geraldkowero1
JF-Expert Member
- Jul 5, 2014
- 1,838
- 644
Unasema kuna emails lukuki, ebu tuma tuzione hapa, tusije jadili mambo ambayo hayana ushahidi dhidi ya mtu ambaye ajapata mahali pa kujitetea. Ila huyu Edward uliyemtaja hapa namfahamu na inakuwa ngumu kwangu kuamini kuwa ni mtu wa namna ya unavyotaka kutuaminisha. Na ukweli uliopo Selasini amekuwa akijitenga na mambo mengi yanayohusu chama kitaifa na hata vijana wameanza kukata nae tamaa labda utuambie ameaanza kubadilika hivi karibuni baada ya kusoma nyakati.
Nimeonelea nisome kwanza michango ya wachangiaji kabla sija comment lolote kumhusu huyu m-bunge wetu wa Rombo mh. Selasini. Kwa kweli na ki-mungu huwezi kubeza mchango wa huyu m-bunge jimboni kwake Rombo. Pia ni fedheha kubwa kumlinganisha ki utendaji na Shibuda. Selasini kwa kawaida ni mtendaji zaidi kuliko kuongea ongea na kujitafutia sifa binafsi. Ukitaka kuliona hilo angalia matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa uliomalizika hivi karibuni. Rombo imepaa ukilinganisha na majimbo mengi na la mh.Mbowe likiwemo. Angalia jimbo la mh. Lissu nalo limepaa. Hii maana yake pana uhai wa chama pale. Wengi niliosoma michango yao hawana hoja zenye mashiko zaidi ya kubwabwaja tu bila pointi za maana. Wangekuwa kweli wanachama wa chadema hoja zao wangepeleka kwenye vikao halali vya chama na sio kuletwa mitandaoni. Kukaa tu na kushusha lawama hakukisaidii chama. Watuambie walishamwona mara ngapi m-bunge wao na kutoa ushauri wao na asiwasikilize? Kwani haipo ofisi ya m-bunge Rombo? Wao wanadhani ipo pale kupokea malalamiko ya wananchi tu au ni pamoja na wananchi kukutana na m-bunge wao na kushauriana nae kuhusu masuala mbali mbali yanayolihusu jimbo? Wasichokijua ni kwamba uongozi wa juu wa chama hawafanyi maamuzi makubwa kiasi hicho kwa kuchukua maoni ya mitandaoni. Sasa niwaombe wote wanaotaka nafasi hizo kuanzia udiwani, ubunge na hata zaidi ya hapo waache kuchafuana mitandaoni na wasubiri muda muafaka wafuate taratibu zitakazowekwa na chama. Hatari ya kuendeleza haya ni kukipa upenyo chama tawala kupita kirahisi jambo litakalokuwa ni pigo sio kwa chadema tu bali ukawa kwa ujumla. Naomba mtafakari huu ushauri.