field marshall1
JF-Expert Member
- Sep 17, 2017
- 1,171
- 2,730
Nimesikiliza hotuba ya rais Magufuli akisema watu wazaane sana na wanawake waachie mayai yao, akawatupia dongo wanao-support uzazi wa mpango kuwa wabanie mayai yao
Naomba nikushauri mheshimiwa rais kuwa UMEKOSEA, kuwa na idadi kubwa (High population) hakumaanishi kuwa kutailetea nchi utajiri. Mfano ulioutoa wa Nigeria, China na India hauakisi utajiri kwani hizi nchi bado zipo dunia ya tatu yaani ni bado ni nchi zinazoendelea (developing nations), Nchi ulizozitaja zina hali mbaya sana kwa uchumi wa raia zake ila ukihesabu kwa GDP-PPP zina namba kubwa kutokana na idadi ya watu lakini wengi wa wananchi wao ni maskini wa kutupwa, mfano Nigeria asilimia 25 ya watu wake ndiyo wana umeme, vijiji na miji imechoka, uhalifu ni kila mahali, machinga ni kila mahali, mauaji ni kila kona hakuna unafuu wowote, China ina GDP- Purchasing power parity kutokana na idadi yake kubwa ya watu lakini bado nchi imechoka ile mbaya ndiyo maana mnaona wachina wengi wanakuja Africa na kufanya biashara za umachinga na kuchoma mahindi, Hali ya maisha ya China ni mbaya sana ndiyo maana uhalifu na wizi ni mkubwa sana tofauti na nchi jirani yenye idadi ndogo ya watu lakini ina strong institution kama Taiwan, Singapore, South Korea au Malaysia.
Mfano ukiangalia USA yenye watu Mil.300 na China yenye watu 1.6 Billions (Zaidi ya mara tano), GDP (Gross Domestic product) nominal ambayo inamgusa kila mtu, kwa USA ni mara 7 zaidi ya China. China zaidi ya watu millioni 450 ni mafukara wa kutupwa, walio na kazi (Middle class) wanalipwa chini ya Dollar 900 kwa mwezi na ni hao wanaofanya kazi kwenye makampuni ya nchi za Magharibi, hivyo hivyo kwa India, Bangladesh, Nigeria na Indonesia.
Mhe. Rais, idadi tuliyonayo tunashindwa kuihudumia hata kwa afya ya msingi tu, hospitali zetu zenye huduma mbovu zinaelemewa sasa kwa idadi hii,je tukiwa na idadi kubwa ya watu wasio na kazi tutaweza kweli.
Utamaduni wetu ni tofauti sana ukilinganisha na nchi nyingine, watu wengi si kwamba hawana mitaji lakini pia hawana utamaduni (culture) ya kufanya kazi kwa bidii, tutaendelea kuzalisha wezi, majambazi nk,
Mhe. Rais usidanganywe na hao wanaokwambia tukiwa na idadi kubwa ya watu ndiyo tutakuwa matajiri....Angalia nchi zenye watu wachache kama Seychelles, Mauritius, Namibia nk zinavyofanya vizuri kiuchumi kulinganisha na nchi zenye watu wengi. Mifano mingine ni Qatar, Kuwaiti, Luxembourg, France, UK, Ireland (Mifano ni mingi)
Kumalizia si kweli kuwa idadi kubwa ya watu ni muhimu kwenye uchumi. Utajiri wetu utapatikana kwa watu kufanya kazi za kujituma, za maarifa, sayansi na ugunduzi lakini siyo za wamachinga.
Hivi kazi za kuuza bidhaa za watu wengine kwa population ya ndani kutawaondolea watu umaskini? Hatutaweza, lazima tuseme ukweli.