Mhariri wa New Habari, Danny Mwakitereko apata ajali Dar

Mongoiwe

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
524
263
Naibu Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New habari (2006) Danny Mwakitereko amepata ajali ya gari jana usiku, jijini Dar es Salaam. Amefanyiwa upasuaji wa kichwa, katika Taasisi ya mifupa Muhimbili, sasa yuko ICU Muhimbili.


Taarifa za awali, zinadai kuwa ilikuwa ni usiku aki-drive na bahati mbaya akaingia lori kwa nyuma hadi uvunguni. Inasemekana ameumia zaidi kichwa na leo asubuhi aliingizwa theatre kwa ajili ya upasuaji.


Tetesi zinadai kuwa huenda ajali ya Mhariri huyo inatokana na TAARIFA iliyoandikwa katika gazeti la Mwanahalisi juu ya MAHOJIANO baina ya Nape na Bashe kuwa Kikwete naye ni Gamba.
 
http://www.blogger.com/share-post.g...894691&postID=4029483274738744333&target=buzz

[h=1]Naibu Mhariri wa Kampuni ya New Habari(2006) Ltd, Danny Mwakiteleko Bado Yupo ICU[/h]



Gari ya Dany Mwakiteleko iliyopata ajali.


Mhariri wa Gazeti la Rai,ambaye pia ni Naibu Mhariri wa Kampuni ya New Habari(2006) Ltd,Danny Mwakiteleko(Pichani)akiwa amelazwa katika wodi ya wagonjwa mahututi ICU cha hispotali ya Taifa ya Muhimbili jana baada ya kuapata ajali juzi usiku wakati akirudi nyumbani kwake maeneo ya Tabata Jijini Dar es Salaam na kusababisha majeraha na maumivu katika sehemu ya kichwani.
 
Naibu Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New habari (2006) Danny Mwakitereko amepata ajali ya gari jana usiku, jijini Dar es Salaam. Amefanyiwa upasuaji wa kichwa, katika Taasisi ya mifupa Muhimbili, sasa yuko ICU Muhimbili. Taarifa za awali, zinadai kuwa ilikuwa ni usiku aki-drive na bahati mbaya akaingia lori kwa nyuma hadi uvunguni. Inasemekana ameumia zaidi kichwa na leo asubuhi aliingizwa theatre kwa ajili ya upasuaji. Tetesi zinadai kuwa huenda ajali ya Mhariri huyo inatokana na TAARIFA iliyoandikwa katika gazeti la Mwanahalisi juu ya MAHOJIANO baina ya Nape na Bashe kuwa Kikwete naye ni Gamba.
Sasa unahusaisha vipi ajali hii na taarifa hiyo, maana kama aligonga lori kwa nyuma na alikuwa akiendesha mwenyewe sio rahisi kukawa na external influence, unless alilogwa ili agonge lori
 
Pole sana kwani ajali ilikuwa mbaya sana. Ni bahati tu kuwa bado yupo hai.
 
RIP Danny, but ninashangazwa na mleta habari kusema eti habari aliyoandika kuhusu mahojiano ya Nape and Bashe ndo imesababisha. Sasa kama gari alikuwa anaendesha mwenyewe na akaingia nyuma ya lori, then hiyo habari ilihusikaje hapo? Labda mtuambie kuna ushirikina hapo! Na mseme pia mshirikina hapo ni nani?
 
Danny amefariki leo asubuhi na msiba uko nymbani kwake Tabata, kwahiyo tumuombee mwenyezi mungu aipumzishe roho yake mahali pema peponi, Amen
 
Mungu aiweke roho yake mahali pema..... Baadhi ya waandishi ndio wanafanya nchi yetu iendelee kuwa nchi kwa kufichua maovu lazima tueshimu kazi zao na kuwaenzi...na wala si wanasiasa wanaoingia majukwaani na kuiba..... RIP Danny.
 
Sasa unahusaisha vipi ajali hii na taarifa hiyo, maana kama aligonga lori kwa nyuma na alikuwa akiendesha mwenyewe sio rahisi kukawa na external influence, unless alilogwa ili agonge lori

Lukansola Tema mate chini!!! Kuna kitu kinaitwa umafioso(Umafia),Ni nomaaaa unaweza ukaliingia gari kwa nyuma mwenyewe kwa kutengenezewa ajali,Think Big Bro!!!!
 
Back
Top Bottom