Mhaya vs Mjaluo

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Sep 20, 2021
3,215
3,587
Nyanja: Mahusiano

(tukio siyo halisi)

Mjaluo Mwl. James Okulo NyakwarChanga wa Kowak (a.k.a Home of Intellectuals) Rorya na Mhaya Rugumamu Ruguyamheto Rutabanzibwa wa Rubya wanalewa kwenye Buffet ya Meli mpya MV Victoria (almaarufu Mama Koku) wakiwa safarini toka Kemondo Bay kwenda Mwanza. Kama zilivyo jadi zao wakaanza kutambiana umaarufu na ubora wa makabila yao:-

  • Mhaya – sisi Wahaya tunawazidi Wajaluo kwa Maprofesa.
  • Mjaluo – sisi Wajaluo tunawazidi kwa Marais. Hakuna Mhaya amewahikuwa rais duniani.
  • Mhaya – maweee… ebu taja Mjaluo hata mmoja tu! Au umelewa sana wewe?
  • Mjaluo – Obama Barak, Garang John, Kiir Salva Mayardit, Okello Tito, Obote Milton, Obasanjo Olusegun (Mjaluo wa ukoo wa Owu wa Yoruba), Idd Amin Oumee b/o Nyabire, Raila Odinga (the President that never was). Wamefika wangapi hapo?
  • Mhaya – kashikwa na butwaa kidogo! My God! How comes kabila moja dogo hili linatoa Marais wengi namna hiyo?! Hawa jamaa hatari ee?!
  • Mhaya – lakini nyie hamjawahi kutoa Kardinali.
  • Mjaluo – Kardinali Otunga Maurice Michael (A Luo naturalized in Maragoli Bungoma County Western Kenya).
  • Mhaya – hamjawahi kutoa Jenerali nyie?
  • Mjaluo – Jenerali Opande Ojijo Daniel (Kamanda wa Jeshi la Umoja wa Mataifa la kulinda amani Liberia, Sierra Leone, Namibia na Msumbiji), Luteni Jenerali Francis Omondi Ogolla, Jenerali Tito Okello ((Field Marshal) Wahaya hamna Field Marshal), Jenerali Oyite Ojok, Jenerali Idd Amin Oumee, Jenerali John Garang, Jasusi Jenerali Salva Kiir Mayardit, Jenerali Olusegun Obasanjo (Mjaluo wa ukoo wa Owu wa Yoruba), Jenerali Odumegwu Ojukwu (Mjaluo kwa asili wa ukoo wa Igbo), Jenerali Joseph Kony (Konyi kwa lugha ya Kijaluo inamaanisha ‘shauri yako’ pia inamaanisha ‘inakusaidia’).
  • Mhaya – kwahiyo mpo lakini hamvumi?
  • Mjaluo – unataka Marais wote hao kuvuma mpaka wawe Ma-Advocates?
  • Mhaya – hahahaaa… wewe jaluo kanywe nyuka huko Rorya.
  • Mjaluo – hakuna Mhaya sura yake imewahi kuwekwa kwenye fedha yoyote duniani, sisi Wajaluo mujarab kabisa, habari ndiyo hiyo mtani wangu Rugu… Rugu...
  • Mhaya – sasa nyie Wajaluo, baada ya serikali kuua biashara yenu ya mihuri mnaishije mijini?
  • Mjaluo – nyie Wahaya, baada ya REA kuua makoroboi Mwanza Atu na Koku wanaishije?
  • Mhaya – nyie Wajaluo siyo Wakenya kweli nyie?
  • Mjaluo – nyie Wahaya siyo Waganda kweli nyie?
  • Mjaluo – wewe Mhaya, sikiliza nikwambie Wajaluo ni nani hapa duniani na wana dira gani kabla Yesu hajarudi, utagundua na kukubaliana nami kwamba Wajaluo ni kama Wayahudi (unawezawaita Wayahudi-weusi). Kama Wayahudi walivyo, Wajaluo pia walitwaliwa eneo lao na Waarabu wa Sudan, baadhi yao kama Wayahudi, wakasambaa maeneo mbalimbali ya dunia kama Uganda, Kenya, Tanganyika, Nigeria na nje ya Afrika kupitia biashara ya masafa marefu (Long Distance Trade), biashara ya utumwa (Slave Trade), uvuvi (mto Nile hadi ziwa Victoria) na biashara ya kuvuka bahari ya Atlantiki (Trans Atlantic Trade). Kupatikana kwa taifa lao Sudan Kusini kuna kila dalili kwamba taifa hili linaenda kuwa na nguvu kubwa kama Israel ya Wayahudi na hasa endapo Sudan Kusini itawataka warudi nyumbani washirikiane kujenga taifa lao hilo kama Wayahudi wa Israel wanavyofanya. Sasa sikiliza haya: Wajaluo wana hisia kali za utaifa (strong sense of nationalism), siku zote popote walipo wanatafuta kwa bidii utaifa wao, wakishindwa wanameza/wanabadili (tamaduni) makabila yanayoishi miongoni mwao. Kule Sudan, wamepambana hadi wakapata taifa lao Sudan Kusini ambako ndiko asili yao (origination). Kule Nigeria, Jenerali Odumegwu Ojukwu (Mjaluo kwa asili, wa ukoo wa Igbo) alianzisha vuguvugu la Biafra kudai utaifa wao wakashindwa. Uganda, Alice Lakwena Abongonowot alianzisha vuguvugu la kutaka eneo lao litambuliwe kama taifa akazimwa akafa, Joseph Kony akapokea harakati hizo toka kwa Alice Lakwena Abongonowot, akashindwa jumla. Kule Kenya, naona wanaota ndoto hizo za utaifa wao baada ya kiu ya kutawala Kenya kwa njia ya uchaguzi kushindikana. Hapa kwetu Tanzania, hawataweza milele yote kwa sababu ndani ya maeneo yao kuna makabila/lahaja nyingi wamechanganyikana nao, hivyo hawana ngome maalum ya Kijaluo (sphere of influence), ukienda Mugango Musoma Vijijini wapo, ukienda Buhemba Butiama wapo, ukienda Mugumu Serengeti wapo, ukienda Ngoreme wapo, ukienda Mirerani wapo, Dsm, Mwanza na Arusha wana diaspora kubwa sana. Wajaluo wako kila kona ya dunia kama walivyokuwa Wayahudi waliotawanywa na Dola la Kirumi. Kule Australia, kuna Kijiji maarufu cha uvuvi kilichoanzishwa na Wajaluo. Kule Michigan USA 1880 kulikuwa na Wajaluo wa ukoo wa Kowak na Canada 1911. Jimbo la Michigan lilikuwa na idadi kubwa ya ukoo wa Kowak 1880. Huko Michigan na Canada walikuwa maarufu kwa kazi za kitaalam za mashine na siyo vibarua kama nyie Wahaya www.ancestry.com , aidha, Profesa mmoja maarufu wa Sayansi-ya-Bahari aliyebobea kwenye uvuvi Mjaluo wa Tanzania, katika ziara zake za utalii-wa-kitafiti duniani aligundua kambi moja kubwa ya uvuvi Ireland iliyoanzishwa na Wajaluo. Wajaluo ni cosmopolitans, tofauti yao ya msingi na Wayahudi wa Israel siyo rangi bali ni ukarimu, Wajaluo ni wakarimu sana na wapenda amani sana. Kwa ukarimu huo, hayati Jaramogi Oginga Odinga alimwachia Jomo Kenyatta urais ambao Odinga ndiyo aliupigania wakati Kenyatta akiwa jela Kapenguria Magharibi ya Kenya. Kwa ukarimu wao huo Raila Odinga alimwachia Mwai Kibaki urais alioupigania wakati Kibaki akiwa kwenye utalii-wa-kimatibabu (Medical Tourism) Uingereza kwenye taasisi ya mifupa kufuatia kuvunjwa mguu kwenye kampeni za uchaguzi. Olusegun Obasanjo mara kadhaa amekabidhi uongozi kwenye serikali ya kiraia kwa njia ya uchaguzi huru na haki ili kutekeleza demokrasia (hakung’ang’ania kubaki ikulu). Tito Okello alimtengenezea njia Milton Obote. Mjaluo (Myahudi mweusi) ni mkarimu kwa viwango vilivyopitiliza mahitaji.
  • Abiria – Nahodha, mdahalo mtamu huu na tunakaribia Mwanza, ebu fululiza hadi bandari ya Sota – Shirati tumpeleke Mjaluo kwao ili tuendelee kufaidi mdahalo njiani, baadaye ndiyo tugeuze tuje Mwanza.
Naomba kura zote.
 
Nawakaribisha wengine Rorya waje waoe au waolewe kwa Wajaluo ili wapate mbegu ya kijaluo preferably ukoo wa Kowak (home of intellectuals).
 
wajaruo umetupa credit sjawai skia. ujazungumzia ile samaki Kamongo mbona hvyo jamani.
 
wajaruo umetupa credit sjawai skia. ujazungumzia ile samaki Kamongo mbona hvyo jamani.
OIP.DNlK1VZxs-O9NiNpUZvWkAHaCT

Taswira kwa hisani ya Google.
 
Omera umemaliza kila kitu.😁😁😁 ila wajaluo ni watu wa sifa sana ndio maana wahaya ni watani zetu.
 
Back
Top Bottom