Mhariri Mtanzania: Kwa siasa za shari, CHADEMA kinajifuta; marehemu alikuwa akiifanyia kazi CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mhariri Mtanzania: Kwa siasa za shari, CHADEMA kinajifuta; marehemu alikuwa akiifanyia kazi CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Sep 17, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 17, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  JUMAPILI, SEPTEMBA 16, 2012 08:05 NA YUSUF HALIMOJA, DAR ES SALAAM

  HAPANA shaka wasomaji wa gazeti la Mtanzania Jumapili watakumbuka kwamba Jumapili iliyopita niliandika makala iliyosomeka "CHADEMA na ndoto ya nchi isiyotawalika."

  Baada ya hapo waandishi wawili wa kampuni inayochapisha gazeti hili walipokea simu kutoka kwa vijana wanaoaminiwa kuwa ni wanachama wa Chadema. Katika simu yao vijana hao walidai kuwa kama wangejua napatikana wapi wangenifuata wanipige kofi! Sababu? Naichafua Chadema!

  Hakuna asiyejua kuwa Chadema ni chama kinachotaka kipewe sifa nzuri wakati wote hata inapofanya vibaya. Nichukue nafasi hii kuwahakikishia vijana wa Chadema kwamba hawawezi kunitisha kwa sababu hata viongozi wao, Mbowe na Slaa, hawakufanikiwa kunitisha.

  Ni kweli walijitahidi kunitia mfukoni kama walivyowatia mfukoni watumishi wengine wa Chadema, kwangu walikwama. Maana huwezi kufanya kazi Chadema kwa furaha kama hukubali kutiwa mfukoni na viongozi wa chama hicho.

  Kwa hiyo nawataka vijana wa Chadema na mashabiki wa chama hicho wafahamu kuwa naiandama Chadema kwa sababu naijua vizuri kuliko wanavyojua wao. Chadema si chama cha kushabikia.

  Niwaarifu tu vijana wa Chadema kwamba nilikuwa mtumishi wa Chadema miezi sita Makao Makuu ya Chadema. Sikuwahi kuomba kazi yoyote ya Chadema lakini ni viongozi wenyewe wa Chadema walionitafuta. Moja kwa moja nikaajiriwa kuwa mkufunzi wa mafunzo ya siasa.

  Binafsi wakati wote sikukubaliana na uongozi wa kidikteta wa Mbowe na Slaa. Kwa mfano, watumishi wote wa chama Makao Makuu tulitarajiwa tusishirikiane na Chacha Wangwe. Lakini nilishirikiana na Chacha Wangwe kwa wazi.

  Na watumishi wote wa Makao Makuu ya Chadema wanajua kuwa nilichangia kwa kiasi kikubwa ushindi wa Chacha Wangwe katika uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti. Mbowe na Slaa hawakumtaka Chacha Wangwe. Lakini mimi nilimtaka. Nikawashinda. Wakati wangu demokrasia ilishinda udikteta.

  Kama ninachosema ni uzushi basi wanachama na mashabiki wa Chadema nchini kote wasubiri kuona kuwa Mbowe na Slaa watakanusha nilichosema. Chadema nilikuwa kiboko cha Mbowe na Slaa. Nilipambana na udikteta wao bila kuchoka. Wenyewe ni mashahidi.

  Chadema kinaendeshwa kwa matakwa ya Mbowe na Slaa na wala si kwa matakwa ya Kamati Kuu ya Chadema au Baraza Kuu. Wanachoamua Mbowe na Slaa lazima kitakuwa. Chadema ni watu wawili: Mbowe na Slaa. Hii ni kusema kwamba watu hawa wawili wakipewa nchi wataiendesha kwa matakwa yao. Si kwa matakwa ya wananchi. Mashabiki wa Chadema wajue hivyo na Watanzania wajue hivyo.

  Kwa vyovyote mwasisi wa Chadema, Edwin Mtei, alitaka chama kiendeshwe kidemokrasia. Kinyume chake kinaendeshwa kidikteta. Matakwa ya Mbowe na Slaa yamegeuzwa kuwa matakwa ya chama.

  Binafsi siamini kwamba wanachama wa Chadema – wenye akili timamu wanataka chama chao kiendeshwe kwa shari. Ukombozi wa Watanzania unaodaiwa kushughulikiwa na Chadema hautaletwa na siasa za shari.

  Viongozi wa Chadema hawawezi kutuaminisha kuwa utawala wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ni mbaya zaidi kuliko ulivyokuwa utawala wa Mwingereza hata wapambane na CCM na serikali yake kwa shari.

  Rais wa TANU, Mwalimu Nyerere aliona mbali. Akajua kuwa TANU isingeweza kukomboa Tanganyika kwa siasa za shari. Kwa hiyo Nyerere alihubiri kutafuta ukombozi kwa kutumia silaha ya umoja na amani. Mbowe na Slaa wanahubiri kutafuta ukombozi wa Tanzania kwa kutumia silaha ya umoja na shari.

  Kwa hiyo watu wenye akili timamu wanajiweka kando. Wanajua kuwa Mbowe na Slaa wanaipeleka nchi pabaya. Yote hayo ni matokeo ya tamaa ya kuingia Ikulu. Basi wakati TANU haikumwaga damu katika ukombozi wa Tanganyika Chadema inamwaga damu katika ‘ukombozi wa Tanzania'.

  Katika makala yangu ya Jumapili iliyopita niliandika kwamba Chadema isifanye mambo kama vile tayari ni serikali. Isikae hapa kuwaamuru viongozi wa polisi na wa serikali kwa jumla watimize matakwa ya Chadema. Eti bila hivyo nchi itashika moto!

  Chadema siyo serikali ya pili ya Tanzania Chadema ni chama tu cha siasa ambacho tunakishuhudia kikijifuta chenyewe kutokana na siasa zake za shari.

  Wasichojua viongozi wa Chadema ni kwamba Watanzania ni wapenda amani. Ndiyo maana nchi yao ikaitwa "Kisiwa cha amani".

  Lakini kwa sababu wanafundisha vijana wao wachangamkie siasa za shari na wanachangamkia basi viongozi wa Chadema wanaona kwamba siasa za shari ndizo zinazotakiwa na Watanzania. Si kweli. Watanzania wanataka siasa za amani.

  Hakuna anayekataa madai kwamba polisi wamehusika na mauaji katika maandamano ya Chadema sehemu mbalimbali za nchi hii. Lakini lazima tuseme kweli bila kumwogopa mtu yeyote wa Chadema. Hayo yote yamekuwa matokeo ya siasa za shari zinazoendeshwa na Chadema.

  Ni kweli maandamano ni haki mojawapo ya raia wa Tanzania. Lakini maandamano yasiendeshwe kwa shari kwa sababu tu kila mtu ana haki ya kufanya maandamano. Polisi wakiwa na sababu ya msingi ya kukataza maandamano basi busara itumike. Mbowe na Slaa wasing'ang'anie maandamano kwa lengo tu la kutimiza siasa zao za shari. Hakuna Rais wa Tanzania aliyekwenda Ikulu kwa shari.

  Kwa jumla wapenda amani wa Tanzania wameshangazwa kusikia kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, anabanwa eti kwa kutamka kwamba anaweza kuifuta Chadema ikiendelea kuendesha siasa za shari. Nani anataka siasa za shari? Chadema kiendelee na siasa za shari lakini kisifutwe? Kivumiliwe tu! Eti hiyo ndiyo demokrasia ya kweli. Ni demokrasia iliyochimbuka nchi gani?

  Ni ukweli usiopingika kwamba karibu mauaji yote yaliyotokea katika maandamano ya Chadema yametokana na ukaidi na uchochezi wa viongozi wa Chadema.

  Cha ajabu na tunachoshuhudia sasa ni kulaumiwa Jeshi la Polisi tu kuhusu mauaji hyo huku watu wa Chadema wakishiriki katika kulaumu bila kuona aibu.

  Hii ni bahati mbaya kwamba watu wanashughulika na matokeo badala ya kushughulika na chanzo. Msajili wa Vyama vya Siasa ni miongoni ma watu wachache wanaoshughulika na chanzo. Chanzo cha vurugu zote na mauaji katika Tanzania yetu ya leo ni tabia ya Chadema ya kukaidi amri ya polisi.

  Mbele ya Chadema uvunjaji wa sheria ndiyo demokrasia. Chukua, kwa mfano, mauaji yaliyotokea Arusha baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

  Baada ya uchaguzi ule Chadema walilazimisha kufanya maandamano kupitia kwenye njia ambazo Jeshi la Polisi liliwazuia kuzitumia. Wao wakazitumia. Na walipotakiwa kuacha maandamano hayo waliendelea na kulilazimisha Jeshi la Polisi kutumia nguvu. Wakafa watu watatu. Waliosababisha vifo hivyo si polisi waliolinda sheria bali ni viongozi wa Chadema walioleta ukaidi. Tuwe wakweli.

  Kule Morogoro siku ya pili tu ya sensa Chadema iliitisha maandamano kinyume cha maagizo ya polisi. Katika vurugu zilizotokea wakati polisi walipoingilia kati maandamano hayo aliuawa Ally Singano. Hayo, tena, yalikuwa matokeo ya Chadema kuleta ukaidi mbele ya Jeshi la Polisi.

  Hata kule Iringa ni Chadema iliyosababisha kifo cha Daudi Mwangosi. Siyo polisi. Ni matokeo mengine ya tabia ya Chadema ya kukaidi amri ya polisi.

  Kwa bahati mbaya katika vurugu zinazosababishwa na Chadema viongozi wa Chadema hawakamatwi. Sasa wananchi wamefika mahali ambako wanaulizana kuna maelewano gani kati ya uongozi wa juu wa polisi na uongozi wa juu wa Chadema? Mbona polisi wanapambana na wanaoshiriki vurugu huku wakiwaacha bila kuwagusa wanaochochea au wanaoongoza vurugu hizo?

  Kinachoonekana hapa ni ukweli kwamba vurugu za Chadema ni kukaidi kwa chama hicho amri ya polisi kunatokana na jeshi hilo kuidekeza Chadema. Hali hiyo ndiyo imefikisha Tanzania mahali pabaya.

  Viongozi wa Chadema ni wanasiasa uchwara. Hawajui siasa. Siasa haiendeshwi kwa mabavu wala kwa shari.

  Tazama! Kule Iringa Slaa alimpigia simu Mkuu wa Jeshi la Polisi akisema, "IGP nasubiri simu yako, wajulishe polisi wako waandae risasi za kutosha na mabomu ya kutosha."

  Huo ulikuwa ujumbe wa Slaa kwa Mkuu wa Polisi nchini katika kuihakikishia polisi kwamba haina ubavu wa kuizuia Chadema kufanya inachotaka. Kwa siasa hizi za shari kwa nini Chadema kisifutwe?

  Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ametangaza tishio la kuitisha maandamano nchi nzima ya kupinga mauaji ya Mwangosi na wananchi wasio na hatia wakati wapenda amani wanajua kuwa mauaji hayo yanasababishwa na Chadema kukaidi amri ya polisi.

  Kwa hivyo maandamano kama hayo yalipaswa yaitishwe na CCM nchi nzima kupinga uvunjifu wa amani unaotokana na ukaidi wa Chadema. Kwa nini CCM isifanye hivyo?

  Mbele ya viongozi wa Chadema kila mtu ni mbaya isipokuwa wao!

  Wanataka Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ajiuzulu. Na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini. Na Mkuu wa Operesheni ya Mafunzo. Na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro. Na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa. Na wananchi waisusie TBC kwa madai kuwa inapendelea CCM! Ipendelee Chadema.

  Halafu imedaiwa Rais Kikwete akishindwa kuwawajibisha viongozi hao basi nchi nzima itaandamana kwa ghafla – maandamano ambayo Mbowe anadai polisi itashindwa kuyazima. Halafu kifuate nini? Uvunjifu wa amani nchi nzima. Kwa manufaa ya nani? Jibu wanalo wasomaji.

  Ukitaka kusema kweli tayari wananchi wa kawaida wamewekwa roho juu. Hawajui kitakachotokea mwaka 2015.

  Tazama! Hali hii mbaya inatokea wakati CCM ipo kimya. Chadema inapambana na serikali. Je, mapambano ya Chadema na CCM yatakuwaje mwaka 2015. Na ndoto ya Chadema ya kuingia Ikulu ikipotea itakuwaje?

  Chadema wanataka tume huru iundwe kuchunguza mauaji mbalimbali nchini yaliyohusisha shughuli za Chadema. Si kitu kibaya. Lakini ni vema tume kama hiyo ikianza kuchunguza kifo cha utata cha Chacha Wangwe ambacho viongozi wa Chadema hawakusikika wakidai kiundiwe tume.

  Mwisho, kwa ndugu zangu wanahabari. Jumapili iliyopita niliandika kwamba ni vema wanahabari wajitazame upya ili mbele ya serikali na umma wasionekane kwamba wao na Chadema ni kitu kimoja au wanaitumika Chadema. Najua wengine hawakunielewa.

  Nitatoa mfano hai.

  Mkuu wa Operesheni ya Chadema inayodaiwa kuwa ni ya Vuguvugu la Mabadiliko, Benson Kigaila amesema kwamba kabla marehemu Mwangosi hajauawa alimwambia Kigaila kuwa alikuwa na wasiwasi juu ya uhalali wa askari waliokuwa katika operesheni ya kuwadhibiti wafuasi wa Chadema.

  "Marehemu mwangosi aliniambia ana shaka na askari waliopo eneo hilo na alikuwa ameniahidi kwamba atanionyesha picha za askari asiowafahamu," amesema Kigaila.

  Baada ya hapo Mwangosi aliwafuata polisi.

  Hapa inaleta picha kwamba marehemu alikuwa akiifanyia kazi Chadema. Na askari walimwona. Kwa hiyo askari mmojawao alipojaribu kumwokoa Mwangosi akisema kwamba anamjua kuwa ni mwandishi wa habari haikusaidia kitu. Polisi wengine walimwona kuwa ni mfuasi wa Chadema chama wanachopambana nacho.

  Jukwaa la Wahariri litafakari hayo.

   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Sep 17, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Ina Maanisha Wahariri wa MTANZANIA hawakushiriki yale Maandamano ya WAANDISHI WA HABARI ?

  Inaonyesha HASIRA zao NI KWA CHADEMA na MWANDISHI ALIYEFARIKI ALIKUWA ANAFANYA KAZI za CHADEMA; Hivi Ndio Maana Mwajiri wake

  CHANNEL 10 NEWS; Walimkataa kuwa si Mwajiri WAO? Ndio Maana POLISI wakamuua sababu walijua kuwa ndie MFANYA-KAZI za CHADEMA?

  Then It was
  PREMEDITATED MURDER...
   
 3. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #3
  Sep 17, 2012
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 315
  Trophy Points: 180
  What a load of rubbish! Does the end justify the means? In the eyes of the convoluted opinion of this excuse for a writer, killing Mwangosi was justified "because he worked for CHADEMA"!

  Kuna watu wanasema magazeti kama Mtanzania yanafaa tu kwa kufungia maandazi. Sasa hiyo ni kukosea haki hayo maandazi: utayafungaje kwa karatasi chafu hivyo?
   
 4. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #4
  Sep 17, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Huo ni kweli usiopingika. Magwanda wanajitahidi kuendelea sera za kijinga za "nchi haitatawalika". Ukweli ni kwamba wao ndiyo hawataitawala hii nchi.
   
 5. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #5
  Sep 17, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,535
  Likes Received: 10,453
  Trophy Points: 280
  huyu mhariri nadhani ni kati ya walio mwalika Nchimbi kupokea maandamano ya wanahabari jangwani matokeo akazomewa. Hivyo ameona ni bora kutoa makala za kuwakandia chadema na wanachama wake kwa ujumla ili kufidia bahasha aliyopewa na ccm.!
   
 6. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #6
  Sep 17, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,568
  Likes Received: 1,935
  Trophy Points: 280
  Kabla sijachangia hapa,ningependa kujuwa kama hili gazeti lina wasomaji wa kutosha bongo,kama linao,nitachangia kuhusu mada iliyoko kwenye bandiko hili.

  Kama sivyo,sitoweza kufanya hivyo,sababu ni kwamba hata mimi kuna magazeti nilikuwa siyasomi kwasababu ya mwelekeo wa kifisadi.Wenye kufahama tafadhali tujulishane.Natanguliza shukran.
   
 7. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #7
  Sep 17, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  hebu soma tena post yako mkuu zomba kama ulimaanisha hivyo,au edit
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #8
  Sep 17, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Nimeona, kweli. nabadilisha.
   
 9. H

  HAMY-D JF-Expert Member

  #9
  Sep 17, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 6,825
  Likes Received: 710
  Trophy Points: 280
  Vyema sana mkuu kwa kutoa taarifa yenye mashiko inayofungamana na ukweli mtupu juu ya undani wa Chama Cha Demokrasia Na Maendeleo na uongozi wake. Binafsi sikuwai kuwa mpenzi wa siasa uchwara zinazoendeshwa na hawa wanaojiita viongozi wa chadema. kama taifa tunahaja ya kuliongelea jambo hili kiubinadamu sasa maana hakuna mtu yeyote aliependezwa na mauaji ya marehemu Mwangosi pale Iringa iwe ni mwanasiasa, mfanyakazi au mtumishi wa umma, mfanyabiashara au mwananchi mwingine yeyote.

  Napata shaka kuamini kama kundi fulani la watu linaguswa na mauaji yanayotokea mara kwa mara pindi chadema wanapokuwa wanaendesha maandamano yao. Kundi hilo ni viongozi wa chadema. Kwanini kila mara tukipata taarifa kuwa kuna mauji yamefanyika, kama kweli viongozi wa chadema wanakuwa mstari wa mbele, mbona sikuwai kusikia hata mmoja kupigwa risasi hata ya mguu, kila mara wanakufa watanzania hawa hawa wa kawaida? Vijana tusikubali kutumia maisha yetu nikimaanisha uhai wetu ili kubadili hali zetu za maisha, tusirudishe mifumo ya maisha ya kale katika ulimwengu wa KUPIGA KURA kumpata kiongozi unayempenda, tutumie haki hii vizuri sio miili yetu dhidi ya vyombo vya usalama. Yanatumika majina ya kishujaa kama vile Mpambanaji kwa vijana wanaopoteza uhai kwa maandamano yaliyofanywa kwa kuvunja utaratibu na maagizo ya mamlaka, kwanini na wao wasife kutuonyesha sisi sote kama kuuwawa kutokana na maandamano ya chadema kunamfanya mtu awe mpambanaji?

  Taifa linaitaji amani na utulivu ili wananchi wafanye shughuli zao za ujenzi wa taifa kila mmoja katika nafasi yake, sio kila siku yapangwe maandamano tu watu watafanyaje kazi zao kwa uhuru? Serikali iingilie kati swala hili na kukemea vikali shughuli zozote zinazoweza kusababisha uvunjifu wa amani, yakiwemo haya maandamano ya chadema, ijifunze kutoka kwa Mhe. January Makamba kupiga marufuku shughuli zao za movement ndani ya mkoa wa Tanga. Taifa linaitaji kupata ufumbuzi wa kudumu wa matatizo yaliyopo ila hawa chadema wanataka kuzua matatizo mapya nchini mwetu ya uvunjifu wa amani. "Hatutaki shari,tabu tulizonazo watanzania zinatutosha".
   
 10. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #10
  Sep 17, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,568
  Likes Received: 1,935
  Trophy Points: 280
  Mtu anaye halalisha mauwaji ya Mwangosi kwa namna yoyote ile,huyo ndiye aliyetiwa mfukoni.Halafu jinsi asivyokuwa na akili,anatoa reference ya mwalimu ambaye hakutaka chama chake kichafuliwe,na kufananisha na Slaa na Mbowe,si afadhali chadema ina wawili wasiotaka uchafu ndani ya chama if thats the case?

  Maana mwalimu Nyerere was an one man army,hakutaka uchafu wowote kwenye chama na wengine walidiriki pia kumwita dikteta!

  Hata alipostaafu bado sauti yake ndani ya chama ilikuwa kubwa na ndiyo maana Lowassa na JK hawakuwa marais kwenye uhai wake.

  Halafu eti huyu makala yake imetoka kwenye gazeti?Kweli Tanzania imekwisha!
   
 11. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #11
  Sep 17, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Pengine aliandika juzi.Hembu asome magazeti ya kesho ajue ni jinsi gani yupo "in the wrong side of History".
   
 12. Gobret

  Gobret JF-Expert Member

  #12
  Sep 17, 2012
  Joined: Jun 11, 2010
  Messages: 320
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Hivi wewe unayejiita mwandishi, haya unayotaka kutuaminisha unayafanya kwa manufaa ya nani kama sio CCM? Funguka, usiwe kama gunia la mkaa. Mh!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 13. Dumelambegu

  Dumelambegu JF-Expert Member

  #13
  Sep 17, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,052
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kuna mtu aliwahi kusema humuhumu jamvini kwamba magazeti ya New Habari Corporation kama Mtanzania ni kwa ajili ya wauza vitumbua na maandazi. Wakati huo sikumwelewa. Kwa tahariri hii, sasa nimeanza kupata picha vizuri zaidi. Hakika inatisha na nadhani hata kitendo cha kufungia vitumbua na maandazi magazeti ya mtanzania ni udharirishaji wa chakula. Ingefaa litumike cho-o-ni.

  Kama mtu anayejiita mwandishi wa habari anaweza kuandika utumbo namna hii na bila wasiwasi akaruhusu uchapishwe kwenye column nyeti kama hiyo ya tahariri, basi hatuna waandishi nchi hii. Ni upu-uzi mtupu. Mmmmhhh, hadi inatia kinyaaa, ptuuuuu!!!
   
 14. H

  Honolulu JF-Expert Member

  #14
  Sep 17, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 5,654
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ccm mwaka huu mna kazi! Hizi zote ni harakati za kujitawaza uchafu wa mauaji!
   
 15. Magu

  Magu Senior Member

  #15
  Sep 17, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 158
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kama watu watakumbuka vizuri kama kweli wana JF ni watu waliosoma vitabu huwezi msahau Yusph Halimoja, ni mwandishi mahili na wa siku nyingi na ndo mwandishi wa makala hii tunayojadili.

  Kwenye makala hii sioni tatizo, mwenzetu kaleta mada ya kujadili ikiwa na observation zake, hebu kama watu huku ndani ni wasomi wenye uelewa wa mambo hebu jadili kipengele kimoja kimoja ukipinga au kuunga mkono hoja.
  Ukisoma post nyingi hapa zilizokwisha za kupinga hapa zinakosa mashiko kwa sababu hatuna data za kutufanya tupinge hoja hii, mana wanasema ''kama huna data huna haki ya kuongea''
  Tusipende kutumia insictinct kwenye hoja ambazo zinahitaji tuwe na majibu sahihi yaliyofanyiwa tafiti, majibu yanayokuja hapa ni dhahiri mwandishi yuko sahihi mana mifano tunaiona hapa, badala ya kujibu hoja wengine wanatukana, tena matusi mabaya, kwa nini tusiamini haya yanayozumzwa na mwandishi.

  Wana jf tujifunze kujenga hoja na siyo kutumia matusi katika hoja
   
 16. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #16
  Sep 17, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Mhariri, its obvious kuwa Chadema kama wameshindwa kukuweka mfukoni, basi kuna aliefanikiwa kufanya hivyo. Manake hayo yoote uliyoelezea yanaonyesha chuki ya kutosha kutokana na kutokubaliana na hao mabwana katika masuala fulani fulani, siri mnaijua wenyewe endapo siri exists.

  Unakiri kuwa viongozi wa chadema hawakamatwi, lakini unaogopa kabisa kuwalaumu polisi ambao unahisi kuwa wana mpango maalumu wa kutokamata viongozi. Wewe kama mwandishi, aren't you loosing focus of what you should do? Not taking sides?! Ama unataka kutuaminisha kuwa kweli ni poli-CCM kama tunavyodhani? Haitakuwa sawa kusema na wewe polisi, ama boss wao ndio wewe unamfanyia kazi? Manake kwa marehemu Mwangosi ku-chit chat na mtu na kumuambia wasiwasi wake sioni kama it was such a big deal. Kwani mwandishi wa habari siku ya mechi ya simba na yanga akichat na mtu wa simba na kumtabiria ushindi, utasema kanunua mechi?

  Kinachoonekana zaidi kwenye macho ya wengi ni 'Police Brutality', kwa kutumia nguvu isiyo na kipimo kupambana na watu ambao hawana hata mawe mkononi! Kama hujaliona hilo basi aisee!

  Tasnia ya habari nchini inakufa kama mhariri ndo anahariri kwa staili hii! Ngoja tupate gas na uranium, wakubwa wagain interest waanze kutuandika!
   
 17. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #17
  Sep 17, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Hahaha! Kumbe na wewe mule mule! Haya edit na wewe hiyo edition yako manake inamuumbua nduguyo. Duh, mjini mipango.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. M

  Mzee Kipara Member

  #18
  Sep 17, 2012
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 83
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 15
  Hufai hata kuwa mwandishi wa jarida la chekechea, kwamba eti polisi walishamwona ni mfuasi wa chadema, tangu lini kuwa mfuasi wa chadema imekuwa ni kosa, tena kosa ambalo adhabu yake ni kufulumushwa utumbo kwa bomu? Ni bora kama una issues na Mbowe na Slaa ungeelezea hizo issues tu, au kama unajua kitu kuhusu kifo cha Wangwe ungesema unachokijua, lakini kujastify mauaji yanayofanywa na polisi unatia kinyaa.
   
 19. Dumelambegu

  Dumelambegu JF-Expert Member

  #19
  Sep 17, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,052
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Nimeshangazwa na mambo mawili kuhusiana na mwandishi wa hili gazeti la kufungia vitumbua:
  (1) Ameonyesha kuwa kifo cha Mwangosi kilikuwa ni halali kwani ushahidi upo unaodhihirisha kuwa kulikuwa na mawasiliano ya marehemu Mwangosi na kiongozi wa CHADEMA.

  (2) Chacha Wangwe aliuawa na viongozi wa CHADEMA ingawa hataki kueleza kwa undani aliuawaje!!

  Kwa ujumla, huyu mwandishi uchwara ana bifu na Mwenyekiti na Katibu wa CHADEMA ingawa hataki kuonyesha waziwazi.
   
 20. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #20
  Sep 17, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,568
  Likes Received: 1,935
  Trophy Points: 280
  Marehemu Chacha Wangwe(RIP), wakati wa mgogoro huo anaouzungumzia huyu kilaza "muhariri", sijui wa kitu gani,alikuwa na mawasiliano na Rostam Aziz(ushahidi wa kukutana chumbani kwenye hoteli huko Arusha ulikuwepo), licha ya uadui mkubwa waliokuwa nao chadema na fisadi yule aliyedai anaachana na "gutter politics",na pia humu kulikuwepo na member anayekwenda kwa jina la mgagagigikoko,pengine ndo yeye muhariri huyo, maana anasema ndo peke yake aliyekuwa akiyasapoti hayo ya marehemu.

  Marehemu alikuwa mpiganaji mzuri,lakini tatizo ni lile lile tu kama la wengineo ie Zitto,kukubali kutumika kwa kigezo cha demokrasia ama kauli kuwa "chama tofauti si uadui".

  Kama kuna wanachadema wanashirikiana na mafisadi,ama kupingana na mipango ya kimsingi ya chama ie vita dhidi ya wahujumu wa taifa na mafisadi,(fundamental issues),basi wana matatizo.

  Kama mafisadi wanapata mabilioni kwenye ufisadi,jiulizeni ni kivipi hawawezi kuzispend ili kuvuruga vyama vinavyohatarisha ulaji wao na pengine kuwaburuza kwenye mkono wa haki?

  Mwandishi huyu ni mchumia tumbo,kama ilivyo kwa kina RPC Kamuhanda na wengineo,andikeni majina yao hao,watakuja kuhojiwa na wao kuwa held accountable.Ukombozi utapatikana na no stone shall be left unturned.
   
Loading...