BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,825
- 287,847
Mhasibu TRA ajilipua kwa risasi
Mwandishi Wetu
Daily News; Saturday,July 26, 2008 @00:02
Mhasibu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Joseph Stephen (45) amejiua kwa kujipiga risasi mbili katika paji la uso juzi mchana nyumbani kwake Mbagala, Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa Stephen alikuwa Mhasibu wa TRA katika Ofisi ya Forodha na kwamba hakuacha maandishi hivyo sababu haijajulikana.
Ni kweli tumepata taarifa jana (juzi) kuwa mhasibu wa TRA amejipiga risasi muda mfupi baada ya kumpigia simu mke wake (hakumtaja jina) mfanyakazi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii Dar es Salaam akimtaka atoke kazini na kurudi nyumbani mara moja, alisema Kova.
Alisema mkewe alitii agizo hilo maana haikuwa jambo la kawaida kwa mumewe; na alipofika nyumbani kwao eneo la Mbagala Kwa Magaya, alimkuta mumewe akiwa amekufa chumbani. Majeraha yanaonyesha alijipiga risasi mbili katika paji la uso na zikatokea nyuma ya kichwa (uchogoni) na kwa kweli mpaka sasa hatujajua chanzo, lakini tunaendelea na uchunguzi, alisema Kova.
Wakati huo huo, Polisi Mkoa wa Dar es Salaam wamekamata magari mawili yenye namba za usajili T 190 AGU, Toyota Corolla na Toyota Baloon namba T 132 ANA; yakiwa na mali za wizi ambazo ni vitenge doti 60, khanga doti 32, drier mbili, karabai moja, redio na spika mbili.
Mali nyingine zilizokamatwa na askari wa doria jana alfajiri ni mkasi na bia aina mbalimbali; na watuhumiwa walikimbia baada ya kusimamishwa na polisi. Polisi wanafuatilia ili kufahamu wamiliki wa magari hayo, mali ilipoibwa na kuwasaka wahusika hao.
Aidha, katika operesheni ya wiki moja sasa, polisi inawashikilia wanawake 99 kwa tuhuma za kuhusika katika ukahaba katika maeneo mbalimbali ya jiji, yakiwamo Buguruni maeneo ya baa ya Achimwene, Kinondoni soko la Ma-Tx, Maisha Club, Ohio, Jolly Club na Hoteli ya Keys. Kova alisema kati yao, 21 waliachiwa baada ya kukiri na kuomba msamaha, lakini wengine hawataachiwa kutokana na kugundua kuwa wanahusika na usambazaji wa dawa za kulevya na utumiaji pia.