Mhariri Daily News kung'olewa, mwingine kutangazwa hivi karibuni

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
233

Habari nilizopata mchana huu kutoka kwa mwandishi mmoja mwandamizi wa gazeti la Serikali la Daily News zinasema kwamba kaimu Mhariri Mkuu wa gazeti hilo, Mkumbwa Alli anang'olewa kutoka wadhifa huo na badala yake kuwekwa mwingine ambaye atatangazwa si muda mrefu.

Huyu mpya atakauwa Mhariri Mtendaji moja kwa moja, na si kaimu tena kama alivyokuwa Mkumbwa Alli.

Habari zinasema Mkumbwa Alli atapangiwa kazi nyingine katika idara/taasisi nyingine ya serikali.

Wenye habari zaidi kuhusu tetesi hii watujuze.
 
Kwa taarifa yako anaweza akapandishwa cheo na si kuwa demoted kama wengi wetu tunavyotarajia. Unaweza kusikia ameukwaa ukuu wa wilaya!!!
 
Wamechelewa sana kumtimua. Huyu alitakiwa atimuliwe siku ya pili tu baada ya kuandika ile tahariri ya kipumbavu.
 
Wala hawamtimui. Labda wamegundua kuwa ile editorial yake aliiandika kwa kukurupuka. Hata hivyo ilikuwa inawasaidia. Watamweka mahali hadi baada ya uchaguzi wakishaiba kura wampatie ulaji zaidi. System ya kimafia huwa iko hivyo, haimtupi mtu hata wananchi wafanye kitu gani.
 
Nafikiri atateuliwa kuwa balozi. Si unajua haribu huku upelekwe kule maadam tu ni "mwenzetu"?
 
Jee, Mzee Mengi sasa hivi anaweza kufurahishwa na habari hii? Nasema hivyo kwa sababu kama mtakavyokumbuka lile sakata lake na Manji miaka minne hivi iliyopita kuhusu kashfa ya magodown ya Ubungo, Mkumbwa aliionekana kuwa upande wa Manji, hivyo kuzuka bifu kubwa kati yake (Mkumbwa) na Mengi.

Lakini sasa hivi tunaanza kuona jinsi Mzee Mengi anavyokula sahani moja na mafisadi, kutokana na msimamo ya vyombo vyake vya habari wakati huu wa kampeni.
 
Kama ni kweli, CCM itakuwa imetii maagizo ya CHADEMA.
kama hii ndio attitude basi hatufiki popote... maana anaweza hata mtu akafa tukasema "kama ni kweli basi mungu amesikiliza sala ya slaa"

i think the company has done justice kumuondoa mtu aliyepitiliza mamlaka yake
 
It's too late, damage already done. Hiyo transfer haitazuia serikali kuburuzwa mahakamani.
 
Jee, Mzee Mengi sasa hivi anaweza kufurahishwa na habari hii? Nasema hivyo kwa sababu kama mtakavyokumbuka lile sakata lake na Manji miaka minne hivi iliyopita kuhusu kashfa ya magodown ya Ubungo, Mkumbwa aliionekana kuwa upande wa Manji, hivyo kuzuka bifu kubwa kati yake (Mkumbwa) na Mengi.

Lakini sasa hivi tunaanza kuona jinsi Mzee Mengi anavyokula sahani moja na mafisadi, kutokana na msimamo ya vyombo vyake vya habari wakati huu wa kampeni.

Tujuze zaidi !
 
ngoja yusubiri, ila jk hawezi kumtupa lazima apewe, au apangiwe kazi nyingine.
 
kama hii ndio attitude basi hatufiki popote... maana anaweza hata mtu akafa tukasema "kama ni kweli basi mungu amesikiliza sala ya slaa"

i think the company has done justice kumuondoa mtu aliyepitiliza mamlaka yake

Ni kweli not everything has to be related to someone
 
Jee, Mzee Mengi sasa hivi anaweza kufurahishwa na habari hii? Nasema hivyo kwa sababu kama mtakavyokumbuka lile sakata lake na Manji miaka minne hivi iliyopita kuhusu kashfa ya magodown ya Ubungo, Mkumbwa aliionekana kuwa upande wa Manji, hivyo kuzuka bifu kubwa kati yake (Mkumbwa) na Mengi.

Lakini sasa hivi tunaanza kuona jinsi Mzee Mengi anavyokula sahani moja na mafisadi, kutokana na msimamo ya vyombo vyake vya habari wakati huu wa kampeni.
Kweli Mzee yuko mstari wa mbele kupiga vita ufisadi, ila pia usijeshangaa, hata yeye mwenyewe sio msafi kihivyo unavyomdhania, naye ana yake, muda muafaka ukifika, yatafumka na utamjua who he really is!
 
Back
Top Bottom