Mhe. Ezekiel Maige: "Mara nyingi watenda mema hufanyiwa hiyana" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mhe. Ezekiel Maige: "Mara nyingi watenda mema hufanyiwa hiyana"

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ngoshwe, Jun 3, 2012.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Jun 3, 2012
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Hii ndio Kauli ya Mhe. Ezekiel Maige katika Ukurasa wake wa Face Book:

  [​IMG]
  ".......Ndugu zangu na rafiki zangu. Kwanza niwape pole kwa mshituko mlioupata kwa haya yaliyojitokeza. Naomba msisikitike sana. Kila jambo alilopanga Mola hutokea kadiri ya mapenzi yake. Route ya maisha ya mwanadamu hupangwa na Mola mara tu anapompulizia pumzi ya uhai. Hili lilipangwa hata kabla sijatokea duniani miaka 42 iliyopita!

  Mungu hakushindwa kumwokoa mwanawe Yesu asisulubiwe, tena kwa kuonewa! Hasha, tungeupataje ukombozi bila hilo kutokea? Wakati mwingine Mungu hutoa nafasi kwa mambomagumu kuwafika waja wake, si kwamba hawapendi,bali ili unabii utimie. Ilifika wakati hata Yesu akaona kama Mungu kamuacha! Hasa sisi kwa hili tunaweza kudhani Mungu katuacha! Hasha, ni njia ya kuufikia ukombozi wa kweli.

  Pili, kwa kifupi sana, niwafahamishe kuwa, yaliyotokea ni ushahidi kwamba maliasili ni ngumu. Kukabiliala na wabaya ni kazi ngumu. Wapo waliojipanga ukiwavamia ovyoovyo unaondoka wewe. Ndivyo ilivyotokea.

  Niwahakikishie, wazalendo wamepoteza mpambanaji. Nimepambana na wahalifu angani, majini, porini, mijini na vijijini ndani na nje ya nchi. Nilitumia kila aina ya uwezo wangu kulizawadia taifa langu utumishi uliotukuka. Sikubakisha chembe ya energy.

  Waziri gani aliyesimamia sheria na kuwapa vitalu watanzania maskini wenye sifa na kuwaacha wazungu kama sheria ilivyoelekeza?

  Waziri gani aliyewafikisha mahakamni watorosha twiga akina Kamrani na wenzake? Watu wametumia records za matukio ya 2009/10 kuficha matendo na maamuzi ya kishujaa ya maige ya 2011. Yawezekana hawakutaka nipate sifa, lakini ipo siku nitaipata. Tena si siku nyingi. Niliwaomba wenzangu wamwogope Mungu. Bado nasisisitza hivyo, si Mungu wangu kama ilivyodhaniwa, bali Mungu wetu wa haki.

  Waziri gani aliyefunga biashara ya wanyamahai?

  Waziri gani aliyeonyesha mfano wa kuchukua hatua kwa watumishi pale alipoona hawatendi sawa? Maige hakusita kuchukua hatua.

  Maamuzi haya ni magumu na yamegusa watu wenye nguvu na ushawishi mkubwa. Nilitegemea vita hii, na ninaamini tutashinda. Nilisema Bungeni, watanzania wapenda haki wanisikilize kwa makini. Muda haukuruhusu, ila nitarudi Bungeni na nitasema.

  Imesemwa issue ya nyumba. Nimefafanua na kutoa vielelezo. Kila mbunge aliyetaka amekopeshwa shs 290m, wengine wameanzisha biashara na wengine wamenununua magari na wengine majumba. Wapo walioficha, na tupo tuliojiweka wazi! Mkopo wangu huo umekuwa my contribution na balance kulipwa na benki na nyumba kuimortgage. Nimetoa nyaraka zote kwa wanahabari na vyombo vyote husika. Nimesema mwenye mashaka aende kwa Msajili wa hati wizara ya ardhi, au kwa kamishna wa maadili, au CRDB Azikiwe na Dodoma nilikokopa au amtafute muuzaji. Kote huko utapata rekodi ya bei na mode of payment. Wapo wahuni, kwa maslahi ya kisiasa na chuki binafsi wametangaza bei tofauti na niliyonunulia. Manasheria wangu anashughulikia hilo.

  Niwahakikishie, vita nimepigana, imani na dhamana nimeilinda, muda wa kutuzwa na mwenye kumbukumbu sahihi, Mungu utafika. Naamini nimejiwekea akiba isyooza Mbiguni.

  Yapo mengi yasiyo sahihi yaliyosemwa. Nitakuwa nafafanua kila nipatapo fursa na muda utazidi kutufunua. Kwa kifupi, kwa suala la vitalu, hakuna kampuni hata moja iliyopewa kitalu cha uwindaji bila kuomba, kukaguliwa na kamati ya ushauri na hatimaye kupewa alama. Kampuni zisizokuwa na sifa ni zile zilizopata chini ya alama 50. Na kwa kampuni zilizokuwa kwenye biashara, passmark ni alama 40 kwa mujibu wa kanuni ya 16(5) ya kanuni za uwindaji wa kitalii za mwaka 2010. Hakuna kampuni iliyopata chini ya alama 50 iliyopata kitalu. Hakuna kampuni ya kizalendo iliyopendekezwa na kamati ya ushauri ambayo haikupewa kitalu.

  Kwa upande wa report ya CAG, haikunigusa binafsi kwani ilikuwa inaishia juni 2010 wakati mimi ilishika dhamana Novemba 2010.

  Ka upande wa biasharaya wanyamahai, hakuna wanyama waliosafirishwa kinyume cha sheria wakati wangu (2011), na matukio ya utoroshaji tulipoyabaini, tulifungua mashitaka kwa watuhumiwa nakufnug biashara hiyo.

  Naanza kazi ya kuwawakilisha wananchi wa Msalala. Nitawawakilisha kwa mujibu wa katiba na ahadi zangu kwao hadi 2015 watakapopata fursa ya kuamua vinginevyo.

  Mara nyingi watenda mema hufanyiwa hiyana. Ka wakristo, naomba msome Mwanzo 4:1-15.

  Wasalaam..... "


  https://www.facebook.com/permalink.php?story_fbid=292151247542210&id=100002420106482
   
 2. asrams

  asrams JF-Expert Member

  #2
  Jun 3, 2012
  Joined: Sep 4, 2011
  Messages: 4,003
  Likes Received: 1,372
  Trophy Points: 280
  Kazi ipo. Je asingepokonywa tonge lake angeyasema hayo yoote??!!

  Anyway pole zako.


  Sent from my NOKIA 3310 using Tapatalk HD
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Jun 3, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,269
  Likes Received: 22,029
  Trophy Points: 280
  Watu wa CCM bwana, wakipigwa chini ni big problem. Je mnayakumbuka mauzauza ya L. Masha alipoukosa ubunge?
   
 4. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #4
  Jun 3, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Tunaifaham hiyo unairudia
   
 5. S

  Sheshejr JF-Expert Member

  #5
  Jun 3, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 435
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Maige kawa maarufu JF.
   
 6. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #6
  Jun 3, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Too much mungu is not good for your health and could prove blinding.
   
 7. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #7
  Jun 3, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Maige anatafuta pa kufia, hana jipya.
   
 8. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #8
  Jun 3, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160
  Mzalendo ni matendo si maneno..........bunge laja tunasubiri kama alivyoahidi
   
 9. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #9
  Jun 3, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,590
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Maige it is enough; achia watu wakutetee na si wewe mwenyewe. Hao unaowapa pole, nafikiri wewe unahitaji hizo pole kuliko wao!

  Let it go!
   
 10. O

  Ogah JF-Expert Member

  #10
  Jun 3, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145


  Kwa hiyo uliwavamia "ovyoovyo"...........wewe Maige ni hovyo kabisa............​
   
 11. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #11
  Jun 3, 2012
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Hakujipanga..
   
 12. andishile

  andishile JF-Expert Member

  #12
  Jun 4, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 1,430
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  ni kweli kuwa mara nyingi mtenda mema hufanyiwa hiyana,lakini kwako hapana!sasa kinachokufanya upite majukwaani kuiponda ccm,upite jukwaani kuwaponda viongozi wa sekretarieti ya ccm ni nini? wakati ulipokuwa waziri hukufanya hivyo?au kama ulijua ccm haifai,kilichokufanya ukubali kuitumika kama waziri wa serikali yake ni nini?haifai baada ya wewe kutolewa uwaziri?umejishushia sana hadhi!piga ua garagaza,wee ni mbunge wa ccm,ungekaa kimya mngekosoana ktk vikao vya chama!
   
 13. Mbelwa Germano

  Mbelwa Germano JF-Expert Member

  #13
  Jun 4, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 789
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Maige anapaswa kuchukua maamuzi magumu na kujivua gamba....kulalamika unanyeshewa na mvua wakati upo kwenye bati lenye matundu ni upuuzi, ezeka bati jipya.
   
 14. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #14
  Jun 4, 2012
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  wengine wanasema ana hotel kahama, hilo analisemeaje?
   
 15. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #15
  Jun 4, 2012
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,073
  Likes Received: 1,806
  Trophy Points: 280
  Maige hana jipya! ....
   
 16. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #16
  Jun 4, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Maige pole sana. Siasa ni mchezo mbaya sana, kama unabisha muulize Zitto Zuberi Kabwe.
   
 17. K

  Koba JF-Expert Member

  #17
  Jun 4, 2012
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 494
  Trophy Points: 180
  Hii Mr Maige seems like a sore loser tuu na haitakusaidia chochote binafsi or in politics,uwaziri/uraisi au cheo chochote ni dhamana tuu unapopewa unafanya kazi kwa bidii na uaminifu ukiondolewa no matter what you be like a man unasema thank you mr president.... na kumtakia mema na kumsaidia anayekuja in transition ili aanze vizuri,kwa wanaokuita mwizi au mla rushwa wakumbushe we have justice system na huna haja ya kujibu hizi kashfa kwenye facebook au magazetini,bado mdogo wewe kama unataka kusaidia wananchi wenzako kuna millions ways sio lazima uwe waziri au in politics.
   
 18. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #18
  Jun 4, 2012
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  kama alikuwa amekopa pesa, na anafanya biashara inayoingiza pesa nyingi kiasi hicho, sasa uwaziri kwake wa nini, si aendelee kufanya biashara sasa, afu uwaziri utakuwa ulikuwa unamzidishia mzigo kwenye biashara yake ya hela nyingi....ndo maana tunasema biashara na uongozi viwe maji na mafuta...
   
 19. Smartboy

  Smartboy JF-Expert Member

  #19
  Jun 4, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,110
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  hivi wabaya wake ni kina nani, mbona hawataji
   
 20. Smartboy

  Smartboy JF-Expert Member

  #20
  Jun 4, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,110
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  mIGE AJE CDM HAYA MENGINE NI POROJO TU
   
Loading...