Mhariri aliyesema DR. SLAA WILL NEVER BE A PRESIDENT yuko katika msukosuko! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mhariri aliyesema DR. SLAA WILL NEVER BE A PRESIDENT yuko katika msukosuko!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by The Informer, Jan 4, 2011.

 1. T

  The Informer Senior Member

  #1
  Jan 4, 2011
  Joined: Jun 14, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkumbwa Ally, deputy managing editor (DME) wa Tanzania Standard Newspapers (TSN), kampuni inayochapisha magazeti ya serikali ya Daily News, Sunday News na Habari Leo, yuko katika msukosuko mkubwa.

  Mkumbwa kwa muda mrefu sasa amekuwa akikaimu cheo cha Acting Managing Editor (ME) wa TSN baada ya ME wake, Isaac Mruma, kuondolewa kwa mazingira ya kutatanisha. Mruma sasa hivi amesharudi Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA) alipotoka baada ya kusota muda mrefu alipoenguliwa TSN.

  Hivi sasa kuna mgawanyiko mkubwa wa wafanyakazi wa TSN huku wakiwa wametengana wale wa Mkumbwa na wale wa Mruma. Mkumbwa analaumiwa kwa upendeleo kwa baadhi ya wafanyakazi na kuwa na chuki binafsi na wengine, yaani ubaguzi wa wazi.

  Wadau wa TSN wanasema kuwa Mkumbwa amekuwa akifanya lobbying kupitia marafiki zake, Sethi Kamuhanda (katibu mkuu wa wizara ya habari) na Charles Kizigha (mwandishi mkongwe wa TSN anayedaiwa kuwa na connections na vigogo serikalini) ili yeye ateuliwe na Kikwete kuwa ME wa TSN. Wanasema amefikia pia kutumia waganga wa kienyeji na kuwaleta ofisini ili akipate cheo hicho.

  Hivi majuzi, Bodi ya TSN chini ya uenyekiti wa Wilson Mukama, imeamuru kuwa TSN itoe matangazo ya kazi kwa nafasi za ME na DME ambapo qualifications za vyeo vyote hivi viwili zinamuengua kabisa Mkumbwa.

  ME anatakiwa kuwa na post graduate ya business administration, preferrably MBA, na DME anatakiwa kuwa na at least first degree ya journalism/mass communication.

  Mkumbwa ana diploma tu ya journalism, hivyo yuko hatarini kupoteza mpaka hiyo nafasi yake ya sasa ya DME.

  Wapasha habari wa TSN wanasema kuwa Mkumbwa kuona hatari kubwa iliyopo mbele yake akazuia matangazo ya DME na ME yasitoke kwenye gazeti.

  Badala yake, ametoa matangazo ya nafasi nyingine kama Management Accountant, Assistant Procurement Officer, Customer Service Officers, Key Account Executive, etc, kujaza nafasi za wafanyakazi kibao waliokimbia TSN kutokana na uongozi wake mbovu.

  Mwenyekiti wa Bodi ya TSN, Wilson Mukama, inasemekana kuwa amekasirishwa na kitendo cha Mkumbwa kuzuia matangazo ya nafasi za DME na ME yasitoke kwenye gazeti na leo ameitisha emergency board meeting.

  Tunatarajia wenzetu wa TSN watupe habari zaidi baada ya kikao hicho cha dharura cha bodi.

  Mkumbwa amekuwa akijitamba kuwa anammudu vyema Mwenyekiti wa Bodi wa TSN Mukama kwa kuwa anakunywa naye pombe sana kwenye bar ya Jolly Club iliyopo Upanga (drinking buddy).

  Ifuatayo ni ile famous editorial aliyowahi kuiandika Mkumbwa kuhusu DK. SLAA:

   
 2. Kaduguda

  Kaduguda JF-Expert Member

  #2
  Jan 4, 2011
  Joined: Aug 1, 2008
  Messages: 670
  Likes Received: 281
  Trophy Points: 80
  Za mwizi arobaini!
   
 3. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #3
  Jan 4, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,473
  Likes Received: 5,852
  Trophy Points: 280
  Si arudi UwT?
   
 4. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #4
  Jan 4, 2011
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,471
  Likes Received: 1,421
  Trophy Points: 280
  Alichezea maji yenye mamba wengi wenye uchu, cheza na CCM sio DR. SLAA
   
 5. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #5
  Jan 4, 2011
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  With due respect; title ya thread inataka kuonyesha kuwa hii misukosuko iliyomkuta Mkumbwa imetokana na ile Editorial yake kwamba 'Dr. Slaa will Never be President?'
   
 6. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #6
  Jan 4, 2011
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,506
  Likes Received: 2,749
  Trophy Points: 280
  Yaani baada ya miaka takribani 50 ya uhuru, ME wa gazeti la serikali anaweza bado kuwa na diploma tu!!! Huyo jamaa inatakiwa apigwe buti arudi mtaani kukusanya habari siyo kukalia hicho kiti.
   
 7. Profesy

  Profesy Verified User

  #7
  Jan 4, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 380
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  du.
   
 8. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #8
  Jan 4, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,473
  Likes Received: 5,852
  Trophy Points: 280
  Utakuta Diploma ni ya DPRK au Jugoslavija
   
 9. kiraia

  kiraia JF Gold Member

  #9
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 1,614
  Likes Received: 268
  Trophy Points: 180
  Kumbe ana diploma tu.
   
 10. KIPANYA

  KIPANYA Member

  #10
  Jan 4, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  ni kweli mkbwa:eek:
   
 11. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #11
  Jan 4, 2011
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,204
  Likes Received: 264
  Trophy Points: 180
  Aondoke tu. siku zote debe tupu haliachi kutika. ile tahariri yake ilimvua nguo kabisa na kuonyesha kwamab yeye ni Mr zero. Kuna watu huwa wanandhani kwamba watadumu milele kwenye nafasi zao. Hana tofauti na Salva
   
 12. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #12
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,792
  Likes Received: 1,337
  Trophy Points: 280
  Serikalini kuna mambumbu na Vihiyo wengi tu.

  Hao hawana vision ya kuongoza vyombo vya serikali.

  Wajifunze kwa yaliyomkuta Tido Muhando


  Tupa kapuni. Hana Elimu,Experience pia imeproove Failure, Piga Chini
   
 13. M

  Marigwe JF-Expert Member

  #13
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 226
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Na mimi nakazia Slaa hatakuwa Rais wa Tanzania. Never!!Never!!Never!!
   
 14. E

  EL+RA=UFISADI Member

  #14
  Jan 4, 2011
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 56
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sawa mama Marigwe, endelea kuimba ngonjera
   
 15. Not_Yet_Uhuru

  Not_Yet_Uhuru JF-Expert Member

  #15
  Jan 4, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  Huyu Mkumbwa ataangukia pua, na ajue kuwa ki-demokrasia ameshafutika na kuliondoa gazeti lao ktk media zenye credibility, iwe ya ndani ya nchi au hata ya Tanzania.

  Na moto aliouwasha ktk jamii hautazimwa na yeyote hadi mwenyewe umtafune. Alidhani 'nguvu ya Umma' ni ya kunyooshea kidole cha upofu na ukurutu wa kutetea wanaoanguka badala ya kusimamia ukweli! Tanzania siyo ya genge la watu wachache wanaoteteana kulinda uozo na upofu kama alivyofanya Mkumbwa.

  Lazima yeye ajue kuwa nguvu ya umma ipo kila mahali, hata ndani ya media anapofanyia kazi na ndiyo maana anatapatapa, na ndiyo itakayomtafuna na lazima ang'oke aungane na wengine (ambao si vizuri kuwataja hapa) aanze kutavanga mtaani kuomba hisani za Media zinazoongozwa na wenye akili na wanaojali maslahi ya nchi na sio kama yeye na diploma yake ya kujitafutia na amebaki kujikomba-komba na kujisifu ili apate kukubalika. Kwa upungufu aliouonyesha, kama ikitokea aipate nafasi hiyo ya ME, tufuatilie kwa makini; hii Kampuni itaelekea kufa.
   
 16. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #16
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,422
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  hivyo kuandika kosa lake ni kutokana na kukalia kiti kisichomfaa --- it was a priviledge!

  fagio hili linatakiwa kupita kote kwa wakurugenzi na wasimamizi wa chaguzi --- inawezekana they dont qualify!

  slaa is already my president! anaongoza kutoka moyoni mwangu!

  nawasilisha!
   
 17. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #17
  Jan 4, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  wacha ale laana yake. malipo ni hapa hapa duniani.

  wanatafuta ajira kwa shida, wakizipata wanaanza kujihisi Mungu-watu.
   
 18. d

  duche Member

  #18
  Jan 4, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa kama anaenda na waganga kufanya ulozi ofisini amechanganyikiwa. Ashindwe na alegee..:angry::angry:
   
 19. z

  zamlock JF-Expert Member

  #19
  Jan 4, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  yah hata mimi dk slaa ndy raisi na ananiongoza mimi kutoka moyoni mwangu sasa huyo anayesema awezi kuwa raisi wakati anawaongoza watanzania na wote wanamtegemea yeye
   
 20. N

  Njaare JF-Expert Member

  #20
  Jan 4, 2011
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 1,075
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135

  Na mimi ningekuwa na Diplomma ningeandamana kutaka NACTE wachunguze Uhalali wa hiyo diplomma. Tahariri yake haiwezi kuwa imetoka kwenye kichwa chenye diploma. Hata mtu wa std 7 anafikiria vizuri kuliko huyu.
   
Loading...