Mhasibu Muhimbili adaiwa kuiba sh mil 330

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
MHASIBU Msaidizi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam, Amos Kabisa, maarufu kwa jina la Angaya amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kusomewa mashitaka matatu likiwemo la wizi wa sh milioni 330.

Kabisa amesomewa mashitaka leo, alipelekwa Kisutu juzi na jana lakini hakusomewa madai hayo yanayomkabili.

Wakili wa Serikali, Epafras Njau, amedai mahakamani kuwa, mshitakiwa huyo alikula njama ya kutenda kosa, kughushi na akaiba fedha hizo mali ya benki ya NMB.

Njau amedai kuwa, Januari 21 mwaka huu katika benki hiyo iliyopo katika jengo la Bank House, mshitakiwa aliiba fedha hizo.

Imedaiwa kuwa, mshitakiwa huyo pia alighushi nyaraka za benki katika akaunti namba 2011000015 ya Jeshi la Polisi akionesha kuwa ni sahihi, na zilikuwa ni halali.

Wakili Njau aliiomba mahakama isimpe dhamana mshitakiwa na akatoa zuio la dhamana lililotolewa na Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP) chini ya kifungu cha sheria namba 1148 (4) cha mwenendo wa makosa ya jinai.

Mahakama ilikubaliana na ombi hilo, mshitakiwa amerudidishwa rumande hadi kesi hiyo itakapotajwa machi 10 mwaka huu.
 
hawa muhimbili wanaangalia zaidi CPA. hawaangalii vitu vingine. ndo maana wanalizwa. hata kama ni cashier wanataka CPA
 
Sio suala la CPA.Ni internal Controls.
Je mtu pekee anaweza kufanya huu wizi?Sidhani.

Sijui ulitaka mtu awe na NAD au NABOCE ?Tuambie
 
hawa muhimbili wanaangalia zaidi CPA. hawaangalii vitu vingine. ndo maana wanalizwa. hata kama ni cashier wanataka CPA

Halafu wachaga ndio wanaongoza kwa kuwa na CPA. Na mchaga mizimu yake imeshamwambia pesa zote halali yake.

Ukienda hapo hapo Muhimbili kwenye maternity ward watoto wa kichaga wakizaliwa hawalii mpaka udondoshe coin sakafuni vinginevyo wanakata kamba.

Mtoto wa kichaga mchanga ukimpa noti ya elfu kumi na dola mia achague anachagua zote. Wa kihaya anachagua ya dola mia, wa kisukuma anachagua ya elfu kumi, wa kikuria anakung'ata mkono, wa kizaramo analala hapo hapo bila kuchagua....haelewi kinachoendelea, wa kifipa anakucheulia mpaka noti ziharibike mkose wote.
 
Dah hatutaendelea kamwe, wizi kila kona jamani. na huyu jamaa hawezi iba peke yake lazima kuna chain kubwa tu ya ushirikiano hapo wa wizi. Pesa itamlinda atahonga kila sehemu, atapata mawakili wa nguvu, mwisho wa siku atawashinda
 
Halafu wachaga ndio wanaongoza kwa kuwa na CPA. Na mchaga mizimu yake imeshamwambia pesa zote halali yake.

Ukienda hapo hapo Muhimbili kwenye maternity ward watoto wa kichaga wakizaliwa hawalii mpaka udondoshe coin sakafuni vinginevyo wanakata kamba.

Mtoto wa kichaga mchanga ukimpa noti ya elfu kumi na dola mia achague anachagua zote. Wa kihaya anachagua ya dola mia, wa kisukuma anachagua ya elfu kumi, wa kikuria anakung'ata mkono, wa kizaramo analala hapo hapo bila kuchagua....haelewi kinachoendelea, wa kifipa anakucheulia mpaka noti ziharibike mkose wote.

Mkuu kwani huyo mhsibu ni mchaga?...
 
Mkuu kwani huyo mhsibu ni mchaga?...

Nilikuwa nalisubiri hili swali saana,,,angekuwa mchaga asingekamatwa baba. Halafu mchaga msomi haibi shilingi mbili hizo ebo? Unapiga kiepaepa, huku ukiendelea kutembelea mgongo wa kobe wa 1969.

Ninachomaanisha kwenye stori nzima ni kuwa tuna system mbovu ya uonevu, wanaacha kukamata wachaga(creative accounting embezzlement) wanakamata huyo halfcast wa kichaga na kindengereko!!

Nitamfuata huko selo nikampe mbinu za kushinda kesi, hapa hamna kesi hapa.

Alichofanya Amos ni kuwasaidia kuona ''Major weaknesses in Internal Controls''. Kwa hiyo anastahili pongezi. Ila nafasi ya kazi waliyoitangaza nitaiomba mimi, nitaficha hizi masters mbili nilizonazo na hii Phd, nitawaonyesha CPA tu, wakinipa nitakuwa nawapiga mara tatu ya hiyo na hawatakaa wajue kamwe.

Internal Controls zao ziko matatani, Hakuna Segregation of duties ya kutosha, hawana control ya check list kwa kusaidiana na benki, hawana Bank Confirmation ambayo ilitakiwa ifanywe na Ma-Director wakiwa wanajua kabisa malipo ni ya nini, mtu anakaa kwenye fedha muda mrefu bila kwenda likizo utajuje mapiko yake? Internal Audit Unit iko dhaifu na haitazamwi vizuri unategemea nini? We ngoja wanipe kazi, na watanipa tu...lazima nijenge viwanja vya ndege kama vitatu hivi.
 
Halafu wachaga ndio wanaongoza kwa kuwa na CPA. Na mchaga mizimu yake imeshamwambia pesa zote halali yake.

Ukienda hapo hapo Muhimbili kwenye maternity ward watoto wa kichaga wakizaliwa hawalii mpaka udondoshe coin sakafuni vinginevyo wanakata kamba.

Mtoto wa kichaga mchanga ukimpa noti ya elfu kumi na dola mia achague anachagua zote. Wa kihaya anachagua ya dola mia, wa kisukuma anachagua ya elfu kumi, wa kikuria anakung'ata mkono, wa kizaramo analala hapo hapo bila kuchagua....haelewi kinachoendelea, wa kifipa anakucheulia mpaka noti ziharibike mkose wote.

Hivi huwa hamchoki?

Eti wachaga wanapenda hela. Nani asiependa hela?
 
.

Internal Controls zao ziko matatani, Hakuna Segregation of duties ya kutosha, hawana control ya check list kwa kusaidiana na benki, hawana Bank Confirmation ambayo ilitakiwa ifanywe na Ma-Director wakiwa wanajua kabisa malipo ni ya nini, mtu anakaa kwenye fedha muda mrefu bila kwenda likizo utajuje mapiko yake? Internal Audit Unit iko dhaifu na haitazamwi vizuri unategemea nini? We ngoja wanipe kazi, na watanipa tu...lazima nijenge viwanja vya ndege kama vitatu hivi.

You raised a good point, however did you know even with strong internal control, COLLABORATION can invalidate all in a minute?

Nina hakika huyu uncle hakuna peke yangu in this deal....
 
Back
Top Bottom