Mhariri Tanzania daima kanunuliwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mhariri Tanzania daima kanunuliwa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gulwa, Mar 24, 2009.

 1. G

  Gulwa JF-Expert Member

  #1
  Mar 24, 2009
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 2,786
  Likes Received: 1,963
  Trophy Points: 280
  Kwa mtu anayefuatilia uandishi na maoni ya mhariri wa Tanzania Daima utagundua kubadirika kwa kiasi kikubwa. Kwa siku za karibuni amejitokeza kuwa mtetezi mkubwa wa Dowans na RA. Nahisi alichopewa Zitto Kabwe ndicho alichoonjeshwa muhariri huyu. Sasa nimeamini hakuna kinachoweza kuishinda nguvu ya pesa. Mungu ibariki Tanzania
   
 2. J

  Jobo JF-Expert Member

  #2
  Mar 24, 2009
  Joined: May 15, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kwani tatizo la kununua mitambo ya Dowans liko wapi? Tusiwe brainwashed na "happy go luck" people kama akina Mwakyembe na Sitta! Hivi unaweza kuamini kwmba mitambo ya Dowans ambayo ina miaka mitatu imechakaa kuliko mitambo ya IPTL? Au leo watanzania tumesahau machungu ambayo tunayapata kwa ajili ya mkataba mbovu wa IPTL? Eti wanasema hizi kampuni mbili haziwezi kulinganishwa! lame excuses, wanajaribu kuexpolit ujinga wa Watanzania ambao hupokea taarifa bila kuchekecha! Hatusemi kuwa Dowans ni clean company, but tujiulize Dowans imeingiaje katika sakata la ufisadi wa Tanzania. Kama si Dowans, umeme uliokuwa uzalishwe na Richmond usingekaa upatikane. Mhariri amejifuta matongotongo na kuamua kueleza what I think is the best opinion kulinganisha na blaablaa za watu kama Mwakyembe, Sitta na Shelukindo!
   
 3. T

  Thuraya Member

  #3
  Mar 24, 2009
  Joined: Mar 24, 2009
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tusimhukumu mhariri kuwa kanunuliwa kwa sababu ya Dowans!Tanzania Daima ni miongoni mwa magazeti makini ambayo yamefanya kazi nzuri ku kuupasha umma habari sahihi katika mambo mbalimbali.Inawezekana ni maoni yake kama yalivyo maoni ya akina Zito,Mwakyembe n.k
   
 4. M

  Mkodoleaji JF-Expert Member

  #4
  Mar 24, 2009
  Joined: Apr 27, 2008
  Messages: 454
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mungu ibariki Tanzania na watu wake. Maana siku hizi kila ukitofautiana na wale waliojibatiza majina kwamba wapinga ufisadi basi wewe aidha umenunulia au unakula na mafisadi. Kweli vita ya ufisadi ni kitovu cha uzembe wa kufikiri. Sasa sijui nani anafaidi huo uzembe wetu wa kufikiri mafisadi au wanajipachika upambanaji wa ufisadi? Ninavyoona wote wanaangalia 2010 wapite kimchekea (mafisadi wakitumia pesa kuhonga na wale waliojibatiza kwa kisingizio kuwa walipambana na ufisadi)
   
 5. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #5
  Mar 24, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 240
  Trophy Points: 160
  Kweli tumetofautiana kimawazo. Yaani hii yote ni kumtafuta Zitto tu. Mnasahu 1000 aliyoisaidia kuionyesha njia ya mfisadi hii nchi, mnakuja na vi-ishu visivyo vya msingi. Anyway kila mtu ana exercise right ya maoni yake.
   
 6. Sabode

  Sabode Senior Member

  #6
  Mar 24, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 159
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Heshima mbele.
  Mzee ikiwa kuna ukweli kuwa Dowans imeweka hiyo mitambo kama dhamana kwa mikopo ilyo pata katika mabenki! Hiv kweli ni sawa kuinunua???
  Hii kwangu sioni kama sawa hata kidogo na nashangaa sana watu ambao kila lina pofika suala hili kulifanya vita kati ya Dr na RA. Hebu lets imagine hawa hawapo ktk sakata hii tuiangalie mitambo pekeyeke labda kwa njia hii tuna weza pata suluhu ikiwa inafaa au laa. Hayo ni mawazo yangu hebu naomba na wengine tuliangalie kwa kona hiyo .
   
 7. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #7
  Mar 24, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Jobo,i think 'YOU ARE THE BRAINWASHED TANZANIAN'...........and you really are!sorry
   
 8. G

  Gulwa JF-Expert Member

  #8
  Mar 24, 2009
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 2,786
  Likes Received: 1,963
  Trophy Points: 280
  Nawaomba wazalendo wenzangu tusirudi nyuma katika mapambano haya japo mafisadi wanazidi kujizolea wapambe ( waliolambishwa ) humu JF. Jana tumeambiwa jinsi Dowans inavyohusiana na pesa zilizowaweka viongozi wetu madarakani 2005. Ufisadi ni zaidi ya ugonjwa wa TB kwa taifa letu hivyo kitu chochote chenye harufu ya ufisadi, lazima tukikimbie na kukikataa kabisa. Lakini hilo lingewezekana tu kama tungekuwa na viongozi waadilifu kama alivyokuwa marehemu Mwanawasa
   
 9. J

  Jobo JF-Expert Member

  #9
  Mar 24, 2009
  Joined: May 15, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Sabode, kama Tanzania ingeamua kununua hii mitambo, isingefanya hivyo kwa siri! Kwani ukiweka nyumba yako rehani, huwezi kuiuza? Kwani huyo anayewadai asingejua kuhusu kununuliwa kwa mitambo ili hela ikitoka akate hela yake!
   
 10. J

  Jobo JF-Expert Member

  #10
  Mar 24, 2009
  Joined: May 15, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  It is your opinion and I do not have to dispute it! I always weigh my words and do not jump into conclusions I cannot scientifically prove, sorry!
   
 11. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #11
  Mar 24, 2009
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Kama Tanzania Daima imenunuliwa au haijanunuliwa haijathibitishwa. Lakini kilicho na uhakika ni kuwa wana policy ya kukubaliana na uongozi wa CHADEMA. Usisahau zito ni deputy secretary general wa CHADEMA. Hivyo Tanzania Daima kuchukua msimamo tofauti na Zitto itakuwa kujenga mipasuko ndani ya Kambi. Hawako pro-RA or Dowans, ila wako pro Zitto na hili halihitaji uthibitisho wowote.
   
 12. Kandambilimbili

  Kandambilimbili R I P

  #12
  Mar 24, 2009
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 782
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  KILA mtu ana uhuru wa kutoa maoni yake WEWE GULWA umenunuliwa na nani???????
   
 13. K

  Kokolo JF-Expert Member

  #13
  Mar 24, 2009
  Joined: Mar 20, 2008
  Messages: 487
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 45
  Wewe Jobo, unaponunua Jaba(Used car) toka Japani ikifika Tanzania baada ya miaka 3 utasema hii gari ilikuwa mpya na ina miaka 3 tu.
  Hii mitambo ya Dowan ina zaidi ya miaka 20 kasoro mmoja LM6000 (50MW), ambao una miaka 7 toka utengenezwe mwingine LM6000 na LP2500 zina zaidi ya miaka 20. Kama unabisha nenda hapo kawaulize. IPTL ni yale yale Mkapa/chenge na wapambe wake inabidi wawe jela kwa kuliangamiza Taifa kwa mikataba mibovu. Life span ya hii mitambo ni kati ya miaka 25- 30, hivyo kama tutanunua mpya wa 100MW kwa $35million plus additional cost ambayo jumla itafika $50million tutakaa nao kwa miaka 30.
   
 14. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #14
  Mar 24, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145

  yaani hili suala linataka kuwafanya watu wasiwe na uhuru wa mawazo... kama angekuwa ule upande mwingine, nako angekuwa amenunuliwa?
   
 15. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #15
  Mar 24, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  "Kwani tatizo la kununua mitambo ya Dowans liko wapi? Tusiwe brainwashed na "happy go luck" people kama akina Mwakyembe na Sitta! Hivi unaweza kuamini kwmba mitambo ya Dowans ambayo ina miaka mitatu imechakaa kuliko mitambo ya IPTL? Au leo watanzania tumesahau machungu ambayo tunayapata kwa ajili ya mkataba mbovu wa IPTL?........"

  **************************

  JOBO:

  1. Hata mimi naamini mhariri huyo kanunuliwa -- na hii si siri hasa miongoni mwa waandishi wa habari -- kama nilivyodokezwa. Na si kwa Dowans tu, ni katika kila kashfa za ufisadi -- Kagoda, Vitambulisho na nyinginezo. Stori nyingi za T. Daima Jumapili -- zile za analysis -- huwa zinajaribu kuosha ufisadi, (katika mada iliyopo wakati huo) kwa njia za kujanjaujanja. Ningekuwa Mbowe (ambaye anasadikiwa kuwa mmiliki wa magazeti hayo) ningemwondoa -- na mara moja utaona ataajiriwa ktk magazeti ya RA. Kuendelea kwake (Mbowe) kupiga kelele dhidi ya ufisadi katika majukwaa ya "Sangara" yanakuwa kichekesho kitupu iwapo anaachia magazeti yake kumpiga vita kwa mlango wa nyuma.

  2. Jobo kaleta tena issue ya ulinganisho kati ya IPTL na Dowans. Hii ilishazungumzwa kwa kirefu katika thread nyingine na kwa mtazamo wa wengi waliochangia vitu hivi viwili ni tofauti kabisa. Atafute na azirejee thread hizo.
   
 16. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #16
  Mar 25, 2009
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Two wrongs do not make a right.Blunders za IPTL zisitumike kuhalalisha ujambazi wa Dowans.

  As to Absalom Kibanda (Mhariri wa TZ Daima) naafikiana 105% na mtoa hoja kwamba mwelekeo wake na gazeti hilo kwa ujumla ni kana kwamba wameshanunuliwa....I couldnt believe my eyes nilipoona mahala flani wakitumia kauli ya moja kwa moja kwamba Dr Mwakyembe analeta ubaguzi wa rangi.....

  Ndo tunaeleka 2010,msimu wa wanahabari kula kwa kutumia kalamu zao.
   
 17. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #17
  Mar 25, 2009
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  tuone mwisho wa haya.
   
 18. J

  Jobo JF-Expert Member

  #18
  Mar 25, 2009
  Joined: May 15, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mlalahoi, kwanini tunaconclude kuwa kanunuliwa? why cant we say that he has a different opinion from the "majority"? I for one, do not believe anything Mwakyembe says in this saga especially after it was revealed that he is also fighting to enrich himself in the power generating business. Absalom anaweza kuwa naye amegundua hadaa ya Sitta na Mwakyembe na kwa kung'amua kuwa hawa watu hawana nia njema basi akaamua kusema aichosema.

  Hivi tunataka tuseme kuwa TANESCO hawana utaalamu wa kugundua mitambo mizuri na mibovu? Kama wao wameona kuwa mitambo ya Dowans ni suruhisho la muda la matatizo ya umeme, kwanini sisi ambao hatuna utaalamu wowote katika eneo hilo tunasema kuwa wamenunuliwa!! Mwakyembe na Sitta ni wanasheria! Shelukindo hana utaalamu wowote wa umeme na hawajasema ni wapi wametoa hiyo thesis kuwa mitambo ya DOWANS haiwezi kuzalisha umeme tunaohitaji kwa muda huu. Na tusisahau kuwa mitambo ya DOWANS ingenunuliwa ingekuwa kwa ajili ya "emergencies" na sasa giza tumeanza kuliona.
   
 19. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #19
  Mar 25, 2009
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,499
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Mitambo ya Dowans ina miaka mitatu tangu iletwe TZ na si tangu ianze kutumika. Ilitumika kwa zaidi ya miaka 10 huko ilikotoka kabla ya kuletwa TZ. Ilikarabatiwa na kupigwa rangi tu. Unajua bei ya umeme ambayo Tanesco hulipa kampuni binafsi, hutegemea kiasi kilichowekezwa. Aliyewekeza zaidi hulipwa bei ya juu. Hivyo kampuni iki-inflate bei ya mitambo na hivyo ku-inflate gharama halisi za uwekezaji, hudai bei ya juu kuliko hali halisi. Na hii ndiyo inayosababisha bei ya umeme TZ kuwa juu sana, Hiki cha juu ndicho wakubwa wanagawana. Milipaji halisi ni mtumiaji wa umeme na mtumiaji wa bidhaa zinazozalishwa kwa kutumia umeme huo.
  Tatizo lingine la mitambo hiyo ni kuwa bei wanayotaka kununulia ni kubwa mno kuliko hata kununua mitambo mipya kabisa. Maana yake ni kwamba kuna cha juu hapa wakubwa wanataka kugawana kwa kisingizio cha dharura. Noungana na wale wanaotaka Dk. Idriss ajiuzulu maana baada ya kutangaza kuwa Tanesco imeachana na mipango ya kununua mitambo ya dowans na kutaka shirika lisilaumiwe ikiwa taifa litaingia gizani, hakuna juhudi zozote anazofanya kuanza mchakato wa kuagiza mitambo mipya. Amekaa nasubiri taifa liingie gizani halafu aseme, si niliwaambia?
  Taifa haliatingia gizani bali lintaingizwa kimaksudi gizani. Sasa hivi tayari giza limeanza wakati mabwawa yamejaa maji! Huu si mchezo wa kitoto? Hapa ndipo tunasema 'mtu mzima ovyo'
   
 20. J

  Jennifer New Member

  #20
  Mar 25, 2009
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ukisoma mtanzania ya leo utashangaa sana, inamshambulian dr mwakyembe na kumuwekea maneneo mdomoni, hali wakijua kuwa hata slaa ambaye nikatibu mkuu wa chadema alishasema kuwa mwakyembe hana maslahi na wala halazimiki kutangaza maslahi ambayo hana
   
Loading...