Mhariri wa Mwanahalisi akatwa mapanga

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
613
Kuna habari kwamba watu wasiojulikana wanaodhaniwa kuwa majambazi wamemvamia mhariri na mmiliki wa Mwanahalisi, Saed Kubena na kumkata kwa mapanga. Habari zaidi baadaye
 
oooh, uwiii, i hope hawakuchukua roho yake! Mpe pole sana utakapoenda kumjulia hali.
 
DUH hizi habari zikoje? maana Halisi hua anakuja na data za mashaka...VP halisi ile kesi yako na TRA kule ARUSHA imeisha maana nshasahau kabisa,...
 
mungu amlaze mahala pema peponi

bwana alitoa na bwana ametwaa

Mmmmmh Mtu Pwani ndio Lugha gani tena hiyo!!.Huyu Bwana Mzima mbona unaandika Lugha Ngumu,ina maana una Taarifa Tofauti na hii aloandika Bwana Halisi?Waungwana hatupo hivyo Mkuu umetoka Mrima nini?
 
Mmmmmh Mtu Pwani ndio Lugha gani tena hiyo!!.Huyu Bwana Mzima mbona unaandika Lugha Ngumu,ina maana una Taarifa Tofauti na hii aloandika Bwana Halisi?Waungwana hatupo hivyo Mkuu umetoka Mrima nini?

alaaa mkuu kumbe nimeelew vibaya kipengele sio, samahanini kwa uelewa mnayaufu.

ila sitoki mrima mkuu mie nnatoka kule kwenye kisiwa cha viungo.

kama yuko hai nnampa pole mungu amjaalie uzima wa haraka ili atuhabarishe
 
DUH hizi habari zikoje? maana Halisi hua anakuja na data za mashaka...VP halisi ile kesi yako na TRA kule ARUSHA imeisha maana nshasahau kabisa,...

Anayekuja na data za mashaka(controversial) nadhani ni Hasara. Namwiminia sana Halisi(Genuine).

Pole bwana mhariri. Wish you quick recovery.
 
mungu amlaze mahala pema peponi

bwana alitoa na bwana ametwaa

Hii Kali kweli, Mtu wa Pwani!! unamtanguliza mwenzako kwenye hukumu ya mwenyezi Mungu kirahisi hivyo? ama unataka kutuambia unafahamu ama ulishiriki kuchapa mapanga na unauhakika hata pona? pole pole mkuu
 
DUH hizi habari zikoje? maana Halisi hua anakuja na data za mashaka...VP halisi ile kesi yako na TRA kule ARUSHA imeisha maana nshasahau kabisa,...

Chuma,

Angalia facts zako maana Halisi ni katika watu wachache sana hapa JF ambao wakisema jambo jua kuna 99% kwamba kuna ukweli.

Pole kwa aliyeumia na mungu amsaidie ili apate nafuu.
 
Pole aliye uliye umizwa mungu akujalie kupona haraka,

Ila wasi wasi wangu, ni ujambazi tu wakawaida?? ama inahusiana na cheo chako cha kuwa mhariri wa gazeti la mwana Halisi, ambalo ni kati ya magezeti yanayo ongoza kwa kuita a spade...
 
Namtakia Mhariri kupona mapema.

Nani kafanya ujambazi huu? Huu ni ujambazi au njama za kuyafunga mdomo magazeti?

Sikujua watu wa Mrima ndiyo hawajui Kiswahili, nilifikiri watu wa Mrima wanajua kiswahili mpaka kuwa na lahaja yao ya Kiswahili Mrima kama ilivyo kwa Kiswahili Unguja.
 
Sasa wale mafisadi baada ya kugundua kwamba wameshindwa kwenda Mahakamani na huenda kuna mambo yatazuka yameamua kampeni ya kuwaondoa wale wote walio chapisha majina yao. OK zile za Kenya sasa zinakuja Tanzania na mtaishia kusema majambazi siyo ???
 
Taarifa rasmi ni kwamba watu watatu wasiojulikana wamevamia ofisi za Mwanahalisi zilizopo Kinondoni, Dar es Salaam na kupambana na Mshauri wa gazeti hilo, Ndimara Tegambwage na baadaye Saed Kubenea, ambaye baada ya kupigwa na kitu kizito kichwani alimwagiwa acid usoni, iliyomwingia mdomoni na machoni.

Ndimara amekatwa mapanga kichwani, shingoni na mgongoni, lakini baada ya kushonwa nyuzi 15 kwa Dr Mvungi kinondoni na baadae yakupaatiwa matibabu zaidi Muhimbili, ameruhusiwa lakini Kubenea amelazwa kutokanan na madhara katika macho yake. Anaona kwa shida na tumuombee Mungu aweze kuona na kuendelea na majukumu yake magumu.
 
Halisi,
Thanks Mkuu- we all wish them quick recovery- yaonekana kuna ill motives associated na vitendo vya ufisadi kutoka ktk hilo gazeti ambalo ndo limeanza tu siku za karibuni!

Muhimu ni kutokata tamaa- na kutambua hii ni vita of social, economic and political justice of our future Tanzania!

Aluta continue!
 
Ni wakina mvi hao (an educated hunch), this might signal the beginning of the end of mafisadi hao. Mwanahalisi ndio wako mstari wa mbele kabisa kuanika uchafu wao. Pole sana waioathirika. Itabidi waondoe mamilioni ya watu kabla ya kudhani siri zao hazitafichuka wale.
 
Kuna habari kwamba watu wasiojulikana wanaodhaniwa kuwa majambazi wamemvamia mhariri na mmiliki wa Mwanahalisi, Saed Kubena na kumkata kwa mapanga. Habari zaidi baadaye

huyu naye alikuwa hasikii alishapelekewa taarifa zamani lakini wapiiii yuko ka Benazir Bhutto vilee
 
Mm sishangai. Maana wameongoza kuwashambulia wakubwa. Sasa mnafikiri hao majambazi wametumwa na kuna motive za kisiasa katika mashambulizi hayo. Wakati wanawashambulia hawakusema chochote? Jamani Tz ndiyo twaelekea nchi jirani? Hiyo sio dawa. Unafikiri mbele ya kamati ya bunge ya Mwakyembe juu ya Richmond si mambo yatawekwa wazi? Sio hayo kaeni mkao wa matazamio siku chache zijazo kuna mambo yataibuliwa kutoka Manispaa mmojawapo za mkoa wa Mwanza au Dar ambayo wengi mtashangaa mtakapoona vigogo wanashinikizwa kuachia ngazi. Sisemi mengi
 
Masikini rafiki yangu Kubenea!!!!

Kulikoni jamani kafanya nini tena, bahati mbaya gazeti lake haliko online, mkipata sababu tujulisheni: who is behind the move...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom