Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Mhariri wa gazeti la Dira ya Mtanznia, Musa Mukama na mwandishi wake William Kapawaga, na meneja wa gazeti hilo Abiudi Mangera, wamekamatwa na Polisi muda huu na wanapelekwa Kanda Maalum ya Polisi.
Waliofika kuwakamata na wakajitambulisha ni mkuu wa Upelelezi(OCD) kutoka kituo cha Msimbazi, na mkuu wa kituo(OCS) wa Oysterbay. Walifika na gari binafsi na wamewachukua tayari.
Waliofika kuwakamata na wakajitambulisha ni mkuu wa Upelelezi(OCD) kutoka kituo cha Msimbazi, na mkuu wa kituo(OCS) wa Oysterbay. Walifika na gari binafsi na wamewachukua tayari.
Mhariri wa Gazeti la Dira (lililoandika kuibiwa kifaru Jeshini) Musa Mkama, amekamatwa na Polisi na kupelekwa Kituo Kikuu cha Kati, Dar.
Gazeti la Dira wanadai kuwa, habari waliyoiandika imetokea mahakamani ilipokuwa ikisikilizwa kama kesi.
Leo gazeti la dira lilitoa habari kwamba wananchi 20 Kijiji cha Tondoroni Wilayani Kisarawe, huko Pwani, wamepandishwa kizimbani kwa kosa la kuiba Kifaru cha JWTZ katika kikosi 83 KJ Kiluvya na kukipeleka kukihifadhi kijijini kwao.
Habari hiyo imesambaa sana Kiasi kwamba JWTZ Tanzania wanetoa kanusho kuhusiana na habari hiyo wakisema sio kweli.