Mhasibu wa zahanati ya Tambukareli mbaroni kwa kuisababishia serikali hasara ya Tsh. Milioni 14

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
546
1,000
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Temeke Jijini Dar es salaam imefanya uchunguzi dhidi ya mhasibu wa zahanati ya Tambukareli iliyopo katika kata ya Azimio, kwa makosa yafuatayo:

(1) Kuisababishia hasara serikali kinyume na kifungu namba 284 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2020 pamoja na

(2) Wizi kwa mtumishi wa Umma kinyume na kifungu na 265 na 270 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2020

TAKUKURU iliokea malalamiko tarehe 28/01/2019 dhidi ya Simon John Mbilanga aliekuwa mhasibu wa zahanati hiyo kuwa alikuwa anakusanya maduhuli au fedha za mapato ya serikali na kutozipeleka benki

TAKUKURU iligundua kuwa kati ya mwaka 2015-2016 Simon John Mbilanga alipokuwa kwenye majukumu yake ya kikazi aliisababishia hasara serikali ya sh. 14,572,800/= kwa kufanyia matumizi binafsi ya fedha alizokuwa akikusanya badala ya kuzipeleka benki.

Uchunguzi umekamilika na TAKUKURU kwa kushirikiana na ofisi ya Taifa ya mashitaka leo tarehe 10/06/2020 mtuhumiwa natarajiwa kufunguliwa kesi ya kuisababishia hasara serikali ya sh.milioni 14 kinyume cha kifungu namba 284 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2020 na wizi kwa mtumishi wa Umma kinyume na kifungu na 265 na 270 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2020
 

Attachments

  • File size
    551.4 KB
    Views
    8

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom