Mhe. Jakaya Kikwete ateka Kawe, Ubungo na Mbagala | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mhe. Jakaya Kikwete ateka Kawe, Ubungo na Mbagala

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by n00b, Sep 4, 2010.

 1. n00b

  n00b JF-Expert Member

  #1
  Sep 4, 2010
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 952
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 60
  [​IMG]
  Mwenyekiti wa CCM Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na viongozi wa CCM wa Ubungo na Kinondoni katika ukumbi wa Ubungo plaza jijini Dar es Salaam jana.  [​IMG]
  Rais jakaya Kikwete akihutubia wana CCM wa jimbo la Ubungo, ukumbi wa Ubungo plaza  [​IMG]
  Kadi za CUF baada ya wenye nazo kiasi cha 80 hivi kuamua kurejea CCM


  [​IMG]
  Wanachama wapya wa CCM wakila kiapo baada ya kutoka CUF uwanja wa Zakheem, Mbagala.


  [​IMG]

  Mwana CCM akita hoja ukumbi wa Nakiete, Mbezi Beach, wakati Jakaya Kikwete alipokutana na wanachama wa jimbo la Kawe


  [​IMG]
  wana CCM wa jimbo la Kawe wakimsikiliza Jakaya Kikwete ukumbi wa Ubungo plaza.


  [​IMG]
  Umati uwanja wa Zakheem Mbagala jana kwenye mkutano wa kampeni wa Jakaya Kikwete  [​IMG]
  Uwanja wa Zakheem, Mbagala, ulitapika wana CCM wakati Jakaya Kikwete alipowahutubia.

  Picha na maelezo ni kwa mujibu wa blog ya Haki Ngowi

  Hivi hizi kadi za CUF mbona naona mpya sana? Si FEKI hizi?
   
 2. Mtoka Mbali

  Mtoka Mbali JF-Expert Member

  #2
  Sep 4, 2010
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 238
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Naanza kuwa na mashaka juu yako.
   
 3. n00b

  n00b JF-Expert Member

  #3
  Sep 4, 2010
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 952
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 60
  Mimi ndo nakuwa na mashaka na wewe, utakuwa CUF si bure. Wambie viongozi wako watwambie kama hizi nazo ni feki tujue kuwa uchakachuaji wa kadi za vyama umeanza rasmi ndani ya CCM.
   
 4. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #4
  Sep 4, 2010
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280

  Ukweli ni kwamba watu walewale wanajikusanya (wanapeana ratiba), wanavalishwa uniform za kijani/njano, wanalipwa (ndiyo kuhongwa?), halafu wanazunguka mji mzima (kujaza watu kwenye mikutan0), wanaigiza kuhama upinzani (na kurudisha kadi feki), n.k.
   
 5. R

  Reyes Senior Member

  #5
  Sep 4, 2010
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 188
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kadi za CUF zina size ya A4 au changa la macho? siamimi kama kadi zina ukubwa wa daftari
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  Sep 4, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Broda, hayo ni maigizo hayo!...
  Ni mipango iliyopangwa ikapangika,..period!
   
 7. n00b

  n00b JF-Expert Member

  #7
  Sep 4, 2010
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 952
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 60
  I suspected this. Bahati mbaya sijaanza kufuatilia baadhi ya sura kuona kama zipo kila mkutano, kuanzia leo naanza kufuatilia
   
 8. b

  bobishimkali Member

  #8
  Sep 4, 2010
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM haiwezi kufanya mchezo wa kitoto kama unavyodhani.Ni ukweli mtupu kwamba wanachama wengi wa vyama vya upinzani wanarudisha kadi na kujiunga na CCM.Hii ni kutokana na vyama vya upinzani kuwa na migogoro mingi,halikadhalika hakuna matumaini yeyote ya vyama hivyo kushinda kiti cha urais katika uchaguzi wa 2010.
   
 9. b

  bobishimkali Member

  #9
  Sep 4, 2010
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Hayo siyo maigizo,ni ukweli mtupu .Wanachama wa CUF wamemchoka LIPUMBA kwa kuwa ni mbinafsi, anataka kugombea kiti cha urais pekeyake tu,hataki mtu mwingine agombee pamoja na ukweli kwamba amekuwa akishindwa katika chaguzi zote zilizopita .Safari hii atashindwa vibaya zaidi na wanachama wa CUF wataendelea kukihama chama hicho
   
 10. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #10
  Sep 4, 2010
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,425
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 160

  Sioni hilo tu, ila nashangaa hao wanachama wapya ni kina mama tu, waone kwenye picha, halafu wanaelekea kutokea kwenye imani moja! Ukiona hivi unapata kigugumizi kama kweli ni kwa hiari yao au wameshurutishwa. Pili, nadhani kichwa cha habari kimekuwa 'exaggerated', kufanya mkutano kwenye ukumbi, sidhani kama kweli ni sawa na anayefanya kwenye uwanja kama Jangwani pale. Naamini aliposti hii ana ajenda zaidi ya anachotaka kusema
   
 11. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #11
  Sep 4, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  Bora aendelee kufanya kampeni huku amekaa....
   
 12. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #12
  Sep 4, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,485
  Likes Received: 19,881
  Trophy Points: 280
  Masikini weeee, waone wenzetu ,wamevalishwa kofia na t shirt, basi watauza haki yao, then badae wataanza kulalamika , mara foleni, mara hatuna ambulance, mara jamaa anasafiri sana. huku akiwa keshasahau t sirt na kofia aliyovalishwa. Jamani tutabadilika kweli kirahisi?.natamanni siku moja niamke asubuhi nikute wananchi wote wamefumbuka macho.
   
 13. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #13
  Sep 4, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mikutano ya CCM yote ni wizi mtupu, daladala karibu zote jana zilikuwa zimekodishwa na ccm kwa ajiri ya kuchukua watu wa kuhudhuria. Hii ni tofauti sana na CUF na CHADEMA ambapo watu wanajitokeza kwa hiari bila kulipiwa gharama za usafiri au kupewa posho yoyote na vyama vyao
   
 14. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #14
  Sep 4, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,618
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Weraaaaaaaaaaaaaaa weraaaaaaaaaaaaaaaaaaa
   
 15. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #15
  Sep 4, 2010
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Ama kweli nyani hauoni kundule! Kuna chama chenye migogoro sasa hivi kushinda CCM? Chama gani kilichokimbiwa na makada wake maarifu kushinda CCM?
   
 16. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #16
  Sep 4, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,618
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Halafu wakaenda wapi??????????Cha ajabu wakitoka CCM kwenda upinzani wanapewa ishu muhimu.Wakati ndani ya Chama kikubwa kama CCM wamekuwa proved kwamba hawafai.
   
 17. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #17
  Sep 4, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,923
  Likes Received: 631
  Trophy Points: 280

  Shangilia Tu. Ila kaka kuna wanaoishi haya maisha, Najua huamini kama hii ni Tanzania, Lakini Hii Ndio Tanzania ya Kikwete Kule Njombe. Watoto wanaenda kubeba Mahindi,


  Mungu tusaidie tuepukane na utawala huu Wa ccm.


  [​IMG] Moja kati ya ajira mbaya kwa watoto mkoani Iringa ,japo ni sehemu ya malezi ila mzigo huu ni mzito sana hii ni adhabu sio malezi tena
  [​IMG] Hata bila punda lazima mkokoteni huu utafika tu hakuna ujanja

  [​IMG] Watoto wakazi wa Wangama wilaya ya Njombe mkoani Iringa ambao majina yao hayakuweza kupatikana mara moja wakikokota mkokoteni wa kuvutwa na wanyama ,wakielekea kubeba mahindi shambani kama walivyokutwa leo majira ya jioni,kwa kawaida mkokoteni huu hukokotwa na wanyama kazi sio binadamu kama hivi
   
 18. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #18
  Sep 4, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Hii kali, siku tatu tu ushaanza kukosa imani na watu.... Ungekaa mwaka je?
  hili ni jukwaa huru na si kwa chama fulani pekee as long as hatupati malaria sugu
   
 19. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #19
  Sep 4, 2010
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Lakini nafikiri Kikwete ndiye rais anayeongoza kwa kudanganywa na watendaji wake, kuanzia serikalini mpaka kichama!
   
 20. M

  Masauni JF-Expert Member

  #20
  Sep 4, 2010
  Joined: Aug 15, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe kibonde kweli ,hujui kuwa mpinga ufisadi kwa CCM ni mtu asiyefaa, bali anayekumbatia ufisadi ndio kiongozi mzuri anayekubarika. mifano hii hapa lowasa fisadi papa approved, chenge fisadi approved, kikwete fisadi approved,RA FISADI approved na nk.
   
Loading...