Mhe. January Makamba akunwa na hotuba ya JK | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mhe. January Makamba akunwa na hotuba ya JK

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ustaadh, Jan 2, 2011.

 1. Ustaadh

  Ustaadh JF-Expert Member

  #1
  Jan 2, 2011
  Joined: Oct 25, 2009
  Messages: 413
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  MBUNGE wa Bumbuli, January Makamba, ameguswa na hotuba ya Rais Kikwete ya Mwaka Mpya na kumpongeza kwa kuunda Tume ya Maalumu ya Katiba, huku akisema wanaodai mfumo wa kuunda Tume kukusanya maoni haufai, wanakosea.

  January aliliambia gazeti hili jana kuwa Tume anayounda Rais Kikwete ni mpya kabisa, kwani huko nyuma hakukuwahi kuundwa Tume ya kupitia Katiba.

  “Nampongeza Rais Kikwete kwa hotuba yake nzuri, na kwa uamuzi wake wa kuanzisha mchakato wa Katiba mpya.

  Hii Tume atakayounda ni Tume mpya kabisa, huko nyuma hakujawahi kuundwa Tume ya kupitia Katiba,” alisema January.

  “Tume za Nyalali (Jaji Mkuu mstaafu Francis) na Kisanga (Jaji mstaafu Robert), zilikuwa na majukumu mengine kabisa na si kupitia Katiba.”

  Mbunge huyo aliyekuwa Msaidizi wa Rais Kikwete kabla ya kujitosa kuwania ubunge katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, alisema kwa hiyo wanaodai kwamba mfumo wa kutumia Tume kukusanya maoni haufai, wanakosea.

  “Kote duniani ndio utaratibu. Zile hoja zinazotaka kupelekwa bungeni kwamba Bunge liweke utaratibu wa kukusanya maoni, ni hoja za kutafuta umaarufu tu.

  “Rais wetu amechukua uongozi kwenye jambo hili, mimi na watu wa Bumbuli tuna imani litafika pazuri na sisi (wabunge) bungeni tutaletewa katika wakati mwafaka kiutaratibu,” alisema January.

  Katika hotuba yake ya Mwaka Mpya juzi kwa Taifa, Rais Kikwete alisema anaunda Tume maalumu ya Katiba ambayo itaongozwa na mwanasheria aliyebobea na kuundwa na wajumbe kutoka makundi mbalimbali ya jamii za pande zote mbili za Muungano.

  “Jukumu la msingi la Tume hiyo litakuwa ni kuongoza na kuratibu mchakato utakaoshirikisha wananchi wote bila kubagua vyama vya siasa, wanasiasa, wafanyabiashara, asasi za kiraia, mashirika ya dini, wanataaluma na makundi mbalimbali ya watu wa nchi yetu kote nchini, kutoa maoni yao juu ya yatakayohusu Katiba ya nchi yao,” alisema Rais Kikwete.

  Kauli ya Rais Kikwete imekuja baada ya kuwapo kwa mjadala mkali wa kuandikwa kwa Katiba
  mpya, kutoka kwa vyama vya siasa na wadau wengine nchini baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu mwaka jana.

  Waziri Mkuu Mizengo Pinda katika mkutano wake na wahariri wa vyombo vya habari Dar es Salaam wiki mbili zilizopita, alisema atamshauri Rais Kikwete juu ya kuunda jopo la wataalamu kushughulikia suala hilo la madai ya Katiba mpya.

  Pinda alisema Serikali haikuwa na kigugumizi wala tatizo na hoja ya mabadiliko ya Katiba, na kueleza kuwa anaamini wanaotoa madai hayo wana hoja.

  Katika mjadala huo, Mbunge wa Ubungo, John Mnyika aliwasilisha hoja binafsi katika Ofisi ya Bunge, akitaka suala la Katiba mpya lijadiliwe na Bunge, akisema kuundwa kwa Tume ni kukosea, akihusisha na Tume zilizoundwa huko nyuma kwamba maoni yao hayakufanyiwa kazi na watawala.

  Nyalali aliwahi kuongoza Tume iliyokuwa na jukumu la kutazama kama Tanzania ilikuwa tayari kwa mfumo wa vyama vingi na sheria nyingine zinazodaiwa ni kandamizi.

  Jaji Kisanga aliongoza Tume iliyokusanya maoni ikijulikana kama White Paper mwaka 1996; na zote baadhi ya mapendekezo yao yalifanyika kazi na Serikali zilizokuwapo.
  ...........
  My take: Tumekuwa na tabia ya kuunda tume lakini huwa mara nyingi tunapuuza matokeo ya hizo tume!
   
 2. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #2
  Jan 2, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Kwani hata Tume ya taifa ya Uchaguzi si tuliipongeza? Unafiki tu hakuna kitu hapo
   
 3. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #3
  Jan 2, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Kwa Januari kukunwa na hotuba ya jk inatusaidia nini sasa. Watu wengine bwana!! Acha kupoteza muda wako kuandika jambo lisilo na mvuto kwa jamii. Kuna tofauti gani kati ya januari na jk!!??
   
 4. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #4
  Jan 2, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,515
  Likes Received: 1,685
  Trophy Points: 280
  January Yusuph Rajab Makamba nikukumbushe kuwa UKITAKA HESHIMA/UMAARUFU KWA NGUVU UTANUNUA DHARAU KWA BEI RAHISI. Zipo tume kibao zimeundwa na waheshimiwa marais, wametoa mchango gani? Tume ya jaji mmoja uliyemtaja hapo juu si ndo ilishushuliwa na BWM? Hapa tusijidanganye kwa kuundwa tume, what are going to get out of it ndo cha msingi
   
 5. A

  AmaniKatoshi Senior Member

  #5
  Jan 2, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 158
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hivi waliomaliza galanosi secondary mwaka 1993 wanamkumbuka huyu January Makamba? Hebu tuambieni mnayokumbuka!
   
 6. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #6
  Jan 2, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Nionavyo mimi bana ni heri ya mtu anayetafuta umaarufu kwa hoja kuliko mtu anayejikomba ili apande kwene piramidi za uongozi.
   
 7. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #7
  Jan 2, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  huyu anatafuta cheap popolarity..anataka kuvamia caliber za akina Mnyika, Mdee et al.
  Kaza buti kama unataka jamii ikuheshimu..achana na hizi kauli za kisanii..zitakubomoa vibaya sana!!
   
 8. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #8
  Jan 2, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mimi sometimes waandishi wetu siwaelewi; Hivi kwanini walimfuata? ili awape news huh?? Hivi unategemea nini from January... aseme hakubali? au hajakunwa na hotuba ya JK?

  In short naona Kikwete is playing us big time, he using dirty tricks used by his predecessors and worse enough, haya ma timu/kamisheni nk. ni kufuja tu pesa and sometimes they are usually edited to fit our leadership needs
   
 9. m

  mams JF-Expert Member

  #9
  Jan 2, 2011
  Joined: Jul 19, 2009
  Messages: 616
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Hakuna jipya!
   
 10. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #10
  Jan 2, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Suala la katiba CCM lazima itapiga chenga ya mwili..ilivyo sasa ni kwamba iko jikoni kuipanga hiyo chenga. CCM haiwezi kukubali katiba mpya ambayo itakata food web of its own existence. Hata kama itakubali marekebisho au katiba, it will be more or less a lost effort.

  Kwa Rais ambaye ni mwenyekiti wa CCM kuunda hiyo sijui tume, ina maana yeye ndio atakuwa mtu wa mwisho kuamua, na binding ya taarifa ya hiyo tume kisheria itakuwa still questionable. Cha msingi kama kweli kuna nia ya kuunda katiba mpya, serikali ya CCM inabidi ikubali role ya urefarii. Kwamba kwanza kuwe na jopo la katiba ambalo ni huru, ambalo litafanya kazi say miaka 2 kukusanya mawazo ya wadau wote..Kisha baadaye bunge likae kuweka sawa hayo mapendekezo na kuyapa hadhi ya kisheria, na tenure ya sasa ya CCM ikiisha basi katiba mpya ianze kazi effectively.
   
 11. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #11
  Jan 2, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,649
  Trophy Points: 280

  Itakuwa aliwaita na walipo ondoka akawapa BAHASHA za kaki!
   
 12. z

  zamlock JF-Expert Member

  #12
  Jan 2, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  january watanzania mpaka kufikia hatua ya kukupa heshima unayoitaka yataka moyo na ujaribu kuwa makini na michango yako usije haribu na ukasahaulika kwenye ulingo wa siasa
   
 13. L

  LAT JF-Expert Member

  #13
  Jan 2, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  jamani JF .... huyu JM anazungumza bila uangalifu kama baba yake...sitashangaa maana ni urithi wa fikra......hapa kuna mawili....... 1.independent commission of constitution review na 2. Presidential commision of constitution review tume kama haitakuwa independent ikapendekezwa na majina yakapendekezwa na jopo la majaji na wanasheria halafu majaji wa mahakama kuu wakachagua kwa kupiga kura na kuwaidhinisha., na mwisho wakaapa kwa jaji mkuu....... hivi hiyo tume ikiundwa na rais wataapa kwa nani...,? yes Rais....., sasa tujiulize tunataka tume ya aina gani
   
 14. Jituoriginal

  Jituoriginal JF-Expert Member

  #14
  Jan 2, 2011
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 362
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mtoto wa jambazi ni Jambazi, ni nani? January Makamba.
   
 15. S

  Selemani JF-Expert Member

  #15
  Jan 2, 2011
  Joined: Aug 26, 2006
  Messages: 871
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Cynicism ya humu ndani bana. Kwani si we wait and see who is in this tume before we become skeptical? What if Mheshimiwa Slaa will be given a substantial role in it? Subra wandugu. We wait and see the whole mchakato and provide commentaries and criticism along the way.

  Regardless, in the continent full of Gbagbos and Musevenis, it is a commendable act for CCM government to even making a tume.

  Besides katiba's role towards development is still vague. We all know Bongo's ailment comes from our awful implementation record in basically any piece of policy that the top paid consultants are crafting for us. All cadres of public servants don't give a sh!t.
   
 16. L

  LAT JF-Expert Member

  #16
  Jan 2, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  in 2010 election we waited for presidential results from NEC for about five days with no avail...... and after a long wait NEC deceived the wish and will of Tanzanians.... now who do you want to wait anymore...... there is reasonable doubt proven ..... better you and antagonists including CCM zealots and all financial oligarchies to wait for a disastrous commission .... and this is your expectations
   
 17. popiexo

  popiexo JF-Expert Member

  #17
  Jan 2, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 743
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hii ni tume nyingine isiyo huru, tume ya uchaguzi haikuwa tume huru kwasababu iliundwa na jk, na hii ya katiba itaundwa na jk uhuru utatoka wapi?
   
 18. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #18
  Jan 2, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Kaka nilijua tu utakuja..

  Tume au nani yupo ndani ya hizo tume is not an issue. Ujue katiba sio kitu kirahisirahisi kama ilani ya chama chenu au a certain policy. Katiba ni sheria mama ambapo matarajio ya watz yanawekewa uzio na kutunzwa, sio matarajio ya wanasiasa., its beyond that.

  Hivyo kwene issue nyeti kama hii, the process has to start 'somewhere', and that 'somewhere' should be a neutral point. Kwa hivi sasa inaonekana hiyo tume kwanza haitakuwa ktk utaratibu wa neutrality na maana ni tume teule ya mtu fulani, na hata ikileta taarifa yake haieleweki yatatekelezwaje kisheria. etc..etc..hivo hapa ndipo umuhimu wa serikali ku-act kama refarii ulipo na hii special case iwe ina-involve wadau wote from the very begining. Bila hivo hii katiba itakuwa ya JK sio ya watz.
   
 19. Bams

  Bams JF-Expert Member

  #19
  Jan 2, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 3,576
  Likes Received: 2,951
  Trophy Points: 280
  Huyu naye ni kam JK haelewi kile ambacho Watanzania wanataka. Watanzania hawajawahi kuwa na katiba ya kwao. Katiba iliyopo ilikuwa imeandaliwa na wakoloni kwaajili ya kututawala. TANU na hatimaye CCM waliirithi katiba hiyo na kuendelea kuifanyia marekebisho lakini nia yao haikubadilika - ilikuwa ni namna ya kututawala. Hii ni katiba ya watawala kwaajili ya kufanikisha malengo yao. Sisi tunataka kwa mara ya kwanza katika uhai wa Taifa letu tuandae katiba tutakayoikabidhi serikali, bunge na mahakama, tukiwaeleza tunavyotaka tuongozwe. Yeye anaunda kamati ya ku-review katiba ambayo siyo yetu. Huyu anaelewa tunachokitaka? Au anataka kututengenezea katiba nyingine?
  Kwa kauli ya JK ya kuunda constituion Review Committee inamaanisha hii kamati inaenda kureview katiba ya mkoloni, na baadaye TANU na CCM ili aone namna gani wanaweza kutuandalia katiba nyingine. Wananchi wanatakiwa kuanza mchakato wa kuandaa katiba chini ya tamko la bunge, na siyo serikali. Hayo mataifa ambayo huyo Mtoto January Makamba anayaongelea, yalikwishakuwa na katiba zao hapo mwanzo, sisi kama Taifa hatujawahi kuwa na katiba yetu wenyewe katika ujumla wetu bali tulilazimishwa kutawaliwa chini ya katiba ya mkoloni na baadaye CCM.
   
 20. T

  Topical JF-Expert Member

  #20
  Jan 2, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Chohote kitakachofanywa, vyovyote itavyofanywa, lazima kuna watu watasema hili lingukuwa bora kuliko lile?

  What is so "Independent" is very relative

  So go ahead mr President,

  Watakao taka kushiriki washiriki watakaogoma taifa linasonga mbele.
   
Loading...