Mhe. Lema Umesema Kweli, Tatizo sio Magufuli bali ni Bunge na Mawaziri

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,745
71,103
Jana tarehe 31/11 katika kikao cha brief cha wabunge kabla ya kuanza vikao vya leo vya kawaida mbunge wa Arusha aliwashukia wabunge na mawaziri na kusema kuwa Rais Magufuli ana laumiwa kwa tabia zake za kutofuata sheria na katiba kwa sababu Wabunge na Mawaziri hawatimizi wajibu wao wa kumkosoa na kumshauri mpaka amefikia kuona kila afanyacho ni sawa kwani anao uhakika kuwa atapongezwa na kusifiwa na hao watu.

Mawaziri ni waoga wa kutenda wanayopaswa hadi wasubiri waambiwe cha kufanya kwa woga, katoa mfano wa Simbachawene baada ya kuambiwa na Lema juu ya utendaji mbovu wa Mkurugezi wa Arusha yeye akamuambia nendeni mfanye fujo ili nipate pa kuanzia. Ajabu waziri kujibu hivyo. Hata alipo mwambia Waziri mkuu kuhusu jibu la waziri wake naye kagwaya hana cha kusema kwa vile anamuogopa Rais.

Kwa vile Bunge sasa hivi lipo pamoja Dodoma na Mawaziri wapo hapo tutumie kauli mbiu ya Lema kuwashinikiza wafanye wajibu wao bila kujali itikadi kwani nje ya Bunge wanaoumia ni wananchi wote bila kujali itikadi zao. Tunataka Bunge lichukue nafasi yake kuwashinikiza mawaziri wamshauri Rais afanye anayopaswa kufanya kuokoa taifa linalo angamia kabla mambo hayajawa mabaya zaidi.
 
Inasikitisha sana. Hilo jibu la Simbachawene km ni kweli anapaswa aajibike mara moja. Hii ni aina ya uongozi unaolivua nguo taifa. Eti kafanyeni fujo nipate pa kuanzia? Mungu wangu. Hv watu wakiuawa, kuumia ndio kigezo cha kumfanya waziri atimize wajibu wake?. Haya serikali ituambie ni wangapi wameumizwa kwa vigezo kama hivi?. Waziri mkuu naye yuko kimya baada ya kujuzwa?. Tanzania yangu jamani!
 
Hivi mpaka leo kuna wanaomwamini Lema?
Me nashangaa sana hivi kwenye masirahi mapana ya taifa bado tunahoji uhalali wa mtoa taarifa nani hajui kinachoendelea sasa hivi huko serikali, uliwahi kuona wapi taifa linaendesha kwa kauli na matukio ya mtu mmoja, ni vema kama taifa tukawa na mfumo mmoja wa maamuzi shirikishi hata wale walio na dhamana ya juu ya uongozi waone ni busara kuwashilikisha hawa wa chini ili pasitokee sintofahamu kama hizi za sasa.....
 
Kama Bunge na Mawaziri wakim tight JPM hawezi kuendelea na mtindo huu wa utawala la sivyo ile dhana kuwa ni Dikteta itajionyesha wazi.

Kwa hulka ya JPM atampoteza mmoja mmoja anayemjaribu mpaka waishe kabla mkakati wao haujafanikiwa, you bet! Anajua skelletons zao wote na soft spot ya kupiga panapouma zaidi! sio bure hata wao wanajua wanachofanya kwa sababu wanayajua madhambi yao, wengi wao wamafanyanae kazi kwa muda mrefu, they know what he is made of and what makes him tick! sio wajinga sana kama wanavyodhaniwa, la hasha! Wengi wao wanavuta subira waone mwelekeo wa upepo kabla hawajajitia muhanga, kumbuka dhana hii; "kama huwezi kupambana nae, basi jiunge nae" hii ndio njia salama wabunge wa CCM na mawaziri wao waliyochagua, na kwa bahati nzuri JPM analaijua hilo na hana wasiwasi!
 
Waache woga wanamtetemekea hivo kwa nini hao mawaziri?aisee kweli jamaa ana act kama Mungu.yaani kumbe wanatetemeka hivo
 
Back
Top Bottom