Mhe. Freeman Mbowe, Salva Rweyemamu, Waunguruma BBC Kuhusu Mkutano wa JK na CHADEMA!

Mhe. Freeman Mbowe, Salva Rweyemamu, Waunguruma BBC Kuhusu Mkutanoo wa JK na Chadema!

Wameunguruma katika kipindi cha Dira ya Dunia, kinachoendela sasa!

Walikuwa wakihojiwa na Mtangazaji Aboubakar Mfamao.

Mhe. Mbowe alieleza lengo lao la kuzungumza na JK. Salva alieleza walivyokubaliwa.

BBC ikauliza Kikao ni lini?. Salva akajibu watafanya mawasiliano ya kiofisi kupanga lini wote watakuwa na nafasi.

Mhe. Mbowe amesema Chadema wako tayari wakati wowote, hivyo determinant ni JK tuu.

Angalizo!. JK yuko kwenye kikao cha NEC Dodoma kwa siku mbili, hivyo huo mkutano lazima uwe Jumatatu au Jumanne kwa sababu JK atausani ule muswada siku ya Jumatano ili Alhamisi tarehe 1 Desemba, sheria hiyo ndio inaanza kutumika!.
Kitendo cha JK kukubali kukutana na Chadema, ni dalili njema, ila kumbukumbu yangu ya arrogance ya rais wetu, wakati ile hotuba yake ya 'Mbayuwayu' naombeni niwape maandalizi ya kisaokolojia ya wale wote wenye Great Expectitions na JK kuwa hatausaini, plese just "Hope for the best, but prepare for the worst!" kwa sababu, ATAUSAINI!

It sounds kama vile umetumwa kama Yohana Mbatizaji "kutengeneza njia!"
 
Jk atajuta sana kukubari ombi la chadema wafuasi wa chama hiki hawawezi wanahitaji siasa za jino kwa jino kama unabisha fuatilia maoni yao hapa JF
 
siasa za wanachadema ni ngumu wamepewa fursa wanatukana kutwa. kama huyo Jk ni arrogant mnakweda kutafuta nini kwa mtu ambaye mnasema uwezo wake ni mdogo?
 
huko dodoma nako naona hao nec wamempa sumu ccm...full kumpotosha..wanasema kama akikutana na chadema basi akutane na vyama vingine vya siasa na si chadema peke yake
Kama maneno haya ni ya kweli basi CCM wanacheza Politics tupu..Kwani wanafikiri Chadema wanakwenda Ikulu kufanya nini?
 
Salva kasema Ikulu na Kamati ya CHADEMA itabidi wapange tarehe ambayo wajumbe wa pande zote mbili watakuwepo.

Jibu la Mbowe ni kuwa wao walipendekeza katika barua yao iwe kabla ya tar 01.12.2011 kwa kuwa mswada unataja kuwa sheria hiyo itaanza kutumika 01.12.11. Lengo la CHADEMA wakutane na Rais kabla hajasaini muswada huo kuwa sheria.

My take: Ikulu wanaanza sarakasi.

ukifuatilia hoja za wanachadema hapa JF sioni kama kuna sababu ya Jk kuwasikiliza Jk anapoteza muda
 
kwa jinsi mjadala wa kumuona Jk unavyopuuzwa sambamba na kejeri sioni sababu ya chadema kuomba kukutana naye
 
NEC mmenena hawa chadema wanatoa masharti hata kabla hawajafika Ikulu hakuna kwenda peke yao Ikulu waambatane na vyama vingine vya upinzani
 
JK kuwa makini na hawa chadema ukiongea nao peke yao pale Ikulu bila wenzao wa upande wa upinzani watatoka na maneno mengi ya uongo Ikulu bora kupata mashahidi kutoka upinzani. maneno yamekuwa mengi hata kabla hujawafungulia mlango wa IKulu watakugeuka hawa na kusema ambayo hukusema
 
Jk atajuta sana kukubari ombi la chadema wafuasi wa chama hiki hawawezi wanahitaji siasa za jino kwa jino kama unabisha fuatilia maoni yao hapa JF
Acha mawazo mgando...wana-chadema wangapi wanao mshambulia huyu mpenda suti wako, unajua je kuwa huyu chadema hutu NCCR -Mageuzi, huyu CCM-B,UDP......
 
arrogance ni ya kwenu mliotoka bungeni wakati Jk akihutubia bunge mwaka jana leo mnaomba kuonana naye bila chembe ya aibu
Ni kwasababu ya umbumbumbu wako ndo maana huelewi sababu ya CDM kutoka bungeni.
 
ndio maana chadema hamkulaani tamko la cameron yule mshirika wenu shoga wa uingereza. sio ajabu umependa sauti laini ya salva na kumuona kama mwali.
Kwani cameron aliongea kama kiongozi wa chama au serikali? Chadema sio chama cha watu wenye mtindio wa ubongo kama nape, Membe alishalaani kwa niaba ya watanzania kama ambavyo cameron aliongea kwa niaba ya waingereza. Sasa mropokaji wa magamba nape alikuwa analaani kama nani? au hajui kuwa membe alituwakilisha wote
 
Jk atajuta sana kukubari ombi la chadema wafuasi wa chama hiki hawawezi wanahitaji siasa za jino kwa jino kama unabisha fuatilia maoni yao hapa JF

Mkuu mbona unatupakazia siasa za jino kwa jino siyo za cdm.
 
Back
Top Bottom