Mhando wa TANESCO afikishwa Kortini Dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mhando wa TANESCO afikishwa Kortini Dar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mgomba101, Oct 6, 2012.

 1. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #1
  Oct 6, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) aliyesimamishwa kazi, William Mhando, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, na kuondolewa bila kusomewa shtaka.

  Mhando alifikishwa mahakamani hapo jana kati ya saa 7:00 mchana na saa 9:00 alasiri, akiwa ndani ya gari aina ya Noah, chini ya ulinzi wa maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

  Kwa mujibu wa vyanzo vya habari ndani ya mahakama hiyo, Mhando alifikishwa mahakamani hapo lakini hakushushwa kutoka ndani ya gari kutokana na muda wa mahakama kufanya kazi ukiwa umekwisha.

  “Amefika hapa akiwa ndani ya gari aina ya Noah, lakini hakushushwa, zaidi mtu mmoja alishuka ndani ya gari hilo na kuingia kwenye mahakamani na kutoka, kisha akarejea kwenye gari na kuondoka, wamekuja muda wa mahakama ukiwa umeisha,” kimebainisha chanzo hicho.

  Julai mwaka huu, Mkurugenzi huyo alisimamishwa kazi na bodi ya wakurugenzi ya shirika hilo ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za ubadhilifu na matumizi mabaya ya madaraka katika shirika hilo.

  Taarifa za kusimamishwa mkurugenzi huyo zilitolewa na bodi hiyo na kusainiwa na mwenyekiti wake, Jenerali Mstaafu Robert Mboma.

  my take! zitto kabwe na Ole sendeka wakamtetee mhando mahakamani kama walivyofanya bungeni
   
 2. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #2
  Oct 6, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Na wale wabunge wenye tuhumu za rushwa kwenye kamati ni nishati na madini zikiwa za kweli nao wafikishwe mahakamani.

  Recall: zitto kabwe alitaka kuunda kamati ndogo ya POAC ili kumsafisha mhando,,,sasa ni wakati muafaka zitto kujitokeza hadharani na aombe radhi watanzania kwa jitihada zake za kutaka kumsafisha Mhando:photo::lol::nerd::spy:
   
 3. Jay One

  Jay One JF-Expert Member

  #3
  Oct 6, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 11,075
  Likes Received: 4,658
  Trophy Points: 280
  Zitto naye yumo ktk ulaji huo.... IPTL mafuta mazito ususahau ile ilikuwa tender fake ili wauze mafuta wanakata makusudi umeme.... Kila mwezi Tanesco ilikuwa inailipa IPTL Tshs 6 bil of which hata yale mafuta wanawasha Generator moja tu then wanawapigia jamaa wa dams wanarudisha maji umeme unaendelea kama kawa....
  Mhando in his account aliyofungua miezi michache ilikutwa kaweka tsh 800mil... kutoka Tanesco.... Mwizi mkubwa huyu....source Waziri wa Nishati na Madini last Bunge....
   
 4. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #4
  Oct 6, 2012
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Jamani JF,tuko nyuma siku hizi naona tunapata habari mfuuuuu, hatuwi wa kwanza tena! vipi jamani?
   
 5. Marire

  Marire JF-Expert Member

  #5
  Oct 6, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 11,420
  Likes Received: 259
  Trophy Points: 180
  Huwa wanaishia kufikishwa mahakamani na hukumu ikitoka analipa faini na mchezo unaisha!
   
 6. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #6
  Oct 6, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  Patamu hapa. Zitto nahisi kama kakalia kuti kavu
   
 7. nitonye

  nitonye JF-Expert Member

  #7
  Oct 6, 2012
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 7,167
  Likes Received: 508
  Trophy Points: 280
  Habari yenyewe ilivyokaa ni ngumu kuipata coz hata mtuhumiwa hakutoka ndani ya gari hivyo kuwepo ugumu wa kupata habari.
   
 8. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #8
  Oct 6, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Duu!! Haya maisha ni noma, juzi tu Mhando alikuwa 'mtu muhimu' sana pale tanesco, lakini leo anapanda karandinga...
   
 9. Ngalangala

  Ngalangala JF-Expert Member

  #9
  Oct 6, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 312
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Hawa takukuru hua wanafanya makusudi kumleta mtuhumiwa late hours mahakamani ili asipate dhamana. mzee Mhando kalala keko hadi jumatatu kudadadeki...
   
 10. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #10
  Oct 6, 2012
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Nakubaliana na wewe, lakini hata issue ya TanTrade nayo tangu J3!

   
 11. THE BIG SHOW

  THE BIG SHOW JF-Expert Member

  #11
  Oct 6, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 13,926
  Likes Received: 1,853
  Trophy Points: 280
  IF A crockdile fail to handle a fight in the land it runs back to the water,because there in the water is where it wil at its strongest...!!pls excuse my language n grammar
  i think zitto must come to chama chetu cha mapinduzi kinachokula nchi,,chuki ya slaa na mbowe kwake imepanda juu sana
  maji yameshamwagika tena hayazoleki,,,people"s power kwishney...!!
  we r too strong to be slaves of politicians,hiv hatuwez ijenga nchi bila politics??i hate this game..:smash::smash:
   
 12. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #12
  Oct 6, 2012
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Ndio maana ya madaraka, ni natamu ila kama ukiyatumia vibaya, unaondoka vibaya....angalia akina saadom hussein, gadafi, walikuwa na kila kitu, wangetawala kwa vipindi kisha wakatoka, si wangekuwa na heshima?

   
 13. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #13
  Oct 6, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Takukuru? Mhando atashinda kesi
   
 14. Z

  Zimamoto JF-Expert Member

  #14
  Oct 6, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 464
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Wakati mwingine mahakamani ni sehemu ya kusafishia mafisadi ili wakaendelee kula walivyolimbikiza. Kwenye sheria si lazima kuwe na haki bali umahiri wa kucheza na vifungu.
   
 15. Borat69

  Borat69 JF-Expert Member

  #15
  Oct 6, 2012
  Joined: Jun 17, 2012
  Messages: 2,536
  Likes Received: 1,220
  Trophy Points: 280
  Mkuu, habari inasema kaletwa mahakamani na NOAH. Sasa Hilo karandinga umelitoa wapi? Au NOAH ndio makarandinga ya mafisadi siku hizi?
   
 16. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #16
  Oct 6, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 24,993
  Likes Received: 37,680
  Trophy Points: 280
  Mbona Jairo hapandishwi kizimbani au kwakuwa hata PM alifaidika na makusanyo yake ya kienyeji.Nakumbuka nae alisani ile posho kutoka ktk fungu harama la Jairo.

  Mkuu wa kaya tupe ufafanuzi wa hii double standard ya serikali yako.

  Mhando na Jairo nani alitangulia kufanya makosa!

  Au ndio uchunguzi unaendelea?

  Nahisi huyu mmoja alikuwa na baraka fulani kutok juu kabisa na ndio maana anapeta.

  Nchi hii kosa la kiufundi ni kula peke yako bila kuwashirikisha au kuwagawia wakubwa.
   
 17. Kennedy

  Kennedy JF-Expert Member

  #17
  Oct 6, 2012
  Joined: Dec 28, 2011
  Messages: 11,312
  Likes Received: 2,973
  Trophy Points: 280
  Wote wameoza na kupungukiwa Utukufu wa MUNGU.
   
 18. m

  mpigauzi JF-Expert Member

  #18
  Oct 6, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Inashangaza nchi hii, watuhumiwa wakubwa wanaachwa na kulindwa hivihivi. Munde na wenzake kwa nini hawajakamatwa na kusimamishwa ubunge?
   
 19. Cheche Mtungi

  Cheche Mtungi JF-Expert Member

  #19
  Oct 6, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 2,487
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Jela hakuna mwenyewe,lakini kwa kuwa ametangulia,Tunaomba akampe Hi Babu SEA!
   
 20. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #20
  Oct 6, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Mijitu mengine bana habari nzuri comment mbaya kama umepiga viroba
   
Loading...