Mhe. Lungu; I am not bulldozing but am walking my words

msambaru

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
245
109
Salamu waungwana,

Jana nilibahatika kuangalia kupitia tv mazungumzo ya Rais wa Zambia mhe. Lungu na Mhe. Magufuli wakiwa na maafisa mbalimbali toka nchi mbili, ikawa kila mmoja alipomaliza kuongea aliulizwa maswali mawili,

Mhe. Lungu aliulizwa na mzambia, kuwa amejifunza nn kutoka kwa Magufuli ikiwa Magufuli amejinasibu kama bulldozer, Mhe. Lungu alijibu kuwa yeye anatembea katika maneno yake (ahadi alizotoa),

Ila bulldozing inaweza poteza muelekeo au kwa maguvu yake ikaleta maonevu, kauli hii imenitafakarisha sana, nikaona niwashirikishe na tumuombee Rais wetu aendelee kubulldoze to the right direction.

Nawasilisha.
 
hahahaha jamaa kampa makavu sema lungu alikuwa anatema lugha ya malikia sijui kama BWANA YULE aling'amua hilo fumbo.


swissme
Aisee tunatatizo kubwa sana katika lugha, yani hata mkalmani wake ni shida na matatizo tupu, poor English.

Bob naye anazidi kupotea, swanglish ilikuwa mbovu sana, hakueleweka anasimamia lugha ipi katika hotuba yake.
Kuna kitu nimejifunza, kama baraza la KISWAHILI lisipofanya haraka kuchukua hatua za haraka, basi kuna kizazi kinakuja hakitokuwa kinajiua KISWAHILI wala Kiingereza.
 
Kila Taifa linapitia nyakati zake, na nyakati hutofautiana, mahitaji ya Tanzania kwa sasa sio mahitaji ya Zambia kwa namna ya uongozi unaohitajika. Magufuli fits perfectly well.
 
Mi nipo hapa Lusaka, toka mwaka jana. Mbona maisha ya hapa ni shida tu bora bongo!!! Watu wake huku wako hoi, mishahara inachelewa mpaka tarehe 4.watumish pia hawajapandishwa vyeo
 
Hawa ndio marais wenye hekma.siyo yule anayefuata Sera za ndugu zake wa Rwanda na Uganda.
 
Kila Taifa linapitia nyakati zake, na nyakati hutofautiana, mahitaji ya Tanzania kwa sasa sio mahitaji ya Zambia kwa namna ya uongozi unaohitajika. Magufuli fits perfectly well.

You have never given any constructive opinion, your avatar fits you fits perfectly well
 
Back
Top Bottom