Mhe. Freeman Mbowe, Salva Rweyemamu, Waunguruma BBC Kuhusu Mkutano wa JK na CHADEMA!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,467
113,557
Mhe. Freeman Mbowe, Salva Rweyemamu, Waunguruma BBC Kuhusu Mkutanoo wa JK na Chadema!

Wameunguruma katika kipindi cha Dira ya Dunia, kinachoendela sasa!

Walikuwa wakihojiwa na Mtangazaji Aboubakar Mfamao.

Mhe. Mbowe alieleza lengo lao la kuzungumza na JK. Salva alieleza walivyokubaliwa.

BBC ikauliza Kikao ni lini?. Salva akajibu watafanya mawasiliano ya kiofisi kupanga lini wote watakuwa na nafasi.

Mhe. Mbowe amesema Chadema wako tayari wakati wowote, hivyo determinant ni JK tuu.

Angalizo!. JK yuko kwenye kikao cha NEC Dodoma kwa siku mbili, hivyo huo mkutano lazima uwe Jumatatu au Jumanne kwa sababu JK atausani ule muswada siku ya Jumatano ili Alhamisi tarehe 1 Desemba, sheria hiyo ndio inatakiwa iwe inaanza kutumika!.

Kitendo cha JK kukubali kukutana na Chadema, ni dalili njema, ila kwa kumbukumbu yangu, JK ni very strict na (arrogant) kwenye issue za kuhatarisha usalama wa taifa letu, kama nilivyo shuhudia wakati wa ile hotuba yake ya 'Mbayuwayu'. Naombeni niwape maandalizi ya kisaokolojia kwa wale wote wenye Great Expectetions na JK kuwa hatausaini, please just "Hope for the best, but be prepare for the worst!" kwa sababu, ATAUSAINI!

Kusikiliza fuata hii link http://www.bbc.co.uk/swahili/medianu...dunia_wed.shtm

Pasco.
 
Mkuu P tafadhali tujuze zaidi ambao hatujapata fursa ya kulisten BBC namna walivounguruma hasa Mbowe maana najua Salva cant!
 
Salva kasema Ikulu na Kamati ya CHADEMA itabidi wapange tarehe ambayo wajumbe wa pande zote mbili watakuwepo.

Jibu la Mbowe ni kuwa wao walipendekeza katika barua yao iwe kabla ya tar 01.12.2011 kwa kuwa mswada unataja kuwa sheria hiyo itaanza kutumika 01.12.11. Lengo la CHADEMA wakutane na Rais kabla hajasaini muswada huo kuwa sheria.

My take: Ikulu wanaanza sarakasi.
 
BBC ikauliza Kikao ni lini?. Salva akajibu watafanya mawasiliano ya kiofisi kupanga lini wote watakuwa na nafasi.

Mhe. Mbowe amesema Chadema wako tayari wakati wowote, hivyo determinant ni JK tuu.
Kama nimemsikia Mbowe vema, ametaka kikao hicho kifanyike kabla JK hajasaini muswada huo. Ametaka kikao kiwe kabla ya december 1 siku ambao, kwa mujibu wake, ndiyo sheria inatakiwa kuanza kufanya kazi
 
Pasco,

..hata mimi naona JK amefungwa na kauli alizotoa kwenye hotuba yake.

..tatizo ni kwamba alitumia muda mwingi sana kuwaponda wote waliokuwa na mtizamo tofauti na wakwake.

..JK alitumia neno WAPOTOSHAJI na UPOTOSHAJI mara nyingi mno.

..sasa nashangaa kwanini JK amekubali kukutana na watu ambao tayari alishawa-label kuwa ni WAPOTOSHAJI??
 
kila ki2 kinakwenda kwa mipango na ratiba hy ni ikulu bwana,, maadam wamekubaliana kukutana shaka iko wapi jamani? Kweli uhuru bila nidhamu ni fujo. Tusiwashurutishe hawa viongozi maadam tumekubali kuwapa ridhaa ya kuonana na mkuu watatuwakilisha vyema. Au kale ka imani bd hakatoshi?
 
Mhe. Freeman Mbowe, Salva Rweyemamu, Waunguruma BBC Kuhusu Mkutanoo wa JK na Chadema!

Wameunguruma katika kipindi cha Dira ya Dunia, kinachoendela sasa!

Walikuwa wakihojiwa na Mtangazaji Aboubakar Mfamao.

Mhe. Mbowe alieleza lengo lao la kuzungumza na JK. Salva alieleza walivyokubaliwa.

BBC ikauliza Kikao ni lini?. Salva akajibu watafanya mawasiliano ya kiofisi kupanga lini wote watakuwa na nafasi.

Mhe. Mbowe amesema Chadema wako tayari wakati wowote, hivyo determinant ni JK tuu.

Angalizo!. JK yuko kwenye kikao cha NEC Dodoma kwa siku mbili, hivyo huo mkutano lazima uwe Jumatatu au Jumanne kwa sababu JK atausani ule muswada siku ya Jumatano ili Alhamisi tarehe 1 Desemba, sheria hiyo ndio inaanza kutumika!.
Kitendo cha JK kukubali kukutana na Chadema, ni dalili njema, ila kumbukumbu yangu ya arrogance ya rais wetu, wakati ile hotuba yake ya 'Mbayuwayu' naombeni niwape maandalizi ya kisaokolojia ya wale wote wenye Great Expectitions na JK kuwa hatausaini, plese just "Hope for the best, but prepare for the worst!" kwa sababu, ATAUSAINI!
Mkuu yawezekana kweli atausaini lakini sidhani kama JK ni mjinga kiasi hicho.. Kwanza kukubali tu kukutana na Chadema ni jambo ambalo hakuna mtu alikusudia. Katika moja ya Tweet zake nilizowahi kuzisoma JK anasema:-
"Best and wise decisions are to be made in major turning points; otherwise you might create a future crisis..."

This is heavy statement!...Na maneno haya nimewaweka ktk nukuu ya favorites zangu...Na hakuna mahala pazuri ambapo JK anaweza jizolea sifa ni hapa. Hii ndio legacy yake, misifa wonna make history! na sidhani kama atakuja ipoteza nafasi kama hii kuandika Katiba ambayo within next 5 yrs itakufa...
Hivyo naweka tumaini siwezi kulipoteza hadi dakika ya mwisho japokuwa simwamini JK... well, simuamini mwanasiasa yeyote!
 
arrogance unayo wewe Jk hakuwaita ikulu mumeomba wenyewe kwenda ikulu kama mnatoa masharti bora mwendelee na maandamano
 
unafikiri mnakweda kwa Jk kunywa na kula chakula. hoja zikiwa dhaifu Jk atazitupilia mbali na kusonga mbele kusaini muswada kuwa sheria
 
huko dodoma nako naona hao nec wamempa sumu ccm...full kumpotosha..wanasema kama akikutana na chadema basi akutane na vyama vingine vya siasa na si chadema peke yake
 
arrogance ni ya kwenu mliotoka bungeni wakati Jk akihutubia bunge mwaka jana leo mnaomba kuonana naye bila chembe ya aibu
 
aisee!
nakumbuka ile thread ya mwanakijiji ya kitendawili, hiki kweli nikitendawili. ngoja tusubiri.
 
Namshangaa Jk kwa nini kawakubalia kwenda huko Ikulu nyinyi watata sana alitakiwa tu kusonga mbele. kawakubalia sasa mna maneno mengi hata kabla hamjaonana naye
 
Back
Top Bottom