Baada ya kushambuliwa na Kundi la watu wasiojulikana jana usiku, Mheshimiwa NYNESS KIWIA amehamishwa kutoka BUGANDO na kupelekwa MUHIMBILI kwa matibabu zaidi.
Mheshimiwa alivamiwa na watu waliokuwa na mapanga, marungu, na silaha zinginezo, wakitokea ndani ya magari mawili na kumzingira Mbunge alipokuwa akirejea kutoka katika harakati za uchaguzi mdogo wa Kata ya KIRUMBA Mwanza.
Hata hivyo Mhe. aliwasiliana na Mhe. WENJE na MACHEMLI,ili wafike kumsaidia, baada ya kujaribu kuwasiliana kwa muda kuwaita Polisi bila mafanikio.
Mhe. Kiwia amepata majeraha makubwa kichwani na mgongoni, pamoja na michubuko iliyotapakaa mgongoni na sehemu zingine mwilini, huku jicho moja likiwa na uoni hafifu.
SOURCE; TBC 1 News!