Mhe. Dkt. Shogo Mlozi Ashiriki Semina ya EALA Women Caucus Bujumbura

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,858
930
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (Member of Parliament - EALA ) Mhe. Dkt. Shogo Mlozi Sedoyeka, PhD anashiriki semina ya EALA Women Caucus juu ya Kuendeleza Utawala unaozingatia Jinsia 31.3.2023 nchini Burundi, Bujumbura.​

Semina ni kwa ajili ya kujenga uwezo kwa wabunge wanawake ili kutetea masuala ya kijinsia na Agenda ya haki za binadamu katika utekelezaji wa shughuli za bunge zinazojumuisha Kutunga Sheria, Usimamizi, na Uwakilishi ili kuchangia kikamilifu kufikia Agenda 2063 ya AU; na SDGs.

Mhe. Joseph Ntakirutimana, Spika wa EALA alifungua semina hiyo akiwa pamoja na Mhe. Dkt. Anne Itto (South Sudan Chapter), Mwenyekiti wa EALA Women Caucus.

Mhe. Dkt. Shogo Mlozi Sedoyeka alipowasili jijini Bujumbura mnamo tarehe 28.3.2023 alipata nafasi ya kumsalimia Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye, ambapo Mhe. Mlozi anasema ilikuwa na heshima kubwa sana kwake.
WhatsApp Image 2023-04-02 at 10.05.48.jpeg
WhatsApp Image 2023-04-02 at 10.05.49(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-04-02 at 10.05.48(1).jpeg
 
Back
Top Bottom