Mhe. Majaliwa amesema viongozi wanatoka Kwa Mungu, najiuliza hata akina Sabaya walipewa mamlaka na Mungu? Vipi kuhusu viongozi wa uchafuzi 2020?

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Kwa sisi Mawakili wasomi kuhoji ni jadi yetu. Nimesikia Mhe. Waziri Mkuu akizungumzia kuhusu madaraka yanatoka Kwa Mungu. Nikajiuliza tunao wabunge wa bunge la Sasa ambapo wapo waliopita bila kupingwa na wengine walipitishwa na tume kuipitia uchafuzi, je hawa wote wanatoka kwa Mungu?

Tuna viongozi kama akina Sabaya, je nao kwa matendo yao tuseme wanatoka kwa Mungu? Lakini Kwanini Mungu ametupa akili ya kujua mema na mabaya? Siyo kwa ajili ya kutumia akili hizo hizo kufahamu viongozi wanaotoka Kwa Mungu na wafuasi wa shetani? Je, tunapobaini Kiongozi huyu ajatoka Kwa Mungu Kwanini tusimtoe?

Nadhani tunataka kunyamazisha watu wasifikiri kuhusu viongozi wa kutoka kwa Mungu na wasiotoka kwa Mungu, tunataka kuwaambia Watanzania kila kiongozi anatoka kwa Mungu which is wrong. Tuendelee kuwafichua viongozi wezi, wasiotenda haki, waonevu, washirikina nk na tuwaondoe maana awqtoki kwa Mungu
 
Nami huwa nawaza kama wewe, ivi enzi za JPM kweli Mungu alikuwa nasi kweli??
Watu wañapotea lenyewe liko ikulu linakuna mipua tu, watu wanapigwa shaba tena adharani lenyewe linashangilia tena ati Raisi anashiriki wizi wa kura kwa mjumbe wa nyumba kumi??
Akawapa vyeo akina sabaya wakawa wanalawiti dada zetu liJPM likimsifia na kumsupport.
In dictatorial state God is alway not there.
Mungu hajawai kuwepo nchi hii.Nchi yenye Mungu haiwezi kua na mambo ya ovyo na kijinga kama hivi.Kuna Mungu jina.Au labda wana maanisha mungu wao wakuchonga.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Mkuu;
Upo sahihi kwamba tunafanya mambo ya ovyo na ya kijinga. Lakini kuhusu MUNGU; Naomba kutofautiana kwa kusema yafuatayo:
Sisi sote ni wa MUNGU muumbaji wetu!
MUNGU katupa vingi sana! Katukamilisha!
Kaweka akili, utashi, utambuzi na uwezo wa kufanya maamuzi.
Yanayotokea ni matokeo ya maamuzi yetu. Ambayo kwa asilimia kubwa hutokana na sisi kutokutambua uwezo wetu wa asili.
Tumebaki watu wa maneno, lawama na uchawa.
Zaidi ya yote tunajikoroga na tunajitengenezea miungu wetu wenyewe!
Tunalazimisha utajiri wa fedha, sifa na madaraka katika mazingira yaletayo uchawa, woga, hofu, ujinga, ukatili, ushirikina, ushetani na mauti.
Tunamkumbuka MUNGU muumbaji wetu pindi mambo yanapoharibika vibaya!

MUNGU yupo! Lakini kamwe hawezi kutuletea uhuru, maendeleo, utawala au unafuu tunaoutaka. Hilo jukumu katuachia sisi!
Hii ni kwa sababu matatizo hayo ni ya kibinadamu na yanamalizwa kibinadamu!

Mfano mdogo: Wabunge haramu wapo Bungeni sasa ukitaka MUNGU awatoe utasubiri sana. Make atanya hivyo kwa ratiba yake! Jukumu lipo kwetu. Maamuzi tunayo sisi!
 
Hii nchi ina wapumbavu wengi sana, according to wapinzani nchi apewe Mbowe
 
Nami huwa nawaza kama wewe, ivi enzi za JPM kweli Mungu alikuwa nasi kweli??
Watu wañapotea lenyewe liko ikulu linakuna mipua tu, watu wanapigwa shaba tena adharani lenyewe linashangilia tena ati Raisi anashiriki wizi wa kura kwa mjumbe wa nyumba kumi??
Akawapa vyeo akina sabaya wakawa wanalawiti dada zetu liJPM likimsifia na kumsupport.
In dictatorial state God is alway not there.
MUNGU hajawahi kutuacha... Aliamua kudhihirisha ukuu wake kwa ratiba yake!
 
Hii nchi ina wapumbavu wengi sana, according to wapinzani nchi apewe Mbowe
Hata akipewa bado hao wapumbavu kwa kuwa ni wengi sana watamsumbua.
Tufanyeni jitihada kuwapunguza kwanza!
Kama mnavyozungumzia betting, pisi kali na timu zenu za Ulaya... Please zungumzieni pia mapungufu ya utawala uliopo madarakani. Amsheni shauku na ari ya wapumbavu kuacha upumbavu!
 
Ukimuamini mwanasiasa yeyote pasipo Na sheria kali umeliwa!

Who’s majaliwa ukiondoa iko cheo chake? Ana maana kwa wale anaowakisha Siyo kwetu watanzania.

Afanye yake aachane na Sisi.

Maisha baina ya Watu hayawezi kuendeshwa kwa msingi wa kuaminiana Bali kwa misingi ya Kukabana Roho kwa Sheria.

Nchi hii eti kiongozi anaonekana ana Power kuliko Mwananchi ajabu Kweli!!

Anyway Watz wengi are not politically Mature, ni swala la muda tuu watatwangana kuleta Revolution katika nchi hii
 
Hata akipewa bado hao wapumbavu kwa kuwa ni wengi sana watamsumbua.
Tufanyeni jitihada kuwapunguza kwanza!
Kama mnavyozungumzia betting, pisi kali na timu zenu za Ulaya... Please zungumzieni pia mapungufu ya utawala uliopo madarakani. Amsheni shauku na ari ya wapumbavu kuacha upumbavu!
2015-2020 ilikuwa ni dhambi kubwa kuukosoa utawala, tulikuwa tunaongozwa na malaika, Nyambaf zenu
 
Kwa sisi Mawakili wasomi kuhoji ni jadi yetu. Nimesikia Mhe. Waziri Mkuu akizungumzia kuhusu madaraka yanatoka Kwa Mungu. Nikajiuliza tunao wabunge wa bunge la Sasa ambapo wapo waliopita bila kupingwa na wengine walipitishwa na tume kuipitia uchafuzi, je hawa wote wanatoka kwa Mungu?

Tuna viongozi kama akina Sabaya, je nao kwa matendo yao tuseme wanatoka kwa Mungu? Lakini Kwanini Mungu ametupa akili ya kujua mema na mabaya? Siyo kwa ajili ya kutumia akili hizo hizo kufahamu viongozi wanaotoka Kwa Mungu na wafuasi wa shetani? Je, tunapobaini Kiongozi huyu ajatoka Kwa Mungu Kwanini tusimtoe?

Nadhani tunataka kunyamazisha watu wasifikiri kuhusu viongozi wa kutoka kwa Mungu na wasiotoka kwa Mungu, tunataka kuwaambia Watanzania kila kiongozi anatoka kwa Mungu which is wrong. Tuendelee kuwafichua viongozi wezi, wasiotenda haki, waonevu, washirikina nk na tuwaondoe maana awqtoki kwa Mungu
ndio wanatoka kwa mungu ila sio Mungu
 
Jumuiya ya uislam imkanye huyu kuongelea uongo wake misikitini au wanamuogopa? Maja hajawahi ongea ukweli
 
kila kitu kinatoka kwa mungu hadi shetani mwenyewe, kinachotuhukum sisi ni free will ya matendo yetu, sabaya anahukumiwa na matendo yake.
 
Kwa sisi Mawakili wasomi kuhoji ni jadi yetu. Nimesikia Mhe. Waziri Mkuu akizungumzia kuhusu madaraka yanatoka Kwa Mungu. Nikajiuliza tunao wabunge wa bunge la Sasa ambapo wapo waliopita bila kupingwa na wengine walipitishwa na tume kuipitia uchafuzi, je hawa wote wanatoka kwa Mungu?

Tuna viongozi kama akina Sabaya, je nao kwa matendo yao tuseme wanatoka kwa Mungu? Lakini Kwanini Mungu ametupa akili ya kujua mema na mabaya? Siyo kwa ajili ya kutumia akili hizo hizo kufahamu viongozi wanaotoka Kwa Mungu na wafuasi wa shetani? Je, tunapobaini Kiongozi huyu ajatoka Kwa Mungu Kwanini tusimtoe?

Nadhani tunataka kunyamazisha watu wasifikiri kuhusu viongozi wa kutoka kwa Mungu na wasiotoka kwa Mungu, tunataka kuwaambia Watanzania kila kiongozi anatoka kwa Mungu which is wrong. Tuendelee kuwafichua viongozi wezi, wasiotenda haki, waonevu, washirikina nk na tuwaondoe maana awqtoki kwa Mungu
Kwahiyo Mungu alimtumbua Magufuli kwa utovu wa nidhamu akamsimika Hangaya! Huwa tunaongea bila kufikiri.
 
Kwa sisi Mawakili wasomi kuhoji ni jadi yetu. Nimesikia Mhe. Waziri Mkuu akizungumzia kuhusu madaraka yanatoka Kwa Mungu. Nikajiuliza tunao wabunge wa bunge la Sasa ambapo wapo waliopita bila kupingwa na wengine walipitishwa na tume kuipitia uchafuzi, je hawa wote wanatoka kwa Mungu?

Tuna viongozi kama akina Sabaya, je nao kwa matendo yao tuseme wanatoka kwa Mungu? Lakini Kwanini Mungu ametupa akili ya kujua mema na mabaya? Siyo kwa ajili ya kutumia akili hizo hizo kufahamu viongozi wanaotoka Kwa Mungu na wafuasi wa shetani? Je, tunapobaini Kiongozi huyu ajatoka Kwa Mungu Kwanini tusimtoe?

Nadhani tunataka kunyamazisha watu wasifikiri kuhusu viongozi wa kutoka kwa Mungu na wasiotoka kwa Mungu, tunataka kuwaambia Watanzania kila kiongozi anatoka kwa Mungu which is wrong. Tuendelee kuwafichua viongozi wezi, wasiotenda haki, waonevu, washirikina nk na tuwaondoe maana awqtoki kwa Mungu
Kwa hiyo anamaanisha viongozi wote peponi
 
Viongozi wazuri ama wabaya woote ni mipango ya Mungu. Kinasabaya walitokea ili tujifunze mpumbavu akipata cheo nini hutokea...
Sanyingine Mungu huacha viongoz katili washike nchi ili wananchi wazinduke... ajabu watz hawazinduki.
Kwamatatizo ya mwendazake ilibidi Leo kilammoja adai katiba mpya haraka lkn wapi!!!! Tumepitia mfano;
-uchaguzi mchafu
-ubaguzi kimaendeleo kujali kwake
-vipaumbele binafsi sio vyakitaifa
-uteuzi wa kiupendeleo kanda yake
-kutisha wakosoaji na kuwadhuru
-kuliingilia bunge na mahakama
-kutojali katiba
-kuua demokrasia
-kukopa atakavyo
-kusitisha mchakato wa katiba
-Kuvuruga watumishi kunyima haki
-kununua midege madarasa hatuna
-kukimbiza wakosoaji nchini
-korona kuua yeye kutojali
-kutukana kufukuza hovyo na kurudisha akisifiwa sana
-kuizamisha kaskazini
-kusema wazi usiponichagua sikupi maendeleo (ubaguzi)
-kuteka watu na kupora Mali zawatu hovyo...
Yooote bado wananchi wanazubaaa hawajui wafanyaje
 
Mkuu;
Upo sahihi kwamba tunafanya mambo ya ovyo na ya kijinga. Lakini kuhusu MUNGU; Naomba kutofautiana kwa kusema yafuatayo:
Sisi sote ni wa MUNGU muumbaji wetu!
MUNGU katupa vingi sana! Katukamilisha!
Kaweka akili, utashi, utambuzi na uwezo wa kufanya maamuzi.
Yanayotokea ni matokeo ya maamuzi yetu. Ambayo kwa asilimia kubwa hutokana na sisi kutokutambua uwezo wetu wa asili.
Tumebaki watu wa maneno, lawama na uchawa.
Zaidi ya yote tunajikoroka na tunajitengenezea miungu wetu wenyewe!
Tunalazimisha utajiri wa fedha, sifa na madaraka katika mazingira yaletayo uchawa, woga, hofu, ujinga, ukatili, ushirikina, ushetani na mauti.
Tunamkumbuka MUNGU muumbaji wetu pindi mambo yanapoharibika vibaya!

MUNGU yupo! Lakini kamwe hawezi kutuletea uhuru, maendeleo, utawala au unafuu tunaoutaka. Hilo jukumu katuachia sisi!
Hii ni kwa sababu matatizo hayo ni ya kibinadamu na yanamalizwa kibinadamu!

Mfano mdogo: Wabunge haramu wapo Bungeni sasa ukitaka MUNGU awatoe utasubiri sana. Make atanya hivyo kwa ratiba yake! Jukumu lipo kwetu. Maamuzi tunayo sisi!
Mungu ametupa akili ya kujua mema na mabaya pia nguvu za kutenda kwa kuitumia hiyo.
Mengine tunamsingizia tu na ni dhambi kumhusisha moja kwa moja na ujinga au uzembe wetu duniani.
Mungu anataka tupange na kutenda mambo yetu kwa ufanisi ikiwemo kuchagua viongozi wazuri na kuondoa wabaya.
 
Mungu yupo na ndiye anayeruhusu yote haya na akiona nafasi aliyokupa unaitumia vibaya ndo hayo yaliyowapata wahusika
 
kwenye riziki Mungu hachagui wa kumpa yeye anakupa tu lkn akili kichwani mwako maana Satan alimuacha pia atujaribu Imani zetu kwamba je,tunajali kwamba Mungu ndo aliyenitaka niwe hapa au la?

sasa wengine maarifa hayo hawana ndo maana tuna watu km sabaya,Makonda nk
 
Wanapenda kutumia kauli hiyo ya kwamba kiongozi utoka kwa Mungu ili kuhalalisha dhuruma zao wanazowafanyia wananchi kipindi cha upigaji kura na baada ya kipindi hicho.
 
Back
Top Bottom