Mhe. Baruani: Bunge lijadili kumkomboa mtanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mhe. Baruani: Bunge lijadili kumkomboa mtanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gobegobe, Feb 10, 2011.

  1. Gobegobe

    Gobegobe JF-Expert Member

    #1
    Feb 10, 2011
    Joined: Nov 23, 2010
    Messages: 245
    Likes Received: 1
    Trophy Points: 35
    Walau kwa leo nimeguswa na hoja iliyotolewa na Mheshimwa Baruani Mbunge wa Lindi, kwamba, wakati mijadala ya BUnge inaendelea pengine ingekuwa vema wakawa wanaonyeshwa picha ya maisha halisi ya mtanzania wanayemwakilisha. Kwa kufanya hivyo, kwa maoni yake Mheshimiwa Mbunge itasaidia kurudisha akili za wachangiaji kwenye hoja za msingi badala ya kupiga porojo kama wanavyoonekana na kusikika wakifanya.

    Kilichonigusa ni jinsi ambavyo Mheshimiwa Mbunge anaonekana kukerwa kutoka moyoni na jinsi wabunge wenzie wanavyokwepa kwa makusudi kujadili mustakabali wa taifa na kuishia kujadili hoja zosizo na mashiko. Moto huo huo Baruani
     
  2. PhD

    PhD JF-Expert Member

    #2
    Feb 10, 2011
    Joined: Jul 15, 2009
    Messages: 3,803
    Likes Received: 777
    Trophy Points: 280
    nimeupenda sana mchango wa huyu bwana, nahisi kwa wabunge wote wa CUF huyu pekee ndiye anazungumza objectively mungu amlinde sana
     
  3. Gsana

    Gsana JF-Expert Member

    #3
    Feb 10, 2011
    Joined: Aug 28, 2010
    Messages: 4,104
    Likes Received: 92
    Trophy Points: 145
    Kwa kweli Baruani kaongea vizuri. Pia aliyefuatia Peter Serukamba katoa point. Peter kaongea kiuchumi zaidi,anahoji kontena linatoka Dubai mpaka dar kwa siku 18,lakini kutoka dar mpaka rwanda ni siku 49 na hapo unakutana na vizuizi 58 na traffics,je unategemea wanyaranda warudi tena dar au unataka kumtafuta mchawi? Pia kaongelea ardhi kama security! Kwa leo hawa watu wamerudisha hamu yangu ya kusikiliza bunge. All in all hotuba ya rais haina uzito!
     
  4. mfarisayo

    mfarisayo JF-Expert Member

    #4
    Feb 10, 2011
    Joined: Nov 23, 2010
    Messages: 4,929
    Likes Received: 87
    Trophy Points: 145
    gud mh. baruani
     
  5. c

    chumakipate Member

    #5
    Feb 10, 2011
    Joined: Dec 18, 2010
    Messages: 86
    Likes Received: 0
    Trophy Points: 13
    Kwa kweli bar'wan amenifurahisha sana badala ya wabunge kujadili matatizo ya wananchi ccm imebaki kwenye mipasho ninyi wabunge wa ccm wananchi ndicho walichowatuma?mtakwenda kujibu.eti sisi ni wawakilishi wa wananchi wamewambia ukatoe utumbo huo au collective behaviour imewa-affect.unakurupushwa na mkeo au hawara yako(refer hotuba fulani ya mwl.nyerere) ukajadili mipasho wananchi wanataka utatuzi wa matatizo yao.mbunge unapoteza dakika nyingi kuongelea fulani alitoka bungeni sasa anajadili nini.ina maana hata sisi tunaosikiliza kupitia luninga ni mbumbumbu hatujui kitu teknohama imekua.bar'wan umeonyesha njia hukutawaliwa na matakwa ya kundi fulani.keep it up bar'wan waliokuchagua wanaweza kujisifu sio ukiulizwa mbunge wako nani unaona hata aibu kujibu kwa madudu wanayoyafanya.bar'wan si cuf tu ila ni zaidi ya mbunge.bravo
     
Loading...