Elections 2010 Mhe Dr Slaa ya Zanzibar 1995 kutokea Tanganyika 2010

Sokomoko

JF-Expert Member
Mar 29, 2008
1,915
1,195
Ndugu wana JF,

Kama Dr Slaa akikataa kukubali matokeo ya uchaguzi uliomalizika punde na kutangazwa Kikwete ndio mshindi. Tunakumbuka jinsi hali ilivyokuwa kule zanzibar baada ya uchaguzi wa kwanza Maalim Seif alikataa matokeo na nchi ikaingia kwenye mgogoro mkubwa wa kisiasa uliopelekea misaada kutoka nchi wahisani kusitishwa sio kwa Tanzania visiwani tu bali mpaka kwa upande wa Tanzania bara.

Kwa maana hiyo nachukua nafasi hii kumsii Dr Slaa akubali kama wenzake walivyokubali lakini at the same time atoe dukuduku lake nini kifanyike ili next election kuwe kuna fair election.

Maalim Seif sio kama ameshindwa ila ameangalia mbali sana na kuona kwanini wananchi wa Zanzibar waumie kimaisha kwa ajili ya siasa? ameamua kukubali ili wajenge nchi na polepole CUF kujenga trust kwa wananchi na jumuia za kimataifa kuwa wanaweza kutawala na sio CCM pekee inayoweza kama Mkapa navyojinasibu.

My take:

Slaa akubali kushindwa aseme uchaguzi ulikuwa huru ila haukua wa haki na atoe facts zake maana kwa kukataa maisha ya mwananchi wa kawaida yatakuwa magumu na ile ndoto ya saruji kupungua bei maana atakapokuja kutwaa uongozi hapo baadae bei itakuwa imepaa sana.

Mhe. Dr Slaa kukataa kwako kutasababisha ugumu wa maisha kwetu ila wale unaowagomea wao wataendelea kula kuku kwa mrija take your time fikiria kwa makini.

Naomba tulijadili hili.
 
Companero

Platinum Member
Jul 12, 2008
5,605
2,000
Ujumbe wako hauendani na hii sahihi yako hapo juu hebu ibadili kwanza: I'd rather die standing than live kneeling (Che guavara)
 
bojuka

Senior Member
Sep 9, 2010
128
0
tangu lini mwenye mali akamnyenyeke a mwizi
dr. msimamo wako endelea nao na UN wajue kilichofanyika ili mwaka 2015 yasijirudie haya.
 
Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
10,830
2,000
Ndugu wana JF,

Kama Dr Slaa akikataa kukubali matokeo ya uchaguzi uliomalizika punde na kutangazwa Kikwete ndio mshindi. Tunakumbuka jinsi hali ilivyokuwa kule zanzibar baada ya uchaguzi wa kwanza Maalim Seif alikataa matokeo na nchi ikaingia kwenye mgogoro mkubwa wa kisiasa uliopelekea misaada kutoka nchi wahisani kusitishwa sio kwa Tanzania visiwani tu bali mpaka kwa upande wa Tanzania bara.

Kwa maana hiyo nachukua nafasi hii kumsii Dr Slaa akubali kama wenzake walivyokubali lakini at the same time atoe dukuduku lake nini kifanyike ili next election kuwe kuna fair election.

Maalim Seif sio kama ameshindwa ila ameangalia mbali sana na kuona kwanini wananchi wa Zanzibar waumie kimaisha kwa ajili ya siasa? ameamua kukubali ili wajenge nchi na polepole CUF kujenga trust kwa wananchi na jumuia za kimataifa kuwa wanaweza kutawala na sio CCM pekee inayoweza kama Mkapa navyojinasibu.

My take:

Slaa akubali kushindwa aseme uchaguzi ulikuwa huru ila haukua wa haki na atoe facts zake maana kwa kukataa maisha ya mwananchi wa kawaida yatakuwa magumu na ile ndoto ya saruji kupungua bei maana atakapokuja kutwaa uongozi hapo baadae bei itakuwa imepaa sana.

Mhe. Dr Slaa kukataa kwako kutasababisha ugumu wa maisha kwetu ila wale unaowagomea wao wataendelea kula kuku kwa mrija take your time fikiria kwa makini.

Naomba tulijadili hili.

Misaada?
Misaaada?
misaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaada?

Hopeless thinking
 
Lukolo

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
5,147

Mkuu Sokomoko, pamoja na ukweli kwamba tumekuwa tukitofautiana sana itikadi za kisiasa, katika hili naomba nikuunge mkono. Ni ukweli kwamba CCM wamefanya dhuluma ambayo haivumiliki, lakini ni vema Dr Slaa akajishusha ili kuokoa maisha ya watanzania wasio na hatia. Kwa kauli yoyote atakayoitoa Dr Slaa yenye kuashiria au kuhamasisha fujo, ni lazima itagharimu maisha ya watu kwa vyovyote vile. Maana CCM hawana hiyo huruma kwa watanzania, katu hawataona shida kuua. Hawana kabisa roho ya ubinadamu hawa watu. Ili kulinda maisha ya hao watanzania ambao yumkini yanaweza kupotea, Dr. Slaa abaki kimya kwa sasa hadi hasira za watu zipungue, na aje atoe tamko hapo baadaye lakini lenye lengo la kuitaka serikali irekebishe mfumo wa uchaguzi. We are tired of CCM, but we also love our children, parents, brothers and sisters and we want them to live.
 
Sokomoko

JF-Expert Member
Mar 29, 2008
1,915
1,195
tangu lini mwenye mali akamnyenyeke a mwizi
dr. msimamo wako endelea nao na UN wajue kilichofanyika ili mwaka 2015 yasijirudie haya.

kama hayo yangekuwa yanafanya kazi yangefanya kwa znz
 
PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,212
2,000
Msianze kutubembeleza saa hizi!
This is just the dawn of situation!...kwani hamkujua what could be the end results za kufanya ridging?
Tusipoumia kidogo kama taifa tutaendelea kufanya makosa coming 2015.
Nitafurahi sana tukipitia kwenye wakati mgumu!
Slaa, wembe ni uleule, tuko nyuma yako sana!
 
Mkuu PakaJimmy, heshima mbele!! Tatizo la vita, ni vigumu sana kutabiri kama itakuwa kidogo au sana. Mkishaanza kuua mtu mmoja, basi vitafuata visasi. Hapo ndipo mtakaposhangaa kwamba vita inaenea kila kona ya nchi, na hata usuluhishaji unakuwa mgumu. Unafikiri wanyarwanda walijua kama wangefikia kuuana kiasi kile? Mimi nafikiri tusiende huko wakuu zangu, wanyarwanda, waburundi, wakongo, wasomali, wasudan, wanauana kila siku, na hakuna kilichobadilika. Maisha yao yameendelea kuwa as hectic as it was before those killings. Ni bora tuitwe makondoo lakini tuwe salama.

Tuchukue mfano wa Kenya. Wakenya zaidi ya 2000 wamepoteza maisha kumtetea Odinga na chama cha ODM. Mwisho wa siku wamekwenda kujiongezea malupulupu bungeni na kusahau kwamba kuna watu waliokufa kwa ajili yao. Tunatambua umhimu wa haki ya raia kuheshimiwa, lakini kuingia kwenye machafuko ni kudhulumu haki ya watu ya kuishi. Zote ni dhuluma. Tuilinde amani yetu kwa nguvu zetu zote, maana ikipotea tu, itakuwa kazi ngumu sana kuirudisha.
 
Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,176
2,000
Slaa anajua wazi kua watanzania walio wengi ni wenye akili hawawezu hata siku moja kufata mambo yasio na maslahi na wao

na hao wehu wachache wajaribu kutupima how smart we are ?

kwenye amani ya nchi hatumbelezani na wala hatuna mzaha na wajaribu waone

mti na macho
 
dwight

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
476
250
We ulietoa mada ni waukweli mno,watakaokufa ni watu wa kawaida na hawa mashabiki wenye jazba za kushindwa.
 
Njowepo

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
9,536
2,000
Dunia nzima inapaswa kujua haya madudu hasa kwa upande wa ubunge na matokeo yake
 
Mtende

JF-Expert Member
Sep 27, 2010
6,387
2,000
Misaada?
Misaaada?
misaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaada?

Hopeless thinking

dependent minded
narrow and poor thinking
lazyness ideas
nonesense

mtategemea misaada mpaka lili?
why dont u stand by ur self while miguu tunyoooo?au hadi usimamie magongo?
 
Mallaba

JF-Expert Member
Jan 30, 2008
2,555
1,170
yaani unakubali kuuza haki yako eti kisa ni misaada,duh ndio maana tutaendelea kuwa masikini kwa kuwa viwete wa akili,fedha wanazozitumia kutunyang'anya haki kama zingetumika vizuri wala tusingehitaji hiyo misaada.Ni kuulize hivi tanzania tumeanza kupewa misaada tangu lini? je hiyo misaada huwa inawafikia walengwa?Tatizo la watanzania ni wepesoi sana wa kukata tamaa na kujifnya kusamehe kinafiki wakati wanaumia,mbadilike lasivyo miaka mingine 50 inakuja na mtaendelea kuwa hivyo hivyo,wenye navyo wanaendelea kuwa mabilionea na masikini wanazidi kufia ndani hata msosi hawajui waende wapi wakale.
Ndugu wana JF,

Kama Dr Slaa akikataa kukubali matokeo ya uchaguzi uliomalizika punde na kutangazwa Kikwete ndio mshindi. Tunakumbuka jinsi hali ilivyokuwa kule zanzibar baada ya uchaguzi wa kwanza Maalim Seif alikataa matokeo na nchi ikaingia kwenye mgogoro mkubwa wa kisiasa uliopelekea misaada kutoka nchi wahisani kusitishwa sio kwa Tanzania visiwani tu bali mpaka kwa upande wa Tanzania bara.

Kwa maana hiyo nachukua nafasi hii kumsii Dr Slaa akubali kama wenzake walivyokubali lakini at the same time atoe dukuduku lake nini kifanyike ili next election kuwe kuna fair election.

Maalim Seif sio kama ameshindwa ila ameangalia mbali sana na kuona kwanini wananchi wa Zanzibar waumie kimaisha kwa ajili ya siasa? ameamua kukubali ili wajenge nchi na polepole CUF kujenga trust kwa wananchi na jumuia za kimataifa kuwa wanaweza kutawala na sio CCM pekee inayoweza kama Mkapa navyojinasibu.

My take:

Slaa akubali kushindwa aseme uchaguzi ulikuwa huru ila haukua wa haki na atoe facts zake maana kwa kukataa maisha ya mwananchi wa kawaida yatakuwa magumu na ile ndoto ya saruji kupungua bei maana atakapokuja kutwaa uongozi hapo baadae bei itakuwa imepaa sana.

Mhe. Dr Slaa kukataa kwako kutasababisha ugumu wa maisha kwetu ila wale unaowagomea wao wataendelea kula kuku kwa mrija take your time fikiria kwa makini.

Naomba tulijadili hili.
 
Sokomoko

JF-Expert Member
Mar 29, 2008
1,915
1,195
We ulietoa mada ni waukweli mno,watakaokufa ni watu wa kawaida na hawa mashabiki wenye jazba za kushindwa.

Nakubaliana na wewe mia kwa mia kujua wajue then nchi iendelee, hivi unadhani dunia haijui kama Maalim Seif na safari hii kaibiwa? wanajua ila amewaonea imani wananchi wa Zanzibar angekataa wangeteseka na ugumu wa maisha ilhali yeye anaponda raha na kubadilisha mboga. Tafakarini jamani maana hawa wanasiasa sometimes wanataka kututmia kama ngazi.

My take.

Slaa kubali kwa grounds kuwa NEC ni yao na ndio maana ameshinda INFACT Slaa atakuwa wa ajabu sana akiamini kuwa kwa tume iliyokuwepo ingemtangaza yeye mshindi na hapo ndio ninapo pata wasiwasi uelewa wa viongozi wetu sijui ni kweli wana nia ya dhati kututumika au laa.
 
Sokomoko

JF-Expert Member
Mar 29, 2008
1,915
1,195
yaani unakubali kuuza haki yako eti kisa ni misaada,duh ndio maana tutaendelea kuwa masikini kwa kuwa viwete wa akili,fedha wanazozitumia kutunyang'anya haki kama zingetumika vizuri wala tusingehitaji hiyo misaada.Ni kuulize hivi tanzania tumeanza kupewa misaada tangu lini? je hiyo misaada huwa inawafikia walengwa?Tatizo la watanzania ni wepesoi sana wa kukata tamaa na kujifnya kusamehe kinafiki wakati wanaumia,mbadilike lasivyo miaka mingine 50 inakuja na mtaendelea kuwa hivyo hivyo,wenye navyo wanaendelea kuwa mabilionea na masikini wanazidi kufia ndani hata msosi hawajui waende wapi wakale.

Hujakatazwa ingia barabarani ufanye fujo pengine wakifa watu kama laki moja hivi chadema mtapewa nchi maana siwaelewi hakuna mtu asietaka mabadiliko jamani kila mmoja anataka mabadiliko lakini angalieni mazingira yenyewe pangeni mikakati sio mkitaka tu basi na iwe mnavyoyatamani madaraka mjue na wenzenu wanayatamani hivyo hivyo... kama nia ni ya kutumikia wananchi basi hatuna budi kukaa na kupanga mikakati tuna wabunge tuwatumie kutuletea tume ya uchaguzi yenye uwakilishi wa vyama vyetu ili at end of the day tupate tunachokihitaji bila kumwaga damu wala watu kufa njaa.
 
The Invincible

JF-Expert Member
May 6, 2006
5,998
2,000
Slaa akubali matokeo? Huu utakuwa mzaha wa mwaka.

CCM dawa yao ni kuwakomalia hivyo hivyo. Chadema haiwezi kulinganishwa na CUF Zanzibar. Viongozi wa CUF ni wachumia tumbo. Bwana Seif Hamad anataka kustaafu akiwa serikalini, hakuna la zaidi.

Kwa wote wenye uchungu na nchi, hakuna kukubali matokeo yaliyochakachuliwa. Utakuwa ni utaahira na ubinafsi wa kiwango cha juu unaofanana na wa chama cha majuha - CCM.

Aluta continua! Hakuna kulala mpaka kieleweke.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom