Mhe. Freeman Mbowe: Ijumaa Kuu njema kwa Wakristo na wananchi wote kwa ujumla

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
IJUMAA KUU NJEMA kwa Wakristo na wananchi wote kwa ujumla. Mwaka jana 2018, Ijumaa Kuu kama leo nilikuwa magereza ya Segerea na viongozi wenzangu 9 wa Chama chetu cha Chadema, baada ya kukosa dhamana katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es salaam. Ujumbe wangu wa Pasaka mwaka jana ulikuwa ni " Udikteta Tanzania sio wa kufikirika tena ni kweli". Leo nikiwa uraiani miezi 12 baadae Watanzania wote tunashuhudia ikisainiwa sheria ya vyama vya siasa Na. 1/2019, ambayo lengo lake ni kuminya demokrasia na vyama vya siasa nchini.

Tutumie siku hii ya Ijumaa Kuu na Pasaka yote kwa ujumla kuliombea Taifa na viongozi tuliowapa dhamana ya kutuongoza watawale kwa hekima na busara, katiba na katiba, wasijawe na viburi , kwamba maneno yao ndio sheria hakuna wa kuyapinga popote bila kufuata sheria.

Muda sio mrefu ndugu zetu Waislam Wataanza mwezi mtukufu wa Ramadhani, nao watumie mwezi huo kuliombea Taifa na viongozi wetu, Mungu awajaze hekima na busara katika kutawala nchi, wasikilize ushauri na maoni mbalimbali ya watu, Kwa mustakabali mpana wa Taifa letu pendwa la Tanzania.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKI DUNIA.

IJUMAA KUU NJEMA.
 
Ilianza Arab spring. . Sasa inakuja "myeusi" spring siku si nyingi
 
Asante Usain Bolt wa ufipa
IMG_20190418_080314.jpeg
 
Back
Top Bottom