Condester Sichalwe: Elimu ya Diplomasia ya Uchumi Itolewe Kwenye Mabaraza ya Madiwani ili Iwafikie Wananchi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,851
928
MHE. CONDESTER SICHALWE - ELIMU YA DIPLOMASIA YA UCHUMI ITOLEWE KWENYE MABARAZA YA MADIWANI ILI IWAFIKIE WANANCHI

"Diplomasia ya Uchumi ni kipaumbele cha Wizara ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Afrika Mashariki. Bajeti iliyopita nilichangia kuhusu vikwazo vya wafanyabiashara wanaoliendea soko la Zambia 🇿🇲 na soko la DRC Kongo kupitia Zambia. Waziri sema neno, bado unatambua wafanyabiashara wanaendelea kupitia vikwazo?" - Mhe. Condester Mundy Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba

"Wizara imesema Kipaumbele namba moja ni Diplomasia ya Uchumi. Kamati inasema Diplomasia ya Uchumi haijaeleweka vizuri kwa wananchi na viongozi wanaosimamia Sekta hizo" - Mhe. Condester Mundy Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba

"Diplomasia ya Uchumi kwa wananchi wa kawaida bado hawajaijua ni nini, Wengi wanadhani Diplomasia ya Uchumi inawahusu wanaotembea kwenye Red Carpet. Lakini tunaamini kwamba kwenye Diplomasia ya Uchumi ndipo palipo na ajira nyingi sana za na zinaweza kukuza uchumi wetu kwa kiwango kikubwa sana" - Mhe. Condester Mundy Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba

"Mwaka jana/juzi tulipewa soko kubwa sana China 🇨🇳 la kupeleka Soya, lakini ilifika hatua hatuwezi kupata Soya hapa Tanzania 🇹🇿 na ilipelekea Watanzania wakawa wanachukua Soya nyingi kutoka Zambia 🇿🇲. Mpakani Tunduma ilikuwa ndiyo biashara kila mtu alikuwa anatafuta Soya" - Mhe. Condester Mundy Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba

"Sisi hapa Tanzania 🇹🇿 tuna Halmashauri 184, tuchukue Halmashauri 100 tu za wakulima mfano Momba, tungewapa tageti wazalishe Soya tani Milioni Moja ambapo kila Halmashauri ingezalisha Soya tani 10 ambacho ni kitu kinawezekana. Matokeo yake tunawasaidia Zambia kuwakuzia Uchumi" - Mhe. Condester Mundy Michael Sichalwe

"Diplomasia ya Uchumi ni mbinu na mkakati unaotumiwa na Nchi na Mashirika ya kimataifa katika kukuza maslahi yao kiuchumi, nje na mipaka yao. Lengo la Diplomasia ya Uchumi ni kuimarisha Uhusiano wa kiuchumi, kibiashara, Uwekezaji na Ushirikiano wa kiufundi kati ya nchi na kuboresha hali ya Uchumi Kitaifa" - Mhe. Condester Mundy Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba

"Diplomasia ya Uchumi inahusisha shughuli kadhaa ikiwa ni pamoja na Uendelezaji wa biashara na Uwekezaji. Nchi zinatumia Diplomasia ya Uchumi kukuza biashara na Uwekezaji kwa kuvutia wawekezaji na kujenga mazingira mazuri ya kibiashara, hivyo wafanyabiashara husaini Mikataba ya biashara na makubaliano na Uwekezaji kushirikiana katika masuala ya kibiashara na kibenki na Ushirikiano wa kiufundi" - Mhe. Condester Mundy Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba

"Diplomasia ya kiuchumi inahusisha kubadirishana Maarifa na Teknolojia. Nchi zinaweza kuweka Mikataba ya Ushirikiano wa kiufundi katika maeneo ya Kilimo, Afya, Nishati, Miundombinu na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano. Hii inaweza kuimarisha Teknolojia na Ujuzi na inachangia katika maendeleo ya Uchumi wa nchi zinazoshirikiana" - Mhe. Condester Mundy Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba

"Katika Diplomasia ya Uchumi nchi zinaweza kutuma wawakilishi wa Serikali kama Mabalozi wa Uchumi au Wajumbe wa biashara kwenye nchi zingine. Hao hufanya mazungumzo na kuwakilisha Serikali na wafanyabiashara, fursa za biashara na Ushirikiano kiuchumi" - Mhe. Condester Mundy Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba

"Malengo ya Diplomasia ya Uchumi ni pamoja na kuongeza mauzo ya nje na bidhaa na huduma, kujenga mtandao wa biashara wa washirika wa kimataifa, kuvutia wawekezaji wa kigeni, kukuza viwanda vya ndani" - Mhe. Condester Mundy Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba

"Tunakuzaje viwanda vya ndani kama hatumshirikishi mwananchi wa kawaida anayefanya shughuli ndogo ndogo hasa kupitia hii Diplomasia ya Uchumi ambayo inamuhusisha?" - Mhe. Condester Mundy Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba

"Wizara ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Afrika Mashariki ilisema inatoa Elimu mbalimbali kwenye Mambo ya Diplomasia ya Uchumi, kwenye Magazeti na Radio" - Mhe. Condester Mundy Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba.

"Niombe Elimu ya Diplomasia ya Uchumi iende kwenye Mabaraza ya Madiwani. Wizara ya Mambo ya Nje muweke dirisha kwenye Wizara ya TAMISEMI ambao wao wanazijua Halmashauri na uwezo wao, wanajua vipato vya Halmashauri.
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2023-05-30 at 14.46.45(1).mp4
    35.8 MB
Back
Top Bottom