo serikali ambayo kila kukicha inazidi kuwagandamiza na kuwanyanyasa
 
Jamani, Pinda being a former TISS official, siyo ajabu kwa yeye kuwa mwongo! Uongo ni moja ya sifa kubwa ya kujiunga na hii taasisi!!
 
Unategemea kuna jibu litakalopatikana kutoka kwao
Utaambiwa mchakato wa kuwashughulikia wahusika unaendelea na tutapewa majibu bunge lijalo na inakuwa ndo imekwisha
Waziri mkuu tuliye nae sijui kama ana uwezo wa kuchukua maamuzi magumu kama hayo ya kuwawajibisha wahusika au kutoa kauli ya walau kukemea mambo kama haya

Tuna serikali yenye watu ambao hawako tayari kuchukua maamuzi magumu ya kuwatetea wananchi wao au kupoigania maisha ya wananchi wao ila ipo serikali ambayo kila kukicha inazidi kuwagandamiza na kuwanyanyasa

Kosa la Mheshimiwa Mbunge Mnyika kwamba Kikwete ni dhaifu liko wapi? Kama Rais ni dhaifu ni dhahiri serikali yake ni dhaifu kwa vile imeundwa na kiongozi dhaifu.

Kiongozi dhaifu atachagua wasaidizi dhaifu kama yeye ndio haya tunayoyaona.
 
Kweli kuongoza Tanzania ni kugumu sana maana unadanganya hivi hivi bila kupenda!!la sivyo utashindwa kuendesha serikali...funika kombe.....
 
Watu wenye busara na machungu ya nchi hii bado wapo. watanzania hatuna sababu yoyote ile ya kukata tamaa, naomba niwatie moyo kwamba, huki tunachokabiliana nacho ni moja ya sababu kuu ya matatizo tuliyonayo, tujitie nguvu na kukiondoa kabisa tukiweza tukitupe mto luvu kiwe chakula cha mamba, tuna miaka mitatu tu tumalizane nacho.
 
Kwa haraka haraka, watu wanaoishabikia ccm (au wapinzani wa chadema) point zao hazina mwelekeo wala mashiko, ni wazi kabisa kuwa kama hawa ni watu wenye akili timamu basi siyo bure wametumwa kufanya upotoshaji.

Sijaona hoja hata moja anayetoa analysis kujibu hoja za kambi rasmi ya upizania bungeni, at least even to try. Alafu imekuwa kama some kind of phenomena, utakuta kwenye almost kila thread JF (jukwaa la siasa) point yao kubwa ni 'ukabila', 'udini' au 'ukanda',wakitoka sana nje utasikia 'mara ooh Lema siyo mbunge, arusha imefulia', bila kujali kwamba thread inahusu nini, yani ni vituko tu.

Hata siku moja hawazungumzii mwanza, shinyanga, musoma, mbeya, iringa nk. Nadhani ingekuwa bora kama moderator anadelete au wafunguliwe thread zao nyingine alafu iwe inasomeka hivi 'ukabila, ukanda na udini katika hotuba ya kambi rasmi ya upizani bungeni'. Vinginevyo waafrika tutaendelea kudharaulika tu, Ehud Barak ataendelea kututukana, mataifa ya ulaya nayo yataendelea kututukana kama walivyofanya Spain hivi karibuni dhidi ya Uganda...(mwingine anaweza kuendelea).

Thread inahusu vitu vingine watu wameng'ana na udini, ukabila na ukanda. Inabidi Mnyika aje na mpya nyingine, 'tumefika hapa sababu ya....... na wendawazimu wa ccm.....mashalobaro wauza sura'.

Kwa wapenda maendeleo, wazalendo, watu wenye upeo, watu wenye nia njema na nchi hii, watu wenye visions, yaaaani washabiki na wapenzi wachadema the killing point is simple kwa hoja dhaifu kama hizi, ukishindwa kuwapuuza waropokaji waccm au wanape basi use this 'wakisema cdm sijue ni wadini, wakabila au wakanda, cdm waseme ccm wanagawa nchi kwa kutumia dini, ukabila na ukanda, ccm hawana sera wanatumia udini, ukabila na ukanda kutaka kudhoofisha upizani, kazi kubwa ya ccm toka nchi hii imepata uhuru nikuiba mali za umma na kuuza rasilimali za nchi kwa wawekezaji na Nyerere aliliona hilo, kwa kweli ccm inawatesa watanzania, ccm hawana jipya!!!'.
 
Wananchi naomba mwenye hotuba ya kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni aliyoitoa juzi bungeni aiweke hapa barazani. Natanguliza shukrani zangu
 
Wananchi naomba mwenye hotuba ya kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni aliyoitoa juzi bungeni aiweke hapa barazani. Natanguliza shukrani zangu
hii

Mbowe ambana Pinda polisi kuua raia

Kambi ya Upinzani bungeni imeitaka serikali kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ahadi ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuchunguza vifo vya raia vilivyotokea mikononi mwa askari polisi au vyombo vya dola. Julai mwaka jana, Pinda aliahidi kwamba serikali ingechunguza vifo hivyo kwa kutumia sheria ya Inquest kuchunguza mauaji ya raia wakiwa mikononi mwa vyombo vya dola.

Kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni, Freeman Mbowe, akitoa maoni ya upinzani kuhusu makadirio ya Ofisi Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha wa 2012/13 alisema pamoja na ahadi hiyo, bado kumekuwepo na mauaji ya kutisha na ya kikatili kwa raia wakiwa mikononi mwa polisi. Alisema taarifa ya Haki za Binadamu na Utawala Bora zinaonyesha kwamba vifo hivyo vimekuwa vikiongezeka kila mwaka na hakuna hatua zozote zinazochukuliwa.

Ni muhimu tukatambua kuwa kila kifo cha mtu ni tofauti na cha mwingine, na hutokea katika mazingira tofauti. Hivyo, kwa kuzingatia kilio cha wananchi ambao Serikali ina wajibu wa kuwalinda, vifo vyote ambavyo vimetokea kwa sababu ya matumizi ya nguvu, kikiwamo kifo cha raia kilichotokea akiwa chini ya uangalizi wa vyombo vya dola, ni vema serikali ikazingatia mazingira husika, alisema.

Alisema taarifa ya haki za binadamu ya mwaka jana inaeleza kwamba kuanzia Januari hadi Desemba 2011, takribani watu 25 wamefariki wakiwa mikononi mwa polisi na maafisa wengine wa ulinzi na matukio mengine yakiwaacha zaidi ya watu 50 na majeraha.

Alikumbusha kwamba ripoti hizo zinaonyesha mauaji ya raia mikononi mwa polisi yameendelea kuongezeka ambapo watu watano walifia mikononi mwa polisi mwaka 2008, watu 15 mwaka 2009 hadi watu 52 mwaka 2010 na katika kipindi cha Januari hadi Mei mwaka jana, watu 9 walikuwa wameripotiwa kuuawa katika eneo la Nyamongo, Tarime mkoani Mara.

Kambi ya Upinzani tunatambua kuwa taarifa hizi za mauaji zinawagusa askari Polisi pia kwa kuwa kwa mwaka uliopita katika maeneo ya Tarime, Tabora, Shinyanga, Arusha na Rukwa polisi watano waliuawa na wananchitunaamini kuwa kuacha kuchukua hatua dhidi ya polisi wachache wanaolichafua jeshi la polisi kwa ujumla inasababisha picha mbaya ya taifa letu kitaifa na kimataifa, alisema Mbowe.

Mbowe ambaye ni mbunge wa Hai (Chadema), alizungumzia pia unyanyasaji wa kisiasa unaowakuta wafuasi na viongozi wa vyama vya upinzani akieleza kwamba matukio hayo yamekuwa yakidhihirika zaidi kwenye chaguzi ndogo za madiwani, ubunge au vijiji na vitongoji hapa.

Alitolea mfano kujeruhiwa kwa wabunge wa Chadema wakati wa uchaguzi mdogo wa madiwani jijini Mwanza, Aprili mwaka huu (Highness Kiwia- Ilemelela na Salvatory Machemli- Ukerewe) walikatwa mapanga wakati wa uchaguzi mdogo wa Udiwani wa Kata ya Kirumba na wanaosadikiwa kuwa wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Alisema polisi wakishindwa kuzuia tukio hilo pamoja na kuwa walifika katika eneo la tukio tena wakiwa na silaha.

Manyanyaso haya hayawezi kuvumiliwa tena ni lazima kama taifa tujue kuwa nchi hii ni ya vyama vingi vya siasa na hivyo kila raia ana haki ya kujiunga na chama chochote cha siasa bila shinikizo. Hii ni kwa sababu bado mikutano ya kisiasa na hata mikutano ya waheshimiwa wabunge wa upinzani inavamiwa mara kwa mara mathalani uvamizi aliofanyiwa Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa, alisema Mbowe.

SHEREHE ZA UHURU, TAIFA
Akizungumzia maadhimisho mbalimbali, alisema siyo lazima sherehe zote zifanyike kila mwaka kwa kuwa zinatumia fedha nyingi bila tija huku akiitaka Serikali iweke wazi kiasi cha fedha kilichotumika kwenye maadhimisho ya Jubilee ya miaka 50 tangu Tanganyika ipate uhuru. Alisema gazeti moja liliripoti kwamba katika maadhimisho hayo, serikali ilitumia Sh. bilioni 64; taarifa ambazo hazikuwahi kukanushwa na serikali.

Kambi ya Upinzani inaitaka Serikali itoe tamko kuhusu matumizi hayo pamoja na mchanganuo wake ili kutekeleza dhana nzima ya uwazi na ukwelitaarifa za gharama za sherehe hizi za Kitaifa zikawekwa hadharani, zikiwemo gharama za mbio za mwenge ili umma wa Watanzania waweze kuchambua na kuona kama kweli bado ni tija na kipaumbele kwa Taifa kuendeleza sherehe hizi kwa mfumo tulio nao leo, alisema.

Alizungumzia tatizo la chaguzi nchini na kusema kuwa kumekuwa na ushahidi kuwa watendaji wa serikali wamekuwa wakiingilia mchakato huo kwa faida ya chama tawala.

Alinukuu barua ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara, B.B Kichinda, ya Mei 23, mwaka huu yenye Kumb. Na FA.291/300/08/25 kwenda kwa Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya na nakala zake kusambazwa kwa wakuu wote wa Wilaya za Mkoa wa Mara, iliyoeleza "Yah: Kusimamisha uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji katika mamlaka za serikali za mitaa"

Alisema katika barua hiyo, Kichinda aliwaelekeza watendaji hao kwamba chaguzi hizo zinasimamishwa ili kupisha uchaguzi wa CCM.

"Kwa barua hii ni dhahiri kuwa Katibu huyu amepewa maagizo kutoka ngazi ya juu na kwa mujibu wa tangazo la Serikali Na 51 la tarehe 17 Disemba, 2010 mwenye dhamana ya kutoa maelekezo hayo ni Waziri Mkuu kwani ndio msimamizi mkuu wa Tamisemi... barua hii ilifuatiwa na agizo la wakurugenzi watendaji wa Halmashauri mbalimbali za Wilaya za Mkoa wa Mara na kusimamisha chaguzi hizo," alisema.

Alimtaka Waziri Mkuu kutoa kauli ya Serikali juu ya kusimamishwa kwa chaguzi hizo ili kupisha uchaguzi wa CCM.
 
Re: Hotuba ya kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni - Mh Aikael Mbowe


Hakuna kiongozi mwenye jina hilo bungeni
 
Kuwataka waislam wadhbitiwe kwa kuwa wanasema vibaya makanisa huku akizitaka redio na magazeti ya kiislam yakionywa. Kwani Mbowe ni msemaji wa kanisa?

ni katika hotuba yake kwa ofisi ya waziri mkuu
 
Back
Top Bottom