Mhariri wa Rai, Danny Mwakiteleko Afariki Dunia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mhariri wa Rai, Danny Mwakiteleko Afariki Dunia

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by X-PASTER, Jul 23, 2011.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Jul 23, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mhariri wa gazeti la Rai, ambaye pia ni Naibu Mhariri Mtendaji wa New Habari (2006) Ltd, Danny Mwakiteleko, amefariki dunia.

  Habari ambazo blogu ya Beda Msimbe, "Lukwangule Ent." alizozipata alfajiri ya leo na kuthibitishwa na watu wa karibu zinasema kwamba Mwakiteleko amefariki leo alfajiri katika hoispitali ya Muhimbili.

  Mwakiteleko alilazwa katika kitengo cha watu mahututi Muhimbili baada ya ajali aliyoipata juzi usiku (jumatano) eneo la Tabata (ToT) na kukimbizwa katika Hospitali ya Amana, Ilala na baadaye Muhimbili.

  Katika ajali hiyo gari alilokuwa akiendesha Mwakiteleko liligongwa na lori lenye trela, ambalo lilitoweka bila kujulikana saa nne usiku. Mwakiteleko alikuwa akitokea kazini Sinza ambako alifanya kazi hadi saa tatu usiku.

  Mwakiteleko alipelekwa katika Hospitali ya Amana kwa uangalizi hadi saa 12 asubuhi, ambapo madaktari waliamua apelekwe Hospitali ya Taifa Muhimbili.

  Baada ya uchunguzi Muhimbili, madaktari walisema majeruhi alikuwa ameumia kichwani na kumfanya apoteze fahamu kiasi (semi-conscious) hivyo ikabidi apelekwe katika chumba cha upasuaji ambako madaktari walimhangaikia kuanzia saa sita hadi saa tisa mchana.

  Jana, Rais Jakaya Kikwete alikwenda kumwona na kuelezwa kwamba hali yake inaendelea vyema.


  [​IMG][​IMG]

  Source: wavuti
   
 2. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #2
  Jul 23, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Poleni Ndugu Jamaa na Marafiki
   
 3. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #3
  Jul 23, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  poleni ndugu, jamaa na marafiki kwa msiba huu mzito. Mungu ailaze roho ya marehemu pema peponi. Amina
   
 4. SIMBA mtoto

  SIMBA mtoto JF-Expert Member

  #4
  Jul 23, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 208
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Poleni familia ya Danny Mwakiteleko na wafanyakazi wa New Habari (2006) Ltd
   
 5. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #5
  Jul 23, 2011
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,813
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  RIP Danny
  Poleni familia, ndugu, jamaa, wafanyakazi wenzake na marafiki wote
  Mungu awape faraja wakati huu wa majonzi mazito
   
 6. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #6
  Jul 23, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,482
  Likes Received: 12,744
  Trophy Points: 280
  Aaah my good friend now YOU are gone, we are behind you! Rest in peace brother danny,we will miss you dearly!
   
 7. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #7
  Jul 24, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,210
  Likes Received: 3,774
  Trophy Points: 280
  Poleni wafiwa wote mungu ailaze roho ya Danny mahali pema peponi ame!
   
 8. Da Pretty

  Da Pretty JF-Expert Member

  #8
  Jul 24, 2011
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 3,050
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Poleni familia,ndugu,jamaa na marafiki.
  Mungu awape faraja katika kipindi hiki kigumu
   
Loading...