Mhariri wa HabariLeo ndani ya midomo la vyombo vya habari vya kiislam leo hii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mhariri wa HabariLeo ndani ya midomo la vyombo vya habari vya kiislam leo hii

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by thatha, Mar 28, 2012.

 1. t

  thatha JF-Expert Member

  #1
  Mar 28, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Baada ya tahariri ya leo ya gazeti la serekali la habari leo kuchapishwa. viongozi na vyombo vya habari vya kiislam vimekuja juu.
  Leo asibuhi karibu ya vyombo vyote vya habari vya kiislam vimelaani thariri hiyo.
  Katika tahariri hiyo eti inadai vyombo vya madhehebu ya kiislam vinaleta uchochezi kwa kuwasema vibaya viongozi wa CCM kwenye vipindi vyao.
   
 2. J

  JacksonMichael JF-Expert Member

  #2
  Mar 28, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 339
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari nusu nusu hatari sana, ila anyway ndo TZ hiyo kila mtu katibu mwenezi.
   
 3. salito

  salito JF-Expert Member

  #3
  Mar 28, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,365
  Likes Received: 352
  Trophy Points: 180
  mhhh niliona humu jf watu wanaita magamba,nadhani ndio mambo yao haya...
   
 4. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #4
  Mar 28, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145  [TABLE="width: 99%, align: left"]
  [TR]
  [TD="class: kaziBody, align: left"]BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) Wilaya ya Dodoma Mjini limehadharisha na kuvitaka vyombo vya habari kuepuka kutumiwa kuchochea vurugu na kukashifu viongozi wa Serikali.

  Badala yake Bakwata kupitia kwa Katibu wa Baraza hilo wa Wilaya, Mussa Kazimiri, imevitaka vyombo hivyo kuacha kufanya uchochezi na vitumike kuelimisha jamii kuhusu masuala ya
  maendeleo na kupambana na umasikini.

  Katika kuthibitisha alichokuwa akikisema, Kazimiri alifikia hatua ya kusema kuna redio ya madhehebu ya Kiislamu ambayo inafanya kazi nzuri ya kuelimisha jamii kuhusu masuala mbalimbali muhimu.

  Lakini hata hivyo redio hiyo imekuwa ikitumia baadhi ya wahadhiri wa chuo kikuu ambacho hakukitaja, kuzungumza kauli ambazo zina kila dalili ya kukashifu viongozi wa kitaifa, jambo
  ambalo si la staha bali ni la uchochezi.

  Tunapenda kuipongeza Bakwata kwa msimamo wake huo ambao unalenga kudumisha amani, utulivu na upendo miongoni mwa jamii, lakini pia kuikumbusha jamii na wanahabari, kwamba
  habari na kauli mbaya vinaweza kusababisha machafuko kwa jamii.

  Mauaji ya kimbari yaliyotokea Rwanda mwaka 1994 na kusababisha kupotea kwa roho za watu takriban milioni moja, kwa sehemu fulani yalichochewa na habari zilizotolewa na wanahabari
  kupitia vyombo vyao zikichochea mauaji.

  Ni kweli kwamba vipo vyombo vya habari nchini ambavyo badala ya kuzingatia dhima zao kuu za kuwapo kwao yaani kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha, vimekuwa vikitumika
  kuchochea chuki na hasira miongoni mwa jamii na kuhatarisha usalama.

  Mbaya zaidi kama alivyosema Kazimiri, vipo vyombo ambavyo vinatumia wahadhiri ambao wana elimu na utambuzi mkubwa wa mambo, kuchochea hasira na chuki kwa jamii; ilhali
  wakijua kuwa wanaaminika katika kauli zao.

  Ni dhahiri, kwamba Bakwata ina dhamira ya dhati ya kukemea tabia hiyo hatari kwani isingekuwa hivyo isingeweza wala kuthubutu kutaja kituo cha redio kinachomilikiwa na Waislamu na kukituhumu kwa mwenendo wake huo mbaya.

  Watanzania tunapaswa kutambua kuwa nchi hii ni yetu sote na kama itachafuka kutokana na habari zinazoandikwa na kutangazwa na vyombo vya habari, bila shaka lamawa zitatuangukia
  sisi wenyewe.

  Kuwapo kwa dini tofauti, itikadi tofauti za kisiasa na utamaduni tofauti, si tiketi ya watu kutofautiana kibinadamu na kuchukiana hata kusababisha machafuko nchini kwa sababu tu
  gazeti, redio au televisheni fulani imetangaza kichochezi.

  Tuendelee kudumisha amani na utulivu, upendo na mshikamano, na tuendelee kukemea vyombo vya habari vinavyotaka kutugawa, kutuchochea na kutupiganisha na hatimaye tukose wa kumlilia kwa ujinga wetu wenyewe.

  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: Text, align: left"] [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 5. t

  thatha JF-Expert Member

  #5
  Mar 28, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160

  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: Text, align: left"]kwanini habarileo hawailani WAPO IFM AU NDIO AU DINI MOJA NA MUHARIRI[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/QUOTE]
   
 6. A

  Anold JF-Expert Member

  #6
  Mar 28, 2012
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,378
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 180
  Huwa hawakosolewi hao!!!!! ila nafikiri huyo mhariri inafaa apewe tuzo!! la kusema ukweli usiotakiwa!!!!
   
 7. mpemba mbishi

  mpemba mbishi JF-Expert Member

  #7
  Mar 28, 2012
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 1,132
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mwandishi wenyewe hakujiamini wakati alipoandika tahriri yake!!! Fuatilia habari usiwe kasuku wewe!
   
 8. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #8
  Mar 28, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,197
  Likes Received: 1,003
  Trophy Points: 280
  Uchochezi unaofanywa na hichi kituo ni mwendelezo wa chuki za kidini/kisiasa zilizoasisiwa na serikali ya ccm wakati wa campaign za mwaka 2010. Wamelegeza mashambulizi kwa mahasimu wa waliowatengeneza na kuyapeleka kwa hao waasisi wao. Hii itakuwa ni mbinu ya kutaka pesa waliyokuwa wakilipwa kwa uchochezi wao iendelee kulipwa maana inaonekana neither imepunguzwa nor imekatwa kabisa.
  .
   
 9. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #9
  Mar 28, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  nakufahamu sana ww ni ant xstians
  wapo ni redio binafsi naiheshimu sana
  haikashifu dini ya mtu bali wanamtangaza kristo na mahubiri
  vipindi vyao ni vya kuelimisha na kujenga na sio majungu kila kukicha kama radio zenu hizo wenye watangazaji vilaza
  wasiojua nini maana ya utangazaji
  [/QUOTE]
   
Loading...