Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,890
- 939
MHE. JANEJELLY JAMES NTATE MBUNGE WA VITI MAALUM ANAYEWAKILISHA WAFANYAKAZI NCHINI AMECHANGIA HOTUBA YA BAJETI YA WAZIRI MKUU BUNGENI
Mbunge wa Viti Maalum, Mwakilishi wa Wafanyakazi Nchini anayetokea Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Janejelly James Ntate leo tarehe 06 Aprili, 2023 amechangia Hotuba ya Bajeti ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa aliyoisoma Bungeni jana tarehe 05 Aprili, 2023.
Mhe. Janejelly Ntate amesema ajira wanazopewa wageni zirejeshwe kwa vijana wa kitanzania maana tunao watalaam wa kutosha wenye uwezo wa kuzifanya kazi wanazopewa hao wageni.
Akiongelea usajili wa vyama vya wafanyakazi, Mhe. Ntate amesema kuwa iko kisheria Kwa Shiria Na. 6 ya 2006 ya mahusiano kazini Kifungu Na 9 inawapa watumishi haki ya kufanya hivyo wapewe haki yao
Aidha, Mhe. Ntate amesema, Mabaraza ya Wafanyakazi ni nguzo ya mahusiano na kuomba wakati wa kuhitimisha walete taarifa ya mabaraza mapya yaliyoanzishwa, yaliyofanyika kwa usahihi na ambayo hayakufanyika waone wamechukua hatuna gani kwa sababu Mabalaza haya ukaguliwa na CAG
Mhe. Ntate amesema, Serikali iweke utaratibu na kuanzisha vitengo vya Mikopo kwenye Halmashauri ili kusimamia fedha za mikopo ya asilimia kumi ili kuondoa jukumu hilo kwa maafisa maendeleo ya jamii ambao hawana utalaam wa fedha lakini pia hawafanyi majukumu yao ya msingi
Mhe. Ntate alimpongeza Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha maslahi ya watumishi nakuomba yale aliyoyafanywa Wizara iyasemee ili kujenga mahusiano mazuri Kati ya watumishi na Mheshimiwa Rais.