Mhe. Freeman Mbowe: Mimi na viongozi wenzangu tunafuatilia kwa karibu yote yanayojiri hususan kamata kamata ya timu zetu katika operation

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,261
2,000
Waheshimiwa Viongozi, Wabunge, Madiwani, wanachama na wapenzi wa Chama chetu Chadema!!

Salaam sana!!

Naamini wengi wetu tumemaliza salama sherehe za Eid na sasa tuko tayari kuendelea na wajibu wetu kwa Chama, Taifa na Jamii yote ya wapigania haki na ustawi.

Wenzetu kadhaa hawakufanikiwa kusheherekea sikukuu ya Eid. Wako waliokumbwa na umauti katikati ya operation, wapo wagonjwa, wapo mahabusu wa kisiasa na wapo waliokuwa kazini kipindi chote cha sikukuu! Tuendelee kuziombea pumziko la Milele waliotutangulia!

Wengine wote naomba kuwatia moyo! Kutweza kwao, kuumia kwao, na hata jasho lao halitapotea bure!

Mimi na viongozi wenzangu tunafuatilia kwa karibu yote yanayojiri hususan kamata kamata ya timu zetu katika operation, zaidi katika Mikoa ya Singida na Morogoro!

Aidha, tunaiona hamaki yenye hofu na pengine woga toka miongoni mwetu. Tunalalamika! Wengine tukitamani kupaza sauti kupitia Press Conference!

Naamini nia ni njema lakini Press conference haisaidii katika haya! Katika mazingira yaliyotuzunguka bado tunapiga kelele kiongozi au Mwana Chadema kuwekwa mahabusu!??

Siioni hasira ya Wabunge kufanyiwa kila aina ya unyanyasaji ndani na nje ya Bunge, jambo lililo baya kuliko hata kulala mahabusu!!

Hiki ni kipindi ambacho laiti kila mmoja wetu angejitoa kwa dhati, bila hofu wala ajizi na kuona kulazwa ndani kusiko halali kama hatua muhimu na chachu ya kutuimarisha na kutukomaza!!

Yawezekana wengi wetu bado hatujitambui kuwa tuko katikati ya vita kali. Vita isiyoheshimu Katiba, Sheria wala utu! Vita isiyo na busara tena isiyo na huruma!!

Huu ni wakati wa kujibu kwa action ndani ya field na siyo kwa maneno na kulalamika!! Adui yetu yuko hoi kuliko sisi lakini wengi wetu bado hatujitambui!!

Wakati huu, operation ya Chama inaendelea kwa wakati mmoja katika majimbo 82 ya uchaguzi. Hii ni operation kubwa kuliko zote zilizowahi kufanywa na Chama hiki! Maelfu ya wapiganaji, wanawake kwa wanaume, wake za watu kwa waume za watu wametapakaa nchi nzima wakiumia usiku na mchana kuifanya kesho yetu kuwa bora zaidi ya leo! Hawa hawana mshahara, hawana posho, hawana magari, wengi wao hawana uhakika wa mlo wao wa siku wala malazi yao kiza kikitinga!!

Watesi wetu wanajua uzito wa kinachofanyika ndani mwetu kuliko sisi wenyewe!!

Wenzetu wana hofu kubwa ya kupoteza dola na wako tayari kuilinda kwa gharama yeyote halali na haramu kuliko sisi tulivyo tayari kuipigania na kuipata hiyo dola!

Tuna hasira ya kutukana na kunung’unika mitandaoni kuliko tulivyo tayari kwenda field kuongeza nguvu za mapambano, kila mmoja wetu kwa eneo lake!!

Mapambano haya yataendelea. Ni vyema na itapendeza tukiwa pamoja. Mwenye roho ya hofu na apishe wenye utayari! Hiki ni kipindi cha kutiana ujasiri kwa maneno na vitendo!

Niwatakie wote kujitambua!

Freeman Aikaeli Mbowe
Mkt T, KUB & MP Hai
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
77,448

Ushujaa wa Mbowe umetukuka .
 
johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
35,134

Huyu Mbowe anajua masharti ya dhamana yake kweli?!!

Uchochezi unaweza kumrudisha segerea mlio karibu naye mkumbusheni!
 
Mkwaruu

JF-Expert Member
Mar 13, 2017
2,943
2,000
Hongereni chadema kwa kutumia hoja kujenga chama haraka siku zote ni udhubutu tuu
 
Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
36,259
2,000
Ukisoma katikati ya mistari,utajua Mbowe na CHADEMA wanakusudia kufanya nini siku zijazo endapo hali hii itaendelea.
Na Nina mashaka sana kuwa baada ya 7 septemba mwaka huu hali itakuwa mbaya sana kwa hawa watesi wa watu watakapo ona muujiza wa sixteen bullets ukitembea na kuwaondoa hofu wale waliokuwa na woga na kukabiliana nao.
 
Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
39,836
2,000
Na Nina mashaka sana kuwa baada ya 7 septemba mwaka huu hali itakuwa mbaya sana kwa hawa watesi wa watu watakapo ona muujiza wa sixteen bullets ukitembea na kuwaondoa hofu wale waliokuwa na woga na kukabiliana nao.
Tuombe uzima tu mkuu.
 
senzighe

JF-Expert Member
Jan 1, 2012
1,557
2,000
Waheshimiwa Viongozi, Wabunge, Madiwani, wanachama na wapenzi wa Chama chetu Chadema!!

Salaam sana!!

Naamini wengi wetu tumemaliza salama sherehe za Eid na sasa tuko tayari kuendelea na wajibu wetu kwa Chama, Taifa na Jamii yote ya wapigania haki na ustawi.

Wenzetu kadhaa hawakufanikiwa kusheherekea sikukuu ya Eid. Wako waliokumbwa na umauti katikati ya operation, wapo wagonjwa, wapo mahabusu wa kisiasa na wapo waliokuwa kazini kipindi chote cha sikukuu! Tuendelee kuziombea pumziko la Milele waliotutangulia!

Wengine wote naomba kuwatia moyo! Kutweza kwao, kuumia kwao, na hata jasho lao halitapotea bure!

Mimi na viongozi wenzangu tunafuatilia kwa karibu yote yanayojiri hususan kamata kamata ya timu zetu katika operation, zaidi katika Mikoa ya Singida na Morogoro!

Aidha, tunaiona hamaki yenye hofu na pengine woga toka miongoni mwetu. Tunalalamika! Wengine tukitamani kupaza sauti kupitia Press Conference!

Naamini nia ni njema lakini Press conference haisaidii katika haya! Katika mazingira yaliyotuzunguka bado tunapiga kelele kiongozi au Mwana Chadema kuwekwa mahabusu!??

Siioni hasira ya Wabunge kufanyiwa kila aina ya unyanyasaji ndani na nje ya Bunge, jambo lililo baya kuliko hata kulala mahabusu!!

Hiki ni kipindi ambacho laiti kila mmoja wetu angejitoa kwa dhati, bila hofu wala ajizi na kuona kulazwa ndani kusiko halali kama hatua muhimu na chachu ya kutuimarisha na kutukomaza!!

Yawezekana wengi wetu bado hatujitambui kuwa tuko katikati ya vita kali. Vita isiyoheshimu Katiba, Sheria wala utu! Vita isiyo na busara tena isiyo na huruma!!

Huu ni wakati wa kujibu kwa action ndani ya field na siyo kwa maneno na kulalamika!! Adui yetu yuko hoi kuliko sisi lakini wengi wetu bado hatujitambui!!

Wakati huu, operation ya Chama inaendelea kwa wakati mmoja katika majimbo 82 ya uchaguzi. Hii ni operation kubwa kuliko zote zilizowahi kufanywa na Chama hiki! Maelfu ya wapiganaji, wanawake kwa wanaume, wake za watu kwa waume za watu wametapakaa nchi nzima wakiumia usiku na mchana kuifanya kesho yetu kuwa bora zaidi ya leo! Hawa hawana mshahara, hawana posho, hawana magari, wengi wao hawana uhakika wa mlo wao wa siku wala malazi yao kiza kikitinga!!

Watesi wetu wanajua uzito wa kinachofanyika ndani mwetu kuliko sisi wenyewe!!

Wenzetu wana hofu kubwa ya kupoteza dola na wako tayari kuilinda kwa gharama yeyote halali na haramu kuliko sisi tulivyo tayari kuipigania na kuipata hiyo dola!

Tuna hasira ya kutukana na kunung’unika mitandaoni kuliko tulivyo tayari kwenda field kuongeza nguvu za mapambano, kila mmoja wetu kwa eneo lake!!

Mapambano haya yataendelea. Ni vyema na itapendeza tukiwa pamoja. Mwenye roho ya hofu na apishe wenye utayari! Hiki ni kipindi cha kutiana ujasiri kwa maneno na vitendo!

Niwatakie wote kujitambua!

Freeman Aikaeli Mbowe
Mkt T, KUB & MP Hai
Yaani wewe Mbowe ni kama mlevi wa unga ambaye akishabwiya anaiona dola hii hapa mkononi.Kawadanganye watoto wa vidudu kwamba waliopo madarakani wana hofu ya kupoteza dola maana hata ukiwaeleza wa shule ya msingi watakuzomea tu
 
social_science

JF-Expert Member
Dec 19, 2015
1,111
2,000
Huyu bwana ni mchumia tumbo alimchukua mzee wa mamvi akamwaibisha.Tz hakuna siasa za upinzani wote wasaka fursa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom